Januari Makamba na wengine wanusurika kwa ajali

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Na Charles Mwakipesile, Ileje

WASAIDIZI wa Rais Jakaya Kikwete jana walinurika kufa katika ajali Mbaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu la nyuma kushoto na gari hilo kuacha njia na kuserereka kwenye korongo.

Ajali hiyo ilitokea saa tano asubuhi katika kijiji cha Ikinga, Wilaya ya Ileje wakati msafara huo ukitoka Kyela kuelekea Shule ya sekondari ya Isange, mahali ambapo Rais Kikwete alitarajia kupokea taarifa ya wilaya na kuweka jiwe la msingi kwenye sekondari hiyo.

Gari hilo Toyota Landcruser lenye namba za usajili STK 3264 likiendeshwa na dereva Peter Makwale, liliacha njia likiwa katika mwendo mkali na kutumbua kwenye korongo lililokuwa jirani na makazi ya watu lakini hata hivyo halikupata madhara na lilisimama kama vile lipo barabarani.

Wasaidizi hao wa Rais wakiongozwa na January Makamba,walitoka salama bila majeraha yoyote na kuendelea na safari baada ya kupatiwa gari lingine Toyota Land Cruser namba STK 4744.

Akizungumza baada ya ajali hiyo, Makamba alimshukuru Mungu kwa kuwanusuru kwenye balaa hilo na kusema bila huruma zake, hali ingekuwa mbaya .

Naye dereva Makwale, alisema alijitahidi kuhakikisha analimudu gari hilo lakini kutokana na vumbi lililotanda barabarani na kupasuka gurudumu, alishangaa kujikuta amepaa na kutua kwenye korongo kubwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Zelotte Steven alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo hata hivyo, alisema wasaidizi hao wote walitoka salama na kuendelea na safari.
 
Poleni sana wasije wakasema ilikuwa JK ndio alitakiwa ikumkute maana ziara yenyewe ilikuwa na maneno mengii
 
Kaponea chupu chupu mkulu, at least anaweza kusema so he can't be hurt critically.

Lakini mbona uandishi wenyewe umekaa kama "Mtu mmoja na wamakonde wanne wanusurika kwa ajali"?
 
Tunashukuru maulana kwa kuwaponya, hasa wewe January ili walu ukamsaidie babako kisaikolojia baada ya kubwabwaja weeeeee huko TARIME akiashia kuangukia pua!
 
Na Charles Mwakipesile, Ileje

WASAIDIZI wa Rais Jakaya Kikwete jana walinurika kufa katika ajali Mbaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu la nyuma kushoto na gari hilo kuacha njia na kuserereka kwenye korongo.

Ajali hiyo ilitokea saa tano asubuhi katika kijiji cha Ikinga, Wilaya ya Ileje wakati msafara huo ukitoka Kyela kuelekea Shule ya sekondari ya Isange, mahali ambapo Rais Kikwete alitarajia kupokea taarifa ya wilaya na kuweka jiwe la msingi kwenye sekondari hiyo.

Gari hilo Toyota Landcruser lenye namba za usajili STK 3264 likiendeshwa na dereva Peter Makwale, liliacha njia likiwa katika mwendo mkali na kutumbua kwenye korongo lililokuwa jirani na makazi ya watu lakini hata hivyo halikupata madhara na lilisimama kama vile lipo barabarani.

Wasaidizi hao wa Rais wakiongozwa na January Makamba,walitoka salama bila majeraha yoyote na kuendelea na safari baada ya kupatiwa gari lingine Toyota Land Cruser namba STK 4744.

Akizungumza baada ya ajali hiyo, Makamba alimshukuru Mungu kwa kuwanusuru kwenye balaa hilo na kusema bila huruma zake, hali ingekuwa mbaya .

Naye dereva Makwale, alisema alijitahidi kuhakikisha analimudu gari hilo lakini kutokana na vumbi lililotanda barabarani na kupasuka gurudumu, alishangaa kujikuta amepaa na kutua kwenye korongo kubwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Zelotte Steven alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo hata hivyo, alisema wasaidizi hao wote walitoka salama na kuendelea na safari.

Tuwape pole kwa kunusurika na ajali hiyo ni miongoni ya kazi yake Muumba Pia wasijishau kwani MMungu alikwisha sema kila nafsi itaonja uchungu wa mauti sasa misuko suko kama hiyo inakuwa ni ukumbusho kwa yale yaliyokuwemo katika nafsi zetu zaidi ya wezetu
 
poleni ..mkulu kaaga ...hicho kibomu wazee wa busara wa mbeya walikuwa wanamjaribu...kahepa..., si ndio maana kila mara alikuwa akiahirisha ziara ..wataalamu wake walikuwa wanaviona hivi...,na as usual kwenye misafara yake kamati ya ufundi huwa haikosekani...

Poleni sana wazee..tunamshukuru mungu kwa ajili yenu...!
 
January Makamba na watu sita wanusurika kufa jalini.Kaazi kwelikweli.
 
Tunashukuru maulana kwa kuwaponya, hasa wewe January ili walu ukamsaidie babako kisaikolojia baada ya kubwabwaja weeeeee huko TARIME akiashia kuangukia pua!

Ooohh hivi kumbe n mtoto wa katibu mkuu wa chama cha mafisadi!! sikulijua hili
 
Back
Top Bottom