JamiiForums thanks

JamiiForums thanks

Ok Dar unaishi VIP wakati hauna kazi . Wewe ni Kabila gani samahan kwa kukuuliza ila ningependa kujua Kabila lako

dar yupo bro so alinichukulia chumba single akanilipia miezi 4 maswala ya msosi namaliza kwake huku nikisoma ramani...kuhusu kabila mimi ni mwenyeji wa kanda ya ziwa
 
dar yupo bro so alinichukulia chumba single akanilipia miezi 4 maswala ya msosi namaliza kwake huku nikisoma ramani...kuhusu kabila mimi ni mwenyeji wa kanda ya ziwa
Huyo kaka yako ingekuwa bora angekupa mtaji ila usijali mungu ni mwema utafanikiwa kanda ya ziwa musoma au . Endapo nikisikia kaz mahali nitakujulisha
 
Huyo kaka yako ingekuwa bora angekupa mtaji ila usijali mungu ni mwema utafanikiwa kanda ya ziwa musoma au . Endapo nikisikia kaz mahali nitakujulisha

bro hawezi nipa mtaji maana na yeye anaunga unga bado ....musoma ndio kabila la baba wa taifa ukisikia nishtue ndugu yangu tabu haina aibu
 
bro hawezi nipa mtaji maana na yeye anaunga unga bado ....musoma ndio kabila la baba wa taifa ukisikia nishtue ndugu yangu tabu haina aibu
Nilijua utakuwa wa musoma manake baadhi ya wanaume wa musoma wanatabia ya kuhama nyumba zao . Wakipata tatizo wenyewe wanakimbia badala ya kutatua tatizo . Nitakustua mkuu
 
Nilijua utakuwa wa musoma manake baadhi ya wanaume wa musoma wanatabia ya kuhama nyumba zao . Wakipata tatizo wenyewe wanakimbia badala ya kutatua tatizo . Nitakustua mkuu

haya bwana
 
Nimehis tu huyo atakua mtu w kanda ileee!! Pole we mwanaume huna haja ya kua na wsws na maamuz yako. Walk the talk
 
Hi Brothesr and sistesr,

Kwanza kabisa napenda kuwashukuru sana members wote humu maana mmenisaidia mengi sana kama miaka 2 iliyopita niliomba ushauri humu mkanisaidia ndoa yangu ilikua inakwenda kwa maji.so nimerudi tena

>>mimi ni mwanaume na nina mke na watoto3 kwangu ni Arusha nimeshajenga nakaa kwangu, mke wangu ni mfanyakazi wa serikalini na mimi ninafanya kazi sector binafsi nimeanza kuishi na mke wangu toka 2004 >2016=12 tuliishi kwa furaha amani na upendo. mwaka 2014 nilisimamishwa kazi kwamatatizo flani flani ya kikazi so mwaka 2014

>>2015 woote nilikua nyumbani namaanisha sikubahatisha kazi kabisa nilizunguka kila kona ya arusha lakini wapi hadi nikahisi nimetupiwa mkosi,2015

>mke wangu akaanza kubadilika akawa mtu wa hasira kitu kidogo tu ataongea usiku kucha bas kuna vitu flani flani haki za mme nikawa sipewi tena kisingizio eti kachoka mfano kama kufua nguo zangu chakula cha usiku na mengine kama hayo ,tunaweza kaa siku tatu hatuongei kanuna lakini the same time akipigiwa cm na marafiki zake anaongea kwa vicheko akikata tu cm anavaa sura ya kazi.au nikiwa sipo anakua na furaha kweli lakini nikiingia tu nyumbani ananuna anakwenda na kulala kabisa ,so hali hiyo imenifanya mimi niwe na mawazo mno imepelekea hata kudhoofu mwili nimekonda mno ,mwanzoni mwa mwaka huu 2016 alinifanyia kituko ndicho kilichonipelekea mimi kuja kuomba ushauri humu tar 20/1/2016 alichelewa kuja home isivyokawaida yake na kila nilipompigia cm yangu alikua hapokei ..nilifunga milango tukaingia kulala na watoto yeye alikuja saa 11 usiku so sikumfungulia mlango kwa hasira alilala nnje alfajiri kumfungulia akaingia kwa matusi naomba ninukuu

