January Makamba: Mbunge wa aina yake

Status
Not open for further replies.
Huyu kijana anaweza kuwa tishio zaidi ya Rostam. Rejea waraka wa dada yake kwa Barrick. Tujitahidi kumpinga kwa nguvu zote.

ndio january ni fisadi mbaya sana mwenye majungu kupita maelezo, ila pia waziri ngeleja ameamua kummaliza kisiasa pamoja na ridhiwani baada ya january kugeuka kuwa msemaji mkuu wa wizara hiyo. hawa jamaa kuna skandal mmoja ya kichinichini ambayo itafichuka karibuni ya huyu mwamvita...........subirini mtaiona
 
Kutoka katika facebook ya January Makamba....


Dakika 5:20. "Matatizo... mengine ni kuhusu uzalendo na rushwa yaliyomo kwenye sekta, ni jambo ambalo ni kubwa na lazima tulizungumze. Kwamba sasa hivi kabla ya kuleta mradi wa umeme lazima uzunguke uzunguke, uongee na watu, ugonge milango. Sasa hayo mambo lazima sasa haishe kama sehemu ya jawabu la kumaliza tatizo la umeme"




Dakika 0:05; "Leo ukisema ubadilishe gari, hamna mtu atayeenda Ikulu pale na briefcase ina Umeme. Huo ndio ukweli. Kwahiyo...kwahiyo kikubwa, haya matatizo yetu kama Watanzania, tuyazungumze..kama hivi tunavyoyazungumza, kwa ukweli na uwazi."




Dakika ya 7:50: "Ni afadhali kutokuwa Waziri kuliko kuwa Waziri ambaye kauli zako haziaminiki."




Dakika ya 0.40: "Mimi nipo katika Chama Cha Mapinduzi kama unavyojua...ni kiongozi tu mkubwa wa Chama. Lakini sisi tumekula kiapo kusema ukweli daima...watu wengine huwa wanashangaa, wanauliza hivi wewe mbona unasema kama vile sio CCM? Nasema, ninavyosema ndio hasa kama CCM. Kwasababu Serikali tuliyoiweka inabidi tuisimamie, hawa jamaa tuwasukume ili sisi tukirudi kwa wananchi, tuwe na chakusema."

 
Last edited by a moderator:
Professional Fisadi in action!! Anaendeleza kazi ya baba yake!

Ndugu uwezo tunao, maono yako nayachukulia kwa umakini wa hali ya juu!
 
SELEMANI,

Hebu kwanza kajipe japo kamuda ili uweze kumeza japo ka-fundo late. Siku zote mtu ukiwa na hoja nzuri utakuta kwamba wala hulazimiki kutumia maneno mengi sana wala nguvu kiasi hicho kulitete. Pumzika kidogo kwanza, mwe!!!!!!

Mbona Jihadi hivyo kumtetea shujaa wako Januari Makamba???????

Nilikuwa najaribu kughamua nini chachu ya huu uzandiki wako. Kwanza nilidhania ni wivu wa kawaida katika maisha yetu. Comment yako hii imenipa mwangaza kumbe ni zaidi ya hilo.......Pole kaka lakini ndio hivyo inabidi ujifunze kuvumilia kuishi Tanzania moja na wanaopaswa kuwa mashehe ubwaba ambao wameamua kujivua hilo gamba na kuwa zaidi ya hapo....pole sana kaka
 
Wana Makamba wanachukiwa kutokana na tabia zao chafu za kifisadi, kimbelembele na majungu....

Sounds like chuki binafsi...jipange na wewe utashinda na kuwa superstar......nafasi bado ipo ukiamua utashinda....
 
Riz1 syo baba yako, hacha kuropoka. Riz ni maji marefu hacheni majungu yenu. Kwa lipi amfanyie majungu kilaza January na dada yake. Tafuten ya maana kusema, mbuzi nyie. Mmeajiriwa na nyie nini? Wanakamba wanafaa kutoswa baharini hawafai

Samahani. Nawajua wote watatu hawa. Ridhwani, January na Mwamvita. Nadhani uwe makini unapojiingiza katika masuala ya nani kilaza nani kipanga. Lakini zaidi hizi siasa za wapita njia kuwagombanisha hawa watatu kamwe hazitafanikiwa. Kama anapodai Lowassa...uhusianao wao haujaanzia barabarani.....
 
