Janja ya Burundi imefichuka

Janja ya Burundi imefichuka

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,407
Reaction score
17,014
Siku zote nilikuwa nikijiuliza maswali mengi kichwani bila kupata majibu yake kuhusu ni kwa vipi nchi kama Burundi yenye migogoro mingi ya kiusalama inawezeje kutoa wanajeshi wake wengi kwenda kuzisaidia nchi nyingine kurejesha amani yao badala ya kusalia nchini mwao kuimarisha amani ya nchi yao kwanza?

Kumbe nchi hizi huwa zinafaidika sana kwa kupitia mishahara wanayolipwa wanajeshi wao na UN au EU. Serikali hizi zinalazimisha mishahara ya wanajeshi wao ilipwe kupitia serikali za nchi zao ili 'kuipiga panga' kwanza kabla haijawafikia walengwa.

Inasemekana UN na EU inawalipa wanajeshi wa kulinda amani takribani mara 26 zaidi ya mishahara ya Burundi kwa US dollar.

Baada ya UN na EU sasa kung'amua janja hii na kutaka kuwalipa wanajeshi wenyewe moja kwa moja mifukoni mwa, weeee!, jamaa sasa wanatishia kuwarudisha nyumbani wanajeshi wao kwakuwa haitakuwa na maana kwao tena.

Huu ni unyonyaji wa hali ya juu kwa watoto wa watu kugeuzwa kitega uchumi na wanasiasa.
 
Siku zote nilikuwa nikijiuliza maswali mengi kichwani bila kupata majibu yake kuhusu ni kwa vipi nchi kama Burundi yenye migogoro mingi ya kiusalama inawezeje kutoa wanajeshi wake wengi kwenda kuzisaidia nchi nyingine kurejesha amani yao badala ya kusalia nchini mwao kuimarisha amani ya nchi yao kwanza? Kumbe nchi hizi huwa zinafaidika sana kwa kupitia mishahara wanayolipwa wanajeshi wao na UN au EU. Serikali hizi zinalazimisha mishahara ya wanajeshi wao ilipwe kupitia serikali za nchi zao ili 'kuipiga panga' kwanza kabla haijawafikia walengwa.
Inasemekana UN na EU inawalipa wanajeshi wa kulinda amani takribani mara 26 zaidi ya mishahara ya Burundi kwa US dollar.

Baada ya UN na EU sasa kung'amua janja hii na kutaka kuwalipa wanajeshi wenyewe moja kwa moja mifukoni mwa, weeee!!!, jamaa sasa wanatishia kuwarudisha nyumbani wanajeshi wao kwakuwa haitakuwa na maana kwao tena.

Huu ni unyonyaji wa hali ya juu kwa watoto wa watu kugeuzwa kitega uchumi na wanasiasa.
Hivi vinchi vyetu kazi kutunisha mabega tu ujanja wetu mdogo sana kwa kuwa ni tegemezi kwa mataifa makubwa 100%; mwangalie Mugabe katunisha misuli sasa wanakula jalalani wazimbabwe!
 
uchunguzi makini sana huu , nainaonekana kwa hivi majuzi tu UN ilipo mfukuza kamanda wa kikenya aliyeshindwa kulinda raia wa Somalia , na nchi ya Kenya ikaonya kuwatoa wanajeshi wake Somalia kumbe wanalipwa halafu hawataki kusimamiwa na boss wao
 
Mkuu isn't Somalia.It's South Sudan.
 
Back
Top Bottom