>>>hivi unathubutu kunifungia nnje mimi ninavyokubeba hapa mjini niende kutafuta nije wewe ule ..unajua hata ni wapi natoa hizo pesa unazo kula?unafikiri hata leo nisipoleta hata kumi utakaa mjini wewe? ngoja sasa kesho naondoka nakuachia hili linyumba na watoto wako mtajua mtakulanini,,,so kwakweli niliumia mno na kwahasira nilimpiga sana kwasiku hiyo alishindwa hata kwenda kazini...ilipofika usiku akenda kulala kwa chumba cha watoto lakini alisahau cm yake chumbani kwangu bass nikaanza kupitia msg nikaona alikua anachat na dada yake mkubwa ..dada yake anampa maelekezo kua amchukue mtoto mmoja ahame hapo kwangu kuna chumba sehem amempatia ,,so nikapata akili haraka haraka kua huyu wife akinitelekezea hawa watoto na mimi sina kazi itakua matatizo zaidi so nikapata wazo bora mimi niondoke hapo nyumbani niende popote pale kuokoa hili jaazi, so alfajiri sana nilidamka nikakamata basi nikaja dar sasa nina mwezi wa 2 huku dar ,,,wiki iliyopita ameanza kunipigia cm ananiomba nirudi nyumbani maana hawezi kukaa mwenyewe na watoto anaogopa pia anadai kua watoto wanamsumbua kumuuliza baba yuko wapi???

NAOMBENI USHAURI NIFANYEJE?? NIRUDI ARUSHA AU NIKOMAE KWANZA DAR NITAFUTE MAISHA?
Mkuuu ushauri mzuni ni wewe kutafta maisha.ukirudi ataendelea kukudharau zaidi.kumbuka hapo hujaitekeleza ila unatafta maisha kwa ajili ya familia yako
 
Aisee pole umenifunza mengi... Kwamba ktk maisha wakati wewe unacheka kuna wengine wanalia...

Kwakweli sijawahi kabiliana na kadhia yoyote kiasi cha kunifanya nione dunia tambarare.... Thanks again umenirudisha kwenye fikra MPYA....

Pole sana kwa uliyopitia but usikate tamaa...

Ushauri wangu komaa kwanza upate hiyo kazi sio mbaya pia ukituambia elimu na fani yako tunaweza kukusaidia coz wengine tuna muda mrefu hapa mjini so vichochoro tunavijua vingi....

Kila la kheri na Mungu akupe Faraja......
I lov this comment
 
Pole bro na kila la kheri..pia mshirikishe Mungu kwenye mihangaiko yako ya siku na ukienda kulala shukuru kwa lolote.
 
Majibu rahisi.kwenye maswali magumu.
Unadhani hajui sitution aliyonayo mme wake?

Wameishi miaka 12 kwa furaha hilo hulioni??

Man usirudi kwani tatizo liko pale pale kama huna mshiko huyo wife ataendelea kukupanda kichwani tu, so long watoto wako mikononi mwa mama na anauwezo wa kuwatunza tafuta kwanza.
 
Majibu rahisi.kwenye maswali magumu.
Unadhani hajui sitution aliyonayo mme wake?

Wameishi miaka 12 kwa furaha hilo hulioni??

Man usirudi kwani tatizo liko pale pale kama huna mshiko huyo wife ataendelea kukupanda kichwani tu, so long watoto wako mikononi mwa mama na anauwezo wa kuwatunza tafuta kwanza.

thanks men nimeipenda hii maana ndio haswa lilikua wazo langu
 
thanks men nimeipenda hii maana ndio haswa lilikua wazo langu
Kumbe Una mastress yakoee ndo mana Kule PM ulikuwa unaongea utumbo mwanzo mwisho, subir nimtafute huyo bidada nkampeleke kwa dokta akapate sindano yetu ilee
 
Kumbe Una mastress yakoee ndo mana Kule PM ulikuwa unaongea utumbo mwanzo mwisho, subir nimtafute huyo bidada nkampeleke kwa dokta akapate sindano yetu ilee


ha ha nsamehe kama nilikukwaza huyo bidada wewe mpeleke tu akadungwe sindano ,,,sindano zipo kwaajili
 
hii story badoo sijaridhika sasa hapa town unafanya nn mkuu upo kwa nani?

umepata kazi kama umepata kwanni bado unaikimbia familia mke alikosea na wewe umekosea watoto wataumia

na unaishukuru nini forum hii?
 
hii story badoo sijaridhika sasa hapa town unafanya nn mkuu upo kwa nani?

umepata kazi kama umepata kwanni bado unaikimbia familia mke alikosea na wewe umekosea watoto wataumia

na unaishukuru nini forum hii?

mzee naishukuru forum kwa ushauri uliotukuka sio mara ya kwanza kuomba hapa ushauri na nafarjka kabisa...kuhusu nakaa wapi nmeshaelezea hapo nyuma nimepangishwa chumba na bro ambae yeye anakaa huku mda sasa...sijapata kaz bado maana tangu nije huku sasa n siku 40 zimepita......
 