Unajua tatizo la mfumo dume kama wetu ni mbaya sana. Mwanamke akifanya kazi na kupanda chati watu wanasema lazima atakuwa anavua chupi. Na tatizo la mabaki ya ujamaa kwa WaTanzania ni kwamba mtu akiwa na strong work ethic, wabongo wanamuita kimbelembele. Sasa wewe unasema Mwamvita ana kimbelembele kila event ya Vodacom yeye yupo--but to us she is aggressive and works hard. In return she is sitting on Vodafone board in London, wakati wewe unapika majungu Jamii Forum. Its all in your perspectives. Ndio maaana Wakenya and non Tanzanians are taking all executive positions in Bongo, kwa sababu ya kasumba ya WaTanzania kuchonga mnoo, ukiona wenzako wanafanikiwa. Wewe Mwamvita piga mzigo, wenye macho na ubongo tunaona.

Well, u said January ana majungu na unadai alimpa barua Mama Shelukindo kuhusu Utumbo wa Jairo na Ngeleja. What u call majungu sisi wengine tunaita kupiga vita rushwa. Kama unavyodai January alimpa data Dr. Slaa kuhusu Riziwani--wewe unaona hayo majungu, sisi wabongo wa mtaani tunaona kijana ana uchungu na nchi. So, Uhuru1 mama, its all in your perspectives. You seem to have a personal hatred against Makamba, which is okay. Endelea kuweka hizo fake email online, au allegations zisizokuwa na ushahidi. Wenzako wanaendelea ku-achieve tangible results.

Acheni kusingizia ujamaa mlioukana miaka 25 na kukumbatia ukuwadi wa ubepari. Iweje maumivu yanayotakanayo na mfumo wa kifisadi wa soko huria yabebeshwe ujamaa mlioudhihaki na kuusaliti?

Vilevile hili jungu la kuwa January kumpa Mama Shelukindo masuala ya Jairo ni uzandiki wa kipumbavu kabisa.January huyu aliyemshinda Mzee Shelukindo leo hii amuamini sana Mama Shelukindo na zaidi kumpa nafasi mama huyo kujijenga kisiasa. Ni kwa akili ilidumaa kifikira tu ndio inaweza kuamini hili au kudhani jungu kama hili linaweza kufanya kazi.....
 
Inashangaza kweli kuona jinsi watu wawili watatu humu wenye IDs zaidi ya mbili kila mmoja wako bize kutumia nguvu nyingi mno kumsafisha Makamba na kashfa ya 'A MILLION DOLLAR EMAIL', sasa ngoja mkija kumwagiwa ya dola 10 mlioni kutoka NASDAQ mtaongea nini???

Mnaona mchezo wa kuigiza huu jamani? Tayari wapo jikoni kupika "skendo" mpya ya NASDAQ. Mtu yoyote hawezi kudai eti anapambana na "ufisadi" wakati yeye mwenyewe ni kinara wa uzushi na uwongo.

Kuhusu hiyo "skendo" ya "A MILLION DOLLAR EMAIL", wala huhitaji mtaalamu wa kugushi kwa mtu mwenye akili timamu kugundua kwamba hiyo email hapo juu ni feki...tena huna hata haja ya kusoma maudhui yenyewe yaliyoandikwa unajua ni feki. Kwanini nasema hivi?

1) Mtu kutumia email address ya kazini kuomba rushwa, na tena kutaja kiwango chenyewe cha hiyo rushwa haiingii akilini, sembuse tu kuandika kuhusu mambo binafsi tena ya kimapenzi. Ungetegemea kama ni kweli mtu huyu asingeacha "paper trail" ya aina yoyote.

2) Karatasi yake inaonekana imekunjwa-kunjwa, lakini maandishi yake yamebandikwa juu ya karatasi bila ya maandishi yenyewe kukunjika. Maneno yanaonekana kabisa kwamba yana kimvuli fulani ambacho kinatokana na jitihada za ku-copy and paste, au ku-fotokopi.

3) Formatting ya email inaashiria kabisa kwamba imekuwa typed kwenye Word document. Tazama indentation kwanzo kabisa wa email ambapo sentensi imeanzia kati kati, na mwisho kwenye sahihi ambapo jina limekuwa centred. Hii formatting haipo katika email etiquette wala katika programs kama MS Outlook au Lotus Notes.

4) Ukiprint email kawaida inatokea mistari fulani juu pamoja na jina la mwenye account, vitu ambavyo havipo hapa.
 
