kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,745
Nilikuwa nasikiliza hotuba za vyama vilivyoungana dhidi ya chama tawala sasa hivi lakini imebidi nizime radio na kuelekea kwenye kanywaji, kwa vile sikuweza kuvumilia derogatory language ya huyu Mh. Tundu Lissu.
Katika kueleza mchakato wa yale yaliyojiri alikuwa akitamka, tena bila aibu, staha wala ustaarabu kuwa amekuwa akiongea na miCCM, maCCM na kwa ujumla kwa kutmia lugha isiyostahili kwa mtu msomi, tena aliyeheshimiwa kupewa dhamana ya kuingia bungeni kwawakilisha wananchi kwa kupitia jimbo lake la uchaguzi.
Pengine Msajili wa Vyama inabidi amkumbushe huyu jamaa kuwa derogatory language haijengi na yule uliyemkusudia akiamua kurudisha matusi basi amani inaweza kuwekwa rehani.
Kwa mtaji huu , Lissu anaingia katika wanasiasa wasio na ustaarabu wa kuelezea yale yaliyo moyoni bila kutumia dharau, matusi n.k.
No wonder humu JF , si ajabu yeye ni mmoja wa wanaoutumia matusi kujieleza.
Nawasilisha.
Na mimi naendela kukuambia ni ujinga kuendelea kuyashabikia maCCM, ebu naomba nikuulize pale mwigulu alipotamka kuwa haongei na Mbwa anaongea na Mfuga Mbwa, na isitoshe huyohuyo Mwigulu wakati ule Kafumu ametangazwa kushinda ubunge kule Igunga alitamka hadharani kuwa CCM wamepiga Mbwa na Mfuga Mbwa na baada ya hapo akaenda Iramba akamvesha Mbwa Bendera ya CHADEMA katika matukio haya wewe unayejifanya kuguswa sana na kauli zisizo za Kistaarabu kuna chochote ulichangia kupinga haya aliyoyafanya Mwigulu?