Janga la ukame/ njaa life fundisho kwa serikali ya Tanzania ili itengeneze irrigation schemes.

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Katika nchi ya E.Africa imebaki Tanzania pekee ambayo haina Government irrigation schemes za kisasa. Hapa naongelea kilimo cha umwagiliaji ambacho maji yanavutwa kutoka kwenye chanzo kikubwa na kuelekezwa kwenye mashamba makubwa au maeneo makubwa yenye ukame yaliyoko mbali na vyanzo vya maji.

Kama kwenye picha hapa chini.
5af416452df83a3cdff2e220d066aec0.jpg
96502daf27aa117c6ca6e044876b266e.jpg
901e213fa06a30950e02a1689a2a5eb7.jpg

Hatuwezi kuwa tunategemea mvua miaka yote. Wenzetu wanakuwa na uhakika wa chakula bila kujali uwepo wa mvua.

Serikali inabidi iangalie uwezekano wa kuweka hizi irrigation schemes katika maeneo mbalimbali kama vile shinyanga kuna maeneo mazuri ya kulima mpunga lakini hakuna maji.

Naomba kuwakilisha hoja.
 
Umeongelea scheme bila utunzaji wa mazingira. ....mvua zingenyesha kama kawaida kama watu wasingeharibu mazingira kwa ukataji miti
People are thinking of solns , you still thing of blaming. Poor tanzanians
 
Tanzania tulizoea kutambikia mvua tuache hizi tamaduni za kizamani.
 
Hili ni kosa kubwa sana ambalo serikali yetu bado inalilea, sijui tunashindwa nini kutengeneza irrigation scheme tukasaidia watu wetu... Karne ya 21 bado tunastruggle na njaa na tuna mito, maziwa, bahari nk..

Watu wetu wananguvu sana za kulima na wanajitahidi sana kulima kwakweli, lakini kinachowaangusha ni kutokuwa na uwezo wa kilimo cha kisasa...
 
Umezungumza jambo moja la msingi sana, lakini watunga sera wapo mjini wanapata chakula kwa bei ya kutupa huku wakulima wakiendelea kuwa maskini. Tanzania imeendelea kuwa maskini kwani zaidi ya 70% ni wakulima tena wengi wao wanategemea mvua. Watunga sera wao wako mijini na kinachowasumbua ni mambo ya mjini na sio kilimo. Sisi wakulima wenye nia kidogo ndio tunajitahidi kulima kwa miradi midogo ya kumwagilia na bado tunakutana na changamoto ya soko. Wakati mwingine nashangaa kusikia maneno kupigania wanyonge huku kilimo kikipewa kisogo. Kama serekali haitowekeza kwenye kilimo tena cha umwagiliaji hivyo viwanda itakuwa ni ndoto na hata vikijengwa vitageuka magofu kwa kukosa malighafi.
 
Hizi scheme nadhan zipo kwenYe mabonde mengi tu nimeona moja hapo ruvu
Hapana mkuu. Usifananishe zile za watu binafsi. Kwa nchi za wenzetu unakuta serikal inatoa maji ziwa victoria inampeleka kama dodoma sehemu maalumu ambya kunakuwa na wakulima wadogowadogo wanagawiwa plots.
 
Ok tusubir halimo labda KwenYe ilani Ya chama
 
Mbona hizi zipo? Au private owned hazitambuliki? Niliona moja yenye kufanana na picha ya tatu huko Ifakara katika kijiji cha Mgudeni! Project yao ilikuwa ni kwenye mpunga ila wameanza pia na kulima mahindi wana kama miaka miwili wanalima mahindi. Mwaka jana nilipitapo mwezi wa Tisa nikakuta wamestawisha mahindi yalikuwa yamestawi vizuri sana!

Kama tukiwa na project kama hizo in a large scale njaa Tanzania itabaki kuwa yakusikia kwa majirani tu.
 
Naongelea miradi ya serikal kuwwzesha jamii.
 
Katika nchi ya E.Africa imebaki Tanzania pekee ambayo haina Government irrigation schemes za kisasa. Hapa naongelea kilimo cha umwagiliaji ambacho maji yanavutwa kutoka kwenye chanzo kikubwa na kuelekezwa kwenye mashamba makubwa au maeneo makubwa yenye ukame yaliyoko mbali na vyanzo vya maji.

Kama kwenye picha hapa chini.
5af416452df83a3cdff2e220d066aec0.jpg
96502daf27aa117c6ca6e044876b266e.jpg
901e213fa06a30950e02a1689a2a5eb7.jpg

Hatuwezi kuwa tunategemea mvua miaka yote. Wenzetu wanakuwa na uhakika wa chakula bila kujali uwepo wa mvua.

Serikali inabidi iangalie uwezekano wa kuweka hizi irrigation schemes katika maeneo mbalimbali kama vile shinyanga kuna maeneo mazuri ya kulima mpunga lakini hakuna maji.

Naomba kuwakilisha hoja.
Kweli
 
Back
Top Bottom