Huyu bwana uwezo wa baba yake nilikua siuelewi vizuri mostly alikua anaropoka tu sidhani kama atakuia nakipya zaidi ya baba yake amesomea hela hizohizo za wizi mwangalieni sana kwenye ishu ya uranium inayokuja hiyo ndo itakua hot kuliko richmond na dowans
 
...........ni kweli anajitahidi kutumia madhaifu ya chama chake lakini ukweli ni kwamba mfumo anatumia kufanya kazi ni ule ule wa kifisadi
 
BAADA YA KADHIA YA MISURURU YA UFISADI KATIKA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA NA RASILMALI ZA UMMA, SASA NI VEMA WADAU MBALIMBALI KUKAA NA KUTOA MUONGOZO WA JUMLA KITAIFA NA USIMAMIAJI WAKE NA WADAU NJE YA SERIKALI

Baada ya shutuma nyingi sana za UFISADI katika mambo ya uvunaji wa rasilmali zetu kupita kiasi, kughubikwa na USIRI kwa wachache na uundwaji wa mikataba mibovu kila kukicha, ni vema hivi sasa kila uwekezaji ama kwa umeme, gesi, wanyama pori au madini yakajibu vigezo kadha vikiwemo:

1. Wa-Tanzania watanufaika vipi MOJA KWA MOJA kutoka na uvunaji wa rasilmali zetu husika (manufaa ya sasa, ya kipindi cha kati, na kipindi cha muda mrefu kwa taifa letu)?

2. Wadau wa sekta nzima wamehusishwa kwa viwango gani katika kupitisha mkataba wa uwekezaji husika?

3. Wataalam wa kuanda mkataba na mchakato mzima umeendeshwa vipi (uwazi wa milango ya kusitisha, kuboresha au kuuvunja mkataba)?

4. Maoni ya kitaalam kutoka kwa taasisi huru juu ya uwekezaji na mambo ya msingi ya kuzingatia?

5. Faida kwa jamii itokanayo na eneo la kufanyika uwekezaji umewekwa vipi?

6. Ushikishwaji wa wazi wa wadau wote wa sekta husika juu ya upatikanaji wa mwekezaji / wawekezji.

7. Nafasi na vipaumbele kwa wawekezaji wazawa imezingatiwa vipi?

8. Nafasi ya asasi za kiraia na vyombo vya habari katika nchi.

9. Mikataba yote kuhusu uwekezaji NDANI YA MIPAKA YETU YA Tanzania kwanza zifungwe kwa kuzingatia sera na sheria zetu hivyo sera na sheria za kimataifa ziwe tu ni ziada tu katika mchakato mzima MPAKA PALE TU AMBAPO NI WAZI KWAMBA MISINGI YETU YA UTAWALA WA KISHERIA imedhihirika kuleta tija kwa washiriki wa mkataba husika.

10. Vigezo vya wazi juu ya ulipaji kodi.

11. Nafasi na ajira muhimu kwa Wa-Tanzania.

NB:
Hatutaki Kupatwa na kitu ufisadi NA MISTUKO YA MARA KWA MARA tena INAYOTUGEUZA kuwa TAIFA LA WALALAMIKAJI kuhusu miradi na au uwekezaji wowote katika mali ya umma hivyo USIRI NA KUTEMBEA NA MUHURI WA TAIFA MFUKONI bila vigezo maalum ikiwa ni pamoja na vigezo hivyo hapo juu iwe ni sababu tosha kwa Mtanzania yeyote yule, wanajamii na au taasisi kuweza kusukumwa kutafuta kusitishwa kwa mkataba husika.
 
Rizwan=future president of Tanzania
Makamba jr=Makamu wa rais

Hawa walibahatika kutoka kwenye familia zilio jiwahi hapa bongo, nyie wengine mtabaki na wivu wenu tu
 
mtoto wa simba naye ni simba, tusitegemee jipya kutoka kwa huyu kijana kwani ni wale wale tu wanaovaa mavazi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali.
 
mtoto wa simba naye ni simba, tusitegemee jipya kutoka kwa huyu kijana kwani ni wale wale tu wanaovaa mavazi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali.

Ungesema mtoto wa nyoka ni nyoka, ukimfananisha na simba unakuwa umempa ushujaa.
 
Mwakalinga unachanganya mambo. Hayo mambo ya Richmond sijui nini--hayajustify wewe kutuletea a copy of email which you know is fake.

Sasa kutuletea fake email ambayo imetengenezwa kwa nia ya kuwachafulia utu watoto wa watu sio ishu. Hizo ni chuki tu bhana. Usichanganye stori apa. Umeleta majungu jamvini, na tunakwambia hapana.

Jamaa kaleta email jamvini, katikati ya watu walioenda shule huwezi kusema tu fake bila kujutify kwa wanajamvi ufake wake. Huwezi kumconvice mtu yeyote humu ndani kwa kusema feki bila kutoa systematic reasons na explanations za ufake wa hiyo email.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom