Habari wakuu,
Jana baada ya kazi zangu nilirudi nyumbani, sikuwa nimekula toka asubuhi kwa hiyo kwa sababu ilikuwa ni muda wa mchana nikaletewa chakula cha mchana, ugali, nyama ya kuchoma na mchicha, nikaanza kula, kwa kuwa nilikuwa na njaa sana, nikawa nakula kwa kasi, nikajikuta nimemeza nyama ambayo sijaitafuna vizuri, kwa hiyo haikukatika vizuri, hivyo nusu ikatangulia kwenye koo nyingine ikabaki kwenye mdomo, sasa kazi ikawa niimeze nyama ya mdomoni au niirudishe ya kwenye koo irudi mdomoni ili nitafune vizuri halafu nimeze upya, hapo ndiyo ilikuwa kazi, aisee kile kipande cha nyama niliyokuwa nimemeza kikaenda kuziba kwenye njia ya hewa, weeeee hapo mbona nilijamba, nikakimbilia bafuni wacha nihangaike, bahati nzuri baada ya kuingiza vidole kwenye koo nikaitapika nyama yote, hamu yote ya kula iliishia hapo, sitaki tena kusikia habari za nyama.
Kuna kitu nimejifunza tutaongea kwenye mjadala