Benny
JF-Expert Member
- Jun 6, 2014
- 3,275
- 5,415
Habari wakuu!
Tanzania tulikua na Kili Music Award ambazo zimekua na changamoto nyingi ila bado ni tunzo ambazo ziliwatia moyo sana wanamuziki wa hapa nyumbani.
Nimepata wazo sisi kama jumuiko dogo la watumiaji wa Jamii Forum tunaweza kuanzisha jambo dogo pia hapa kwa lengo la kutoa heshima kwa wanamuziki na kazi za muziki zilizofanya vizuri "kila mwaka" hatuwezi kuandaa tamasha kubwa la utoaji tunzo ila kwa bandiko kama hili litabaki hapa milele na milele kuonyesha nani aliwahi kufanya vizuri mwaka flani na itakua heshima kwake na kwa kila aliyeshiriki kuandaa hili.
Kwa kuanza nakaribisha mawazo kwa kila mdau kama litapokelewa vizuri.
Tunaweza kuandaa vipengele vichache sana na kupigia kura hapa na kutangaza washindi wetu kwa muda usiozidi miezi miwili tu yaani siku 60.
Pia ili kuepusha mkanganyiko tunaweza kuangazia kazi zilizotolewa miezi kumi au tisa tu iliyopita na baada utaratibu wa upigaji kura (kama tutafika huko) kupata na kutangaza zilizo bora tutasubiri tena kuangazia zitakazotoka kwa miezi kumi inayofuata.
Binafsi sina maslahi wala lengo lolote lilijificha juu ya jambo hili bali tu nia njema tu na upenzi wangu mdogo wa burudani na maendeleo ya muziki wa hapo nyumbani.
Kwa kua jambo hili ni kwa ajili ya watumiaji wa mtandao huu litahususha wale tu watakaopenda kushiriki na pia tutaheshimu sana ambao hawatapenda kushiriki (sio wote wapenzi wa muziki)na litakapokubalika basi na libaki kuwa letu halitahusiahwa na maslahi ya mtu yoyote binafsi humu au kikundi kidogo cha watu.