Jando na Unyago: Ngoja niwafunde wadogo zangu muepukane na magonjwa ya kujitakia

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,659
698,441
Tuna magonjwa mengi binadamu ya kuambukiza, na yasiyo ya kuambukiza. Kati ya hayo kuna baadhi ni ya kujitakia hasa kutokana na uchafu. Yaani kutooga kabisa, kutooga vizuri ama kujisafisha vema.
Hii ni mada ya jinsia zote hivyo fuatana nami kwenye hili jando na huu unyago

Hakuna kitu kinavutia kama mtu anapokuwa msafi kuanzia kwenye nguo hadi mwilini. Usafi wa mwili na nguo huleta amani na utulivu moyoni, usafi huleta tabasamu, huleta mvuto pia. Lakini unapokuwa mchafu inakukera hata wewe mwenyewe.

Sasa kuna haya magonjwa ambayo huambatana na uchafu hebu tuyaone ni yapi hayo

1. Kuzama chumvini kwenye papuchi isiyooshwa vema

Body morphology ya mwanamke ni tofauti ya ya mwanaume hivyo ni rahisi kufuga bakteria kama usipotunzwa vema na kusafishwa itakiwavyo. Wakati unapozama chumvini unaweza kulamba ugiligili wenye vimelea na kujikuta unaondoka na gonjwa la kunuka mdomo lisilo na tiba ama fungus kuzunguka mdomo.

2. Kunuka mdomo

Ukiachana na ishu ya kuzama chumvini mdomo hauna tofauti sana na uchi wa kike. Usipopiga mswaki vizuri hasa ndani kwenye pembe za mdomo na ulimi lazima utanuka. Ulimi hubeba tabaka kubwa la mabaki ambapo usipousugua vema hasa asubuhi utajikuta mabaki yale kuoza na kuzalisha bakteria. Ni vema kupiga mswaki vizuri

3. Kunuka uchi

Hapa sababu ni nyingi. Kwa wanawake ni uvivu wa kujiingiza vidole na kujisafisha hadi ndani kabisa hasa nyakati za baada ya kufanya ngono, kutoka kuamka, baada ya kujisaidia, baada ya kumaliza hedhi na baada ya kutembea mwendo mrefu au kutoka jasho.

Kwa wanaume ni uvivu wa kunyoa sehemu za siri, kuwa na govi, kutobadili nguo za ndani, kutokuoga, kulala na janaba.

4. Kunuka miguu

Hakuna kitu kinakera kama kunuka miguu. Yani mtu akivua viatu hata nzi wanazirai. Ni kamongo tupu. Hili ni tatizo la kutooga vizuri na kusafisha vema miguu hasa katikati ya vidole, kuvaa soksi nyevu ama kuvaa soksi zaidi ya mara moja, kuvaa viatu visivyo na sehemu ya kupumulia, kutopaka mafuta hasa ya nazi na kuvaa viatu na miguu nyevu.

5. Mba, upele na ukurutu

Magonjwa yote haya ni magonjwa ya uchafu. Ukitaka kujilinda, epuka haya
1. Kutobadili shuka kwa muda mrefu
2. Chumba kuwa na makorokoro mengi halafu bila mpangilio
3. Kutosafisha chumba mpaka uvunguni na sehemu zisizoonekana. Huko ndio kwenye makazi ya papasi, viroboto chawa mende, funza na kunguni.
4. Chumba kinahitaji mpangilio, vitu vichache mwanga na hewa ya kutosha

6. Kunuka kikwapa

Hili nalo ni tatizo. Kama usipooga ama usipooga vizuri na kujisafisha vema sehemu za kwapa bila kusahau kunyoa lazima utanuka.

Magonjwa haya ni ya kujitakia na unaweza kuyaepuka kwa kuwa msafi na kuzingatia kanuni za afya.

Zingatia haya

Oga mara mbili ama zaidi kwa siku.
Kumbuka kujisafisha vema mara baada ya kujisaidia.
Usifuge nywele ndefu sehemu za siri na kwapani na ukizifuga usisahua kuzihudumia.
Usifuge kucha ndefu.
Usirudie nguo hasa za ndani.
Usivae nguo zenye unyevu hasa za ndani pamoja na sox.
Usitumie shuka, foronya ama blanket muda mrefu bila kufua.

Muhimu

Mara zote baada ya kuoga na kujisafisha vema, baada ya kujikausha maji yote mwilini kwa taulo safi usiache kujipaka MAFUTA YA NAZI hasa kwenye maungio. Msisahau pia sehemu zilizojificha kama makalioni.

===========
michango:

Hapo kwenye kujiingiza vidole kwa mwanamke sisashauri wengi wanaofanya hivyo hawaishwi kunuka na kupata magonjwa ya njia ya mkojo. Hata kisayansi haitakiwi. Mikono ina bacteria wengi na uke unajisafisha wenyewe safisha nje hakuna haja ya kuingiza madole huko.

Ubahili na kupenda vitu vya kuchangia pia husababisha magonjwa ya ngozi na mapele hasa kidevuni kichwani na sehemu za siri
Kwa kawaida unapaswa kutumia viwembe disposable... Yank usitumie zaidi ya mara mbili na uhakikishe usafi wake kama utatumia tena
Epuka viwembe vya bei poa hivi inabidi utumie nguvu nyingi hivyo kuathiri ngozi
Epuka kutumia saluni zisizozingatia usafi
 
Hapo kwenye kujiingiza vidole kwa mwanamke sisashauri wengi wanaofanya hivyo hawaishwi kunuka na kupata magonjwa ya njia ya mkojo. Hata kisayansi haitakiwi. Mikono ina bacteria wengi na uke unajisafisha wenyewe safisha nje hakuna haja ya kuingiza madole huko.
 
Hapo kwenye kujiingiza vidole kwa mwanamke sisahauri wengi wanaofanya hivyo hawaishwi kunuka na kupata magonjwa ya njia ya mkojo. Hata kisayansi haitakiwi. Mikono ina bacteria wengi na uke unajisafisha wenyewe safisha nje hakuna haja ya kuingiza madole huko.
Ndani kidogo kwenye mashavu Cajojo sio kule ndani kabisa na inabidi mikono iwe safi
Maji vuguvugu yenye chumvi kidogo na mdalasini hufaa zaidi
Kwa wanaume chicha husugua korodani mpaka zinameremeta maana wengi hawajui hiki kiwanda cha watoto kinabeba uchafu mwingi pia
 
Aisee inabidi nimtafute yule Dada wa ara za roho diva wa clouds akupe kipindi swali la kizushi utakubali kuwa mshana jr wakuone watu au utaitaji mask na wewe ili usijulikane
 
Back
Top Bottom