[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]FAKE EMAIL CIRCULATING ABOUT THE MAKAMBAS......[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Written by Mange[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: createdate, colspan: 2"]Thursday, 20 October 2011 17:58[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Phony/fake email circulating about the makambas
Recently kuna email ambayo allegedly inatoka kwa Mwamvita kwenda kwa kibopa wa barrick ,Email inahusu Mwamvita kumuombea kaka yake rushwa.
Huu ni uongo na unyama usiokua na kipimo. Hivi mtu unakua na akili gani ukakaa ukatumia muda wako kutengeneza uongo kama huu?? Unafanya hivi ili iweje? Ni wivu? Chuki binafsi au ushetani??
Ni ngumu kufikiri kwamba watanzania wamefikia kiwango hiki cha kukosa utu. Ukweli siku zote unaonekana kuzidi uongo. Janaury ni msema kweli, mchapa kazi na mtu msafi. Kama hamna cha kuonyesha ndio mtengeneze?? Nimeguswa sana na jambo hili, na naomba wale wapenda haki waniunge Mkono kukumea vitendo vya kizindaki na vya kishenzi katika nchi yetu.
Nahakika, aliefanya jambo hili atajulikana na atawekwa hadhari in a very near future. Na kama ni wewe, be very scared.
I mean really hili jambo limenisikitisha sana. Mwamvita is a young woman that many young Tanzanian women are looking up to. Kwa nini mtu aamue tu kumchafua dada wa watu? Hivi kwani Mwanamke hawezi kushika nafasi nzuri nchi hii kwa kutumia usomi wake na ushapu wake? Kwa nini mwanamke akisha fika juu basi aanze kuchafulia na kuambiwa kafuka pale kwa sababu zisizo za msingi au anatumia nafasi yake vibaya?
Roho imeniuma sana juu ya hili jambo. Bora hata wangetengeza email wakamsema kaka yake January kaomba rushwa labda kidogo ingeeleweka ni yale yale mambo ya siasa za kishenzi za nchi hii. Sasa msichana wa watu hata sio mwana siasa nchini kwa nini atumike kumchafua kaka yake?
Alafu vitu vingine vinahitaji common sense tu kujua kama is this true or not. I mean kweli where in this world umewahi kuona mtu anaomba rushwa kupitia email ya kazini kwake jamani? Tena sio kuomba rushwa tu, na kuweka mapenzi humo humo. Really? Na email address ya ofisini kwako?
Anyways, Mwamvita would like to thank wengi wenu mliompigia simu na kumtumia email kumpa pole kwa hili jambo la kishetani lililofanya na walemavu wa akili na utu.
And shewould like all of you to know that, vita vya kipuuzi kama hivi against her and her family will never hold her back. And she would like all the other women to know that, we have to be strong in this men dominated world, na tusikubali kurudishwa nyuma na kitu chochote kile. Na anawashukuru mno kwa support yenu katika kipindi hiki kigumu kwake na familia yake.
And she would like to assure you that, the email was 100% percent fabricated na sababu kubwa ikiwa ni kumuharibia kaka yake kazi.
Anyways, mimi kama rafiki yake pia nimeumia sana. Kwa kweli its hard kuona ndugu yako au rafiki yako anakuwa bullied bila sababu. Tena ukizingatia hajamkosea mtu chochote. Dada wa watu sio mwanasiasa, anaamka zake asubuhi anaenda kazini,usiku anarudi nyumbani kulala hana shida na mtu. Sasa kwanini wanataka kumwaribia image yake? Au ni kwasababu ni mwanamke mwenye umri mdogo na kafika hapo alipofika?
SASA NAULIZA TANZANIA KWA SIASA ZA KISHEZI HIZI TUTAFIKA KWELI???
MANGE KIMAMBI
PS: Ka email kenyewe kame fojiwa na mtu ambae hata hajui photoshop/kufoji vizuri. hajui hata chini ya email za mwammy huwa kuna headers za kampuni zinatokeaga. Also any email ikiwa printed out inatokea na headersAny IT professional would look at that stupid email and laugh.hata wewe ukitaka unaweka kukaa kwenye word document yako and create it yani thats how poorely done it was.
alafu bora hata angeenda kutafuta mtu anaejua kiingereza lol...kaweka ma broken english humo ili mradi tu. Mwam haongei english kama hiyo,try harder next time.... and soon nakuumbua humu, be ready.....
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]