PreGE2025 Janeth Rithe: Wanawake msimchague tena Rais Samia, haoni dira mbele yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa kupitia chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe, ametaka Wanawake nchini kutomchagua tena Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi ujao, akidai kuwa kiongozi huyo mkimuangalia "amechanganyikiwa".

Pia, Soma: Polisi wafika Ofisi za ACT Wazalendo kumkamata Janeth Rithe kwa agizo la ZCO

Kauli hiyo ameitoa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ubungo, tarehe 18 Juni 2025

"Ndugu zangu Wana Ubungo na Watanzania kwa ujumla, Nchi yetu imejaa na Majonzi na Masikitiko mengi na hata ukituona tunavyotembea wote tumejawa na majonzi na masikitiko"

"Haki yetu ya msingi inaporwa kila baada ya Uchaguzi toka mwaka 2020, lakini wanao-sababisha mambo haya yatokee ama uporwaji huu wa Uchaguzi ni CCM na dola la CCM"

"Sasa tunakwenda kwenye Uchaguzi mwezi wa 10, naomba Wanawake wa Tanzania, kila Mwanamke popote alipo ajue kwamba anajukumu la kupiga Kura lakini pia anajukumu la kulinda."

"Wanawake tumetongozwa na CCM na sisi tumekubali, sasa hivi [...amesema Mwenyekiti wa Mkoa] watu wamegeuka kuwa Machawa nawaona Wanawake wakiwa wamevaa mavazi ya gharama na wanapita wakikwambia Samia tena Mitano 5"

"Nikiangalia ninashangaa Wanawake wa Tanzania, madhira makubwa tunayoyapata ni kutokana na Uongozi mbovu wa Chama cha Mapinduzi, madhira makubwa tunayo yapata ni kutokana na Uongozi huo huo wa Samia"

"Kwanza mimi na swali ambalo najiuliza, hivi hatuoni kama Samia anaenda kuongoza Miaka 15?. Amekuwa Makamu wa Rais kwa miaka 5, amekuwa Rais kwa Miaka 5 tena na sasa tunaenda kumpa 5 mingine. Hatuoni kwamba ameongoza kwa miaka 15 na amevunja Katiba.

"Na mkimuangalia amechanganyikiwa jamani, sasa mnaendaje kumchagua mtu aliyechanganyikiwa. Juzi katuambia eti Tanzania Uchumi umekuwa kuliko Marekani, hata kipofu na Kiziwi hili jambo akisikiliza anachanganyikiwa kabisa, ni namna ya Kiongozi aliyechanganyikiwa, ni namna ya Kiongozi ambaye haoni dira mbele yake, sijui kitu gani kinamchanganya, ndio maana CCM wamebakia kulindwa na Dola ama Polisi"

Utasikia kapewa kesi ama kavamiwa na wahuni wa watawala na kumbaka na vipigo juu!!
Tayari Abdul anakunywa alikasusi na anapaka mkongo. Maana anasakwa hatari.

Screenshot_20250620-145637.png
 
Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa kupitia chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe, ametaka Wanawake nchini kutomchagua tena Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi ujao, akidai kuwa kiongozi huyo mkimuangalia "amechanganyikiwa".

Pia, Soma: Polisi wavamia Ofisi za ACT Wazalendo kumkamata Janeth Rithe kwa agizo la ZCO

Kauli hiyo ameitoa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ubungo, tarehe 18 Juni 2025

Sio kwamba huyu ndio kachanganyikiwa?

By the way ni lini wanawake wakachaguana? Wanaume ndio tutamchagua na hivyo bibi amekazidi uzuri basi ndio kubinua midomo kutazidi 😁😁
 
Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa kupitia chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe, ametaka Wanawake nchini kutomchagua tena Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi ujao, akidai kuwa kiongozi huyo mkimuangalia "amechanganyikiwa".

Pia, Soma: Polisi wavamia Ofisi za ACT Wazalendo kumkamata Janeth Rithe kwa agizo la ZCO

Kauli hiyo ameitoa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ubungo, tarehe 18 Juni 2025

"Ndugu zangu Wana Ubungo na Watanzania kwa ujumla, Nchi yetu imejaa na Majonzi na Masikitiko mengi na hata ukituona tunavyotembea wote tumejawa na majonzi na masikitiko"

"Haki yetu ya msingi inaporwa kila baada ya Uchaguzi toka mwaka 2020, lakini wanao-sababisha mambo haya yatokee ama uporwaji huu wa Uchaguzi ni CCM na dola la CCM"

"Sasa tunakwenda kwenye Uchaguzi mwezi wa 10, naomba Wanawake wa Tanzania, kila Mwanamke popote alipo ajue kwamba anajukumu la kupiga Kura lakini pia anajukumu la kulinda."

Kweli kachanganyikiwa aisee na amelewa navyoona. Pole yetu
 
Back
Top Bottom