Hahhaaa poapoa man!

Pale mwanamke unapojua kazi yake kwa mda mrefu, halafu siku anakwambia hivi wewe una akili? We unakula tu unajua hizi lesa nazipata wapi na nazipataje??

Inauma sana lkn no way!
 
Hi Brothesr and sistesr,

Kwanza kabisa napenda kuwashukuru sana members wote humu maana mmenisaidia mengi sana kama miaka 2 iliyopita niliomba ushauri humu mkanisaidia ndoa yangu ilikua inakwenda kwa maji so nimerudi tena.

>>Mimi ni mwanaume na nina mke na watoto3 kwangu ni Arusha nimeshajenga nakaa kwangu, mke wangu ni mfanyakazi wa serikalini na mimi ninafanya kazi sector binafsi nimeanza kuishi na mke wangu toka 2004 >2016=12 tuliishi kwa furaha amani na upendo. Mwaka 2014 nilisimamishwa kazi kwamatatizo flani flani ya kikazi so mwaka 2014

>>2015 wote nilikua nyumbani namaanisha sikubahatisha kazi kabisa nilizunguka kila kona ya Arusha lakini wapi hadi nikahisi nimetupiwa mkosi,2015.

>Mke wangu akaanza kubadilika akawa mtu wa hasira kitu kidogo tu ataongea usiku kucha basi kuna vitu flani flani haki za mme nikawa sipewi tena kisingizio eti kachoka mfano kama kufua nguo zangu chakula cha usiku na mengine kama hayo,tunaweza kaa siku tatu hatuongei kanuna lakini the same time akipigiwa simu na marafiki zake anaongea kwa vicheko akikata tu simu anavaa sura ya kazi au nikiwa sipo anakuwa na furaha kweli lakini nikiingia tu nyumbani ananuna anakwenda na kulala kabisa.

So hali hiyo imenifanya mimi niwe na mawazo mno imepelekea hata kudhoofu mwili nimekonda mno mwanzoni mwa mwaka huu 2016 alinifanyia kituko ndicho kilichonipelekea mimi kuja kuomba ushauri humu tar 20/1/2016 alichelewa kuja home isivyokawaida yake na kila nilipompigia simu yangu alikua hapokei, nilifunga milango tukaingia kulala na watoto yeye alikuja saa 11 usiku so sikumfungulia mlango kwa hasira alilala nnje alfajiri kumfungulia akaingia kwa matusi naomba ninukuu.

>>>Hivi unathubutu kunifungia nje mimi ninavyokubeba hapa mjini niende kutafuta nije wewe ule unajua hata ni wapi natoa hizo pesa unazo kula?Unafikiri hata leo nisipoleta hata kumi utakaa mjini wewe? Ngoja sasa kesho naondoka nakuachia hili linyumba na watoto wako mtajua mtakulanini,so kwakweli niliumia mno na kwahasira nilimpiga sana kwa siku hiyo alishindwa hata kwenda kazini ilipofika usiku akenda kulala kwa chumba cha watoto lakini alisahau simu yake chumbani kwangu basi nikaanza kupitia msg nikaona alikua anachat na dada yake mkubwa, dada yake anampa maelekezo kua amchukue mtoto mmoja ahame hapo kwangu kuna chumba sehemu amempatia.

So nikapata akili haraka haraka kua huyu wife akinitelekezea hawa watoto na mimi sina kazi itakua matatizo zaidi so nikapata wazo bora mimi niondoke hapo nyumbani niende popote pale kuokoa hili jaazi, so alfajiri sana nilidamka nikakamata basi nikaja Dar sasa nina mwezi wa 2 huku Dar wiki iliyopita ameanza kunipigia simu ananiomba nirudi nyumbani maana hawezi kukaa mwenyewe na watoto anaogopa pia anadai kua watoto wanamsumbua kumuuliza baba yuko wapi?

NAOMBENI USHAURI NIFANYEJE? NIRUDI ARUSHA AU NIKOMAE KWANZA DAR NITAFUTE MAISHA?

Pole sana, ndo maisha yalivyo. Maamuzi uliyoyafanya sio mabaya sana, sometimes it happens even to others kwa sababu BINADAMU WANAKERA SANA. Hivyo kutafuta suluhu ya muda kuondoka home sio mbaya kwa sababu 1. uliepusha vita 2. Ulitafuta furaha ya muda 3. Uliotoa muda kwa wife ili aweze kuona umuhimu wako. 4. Umepata jambo la kutuambia ili nasi tujifunze toka kwenye haya matukio ya mahusiano.
Pamoja na yote hayo fahamu kuwa wewe ndio kichwa cha familia. Na ili uwe kichwa kizuri lazima ujue kuwa unapaswa kutimiza majukumu yako yakibaba kwa mkeo na wanao. So, unatakiwa uwe na shughuri ambayo itakuingizia kipato ya kukidhi mahitaji ya familia yako. Kwa maaana hiyo ni lazima ujitume ili gurudumu lisonge. Katika maisha kuna shughuri za aina nyingi kama vile Biashara, Ajira na Uwekezaji. Nilazima ufanye ma moja kati ya hizo au zote ili goma lisonge.
Kufukuzwa, kuondolewa, kusimamishwa kazi si mwisho wa maisha, yakikukuta hayo unachotakiwa kufany ni kubadilisha Mtazamo wako na kutafuta shughuri ambayo inaendena na wakati unaokabiliana nao. Si vyema kujifungia nyumbani. Toka, changanyika, jifunze usichokijua kwenye shughuri zilizopo mtani ili maisha yako yasonge.
Ukiondoa aibu, kila kitu kitakaa sawa kwani kuna shughuri kibao mtaani (Zimeambatanishw) ambazo ukizifanya zitakuingizia kipato cha kuendesha maisha ya familia yako. Usipofanya hivyo utakuwa unataka kubadili majukumu ya familia ambapo utamtaka mama achukue majukumu ya baba, hapo ndipo matatizo yanapoanziaga. Akianza yeye kutafuta kwa ajili ya kuziba pengo lako, inamaanisha kuwa wewe si muhimu tena kwao. Kinachofuata ndio kile kilichokukuta.

Badilika, acha kujifungia ndani, tafuta shuguri ya kufanya ili utimize majukumu yako kama baba.
 

Attachments

Mkuu miongoni mwa watu wenye akili na wewe umo, atakaesema umefanya makosa kuondoka na yeye ni akili zake.

Mwanaume unatakiwa kuwa mvumilivu lakini pia kuna uvumilivu wa kijinga.

Kwa maelezo yako hukuondoka nyumbani kwa kukwepa majukumu la ila kwa kuinusulu ndoa na familia yako pia kupuka manyanyaso ya akili na roho.

Kwa nionavyo mimi ulifanya jambo la busara kwani usingeondoka ambalo lilikuwa linajili ni kutengana na kugawana mali yenu hali ambayo ingewaweka watoto katika mazingira magumu sana.

Ushauri wangu ni kwamba endelea kuwasiliana na mkeo wasalimie watoto kila siku hata ikibidi wadanganye unafanya kazi na ukipata chochote wakumbuke uwatumie zawadi na mahitajio mengine.

Ila wakati huo ukiwa unatafuta kazi popote pale, mungu hamtupi mja wake utapata iwe arusha au hata huko Dar, baada ya kupata kazi rudi nyumbani.
 
mzee naishukuru forum kwa ushauri uliotukuka sio mara ya kwanza kuomba hapa ushauri na nafarjka kabisa...kuhusu nakaa wapi nmeshaelezea hapo nyuma nimepangishwa chumba na bro ambae yeye anakaa huku mda sasa...sijapata kaz bado maana tangu nije huku sasa n siku 40 zimepita......
komaa upate kazi la si hivyo mambo yatazidi kuwa mabaya yaani mie ni ke lakini huwa hata zege naweza kubeba naogopa sana ujobless kwakiwa sijaumbwa kutegemea mtu yeyote naogopa kuomba kwa mwanaume........naogopa manyanyaso uwii
 
Back
Top Bottom