JamiiForums thanks

JamiiForums thanks

Ulifanya sawa kuondoka maana kwangu mimi kuliko watoto waone baba na mama wanalala vyumba tofauti ni bora usiwepo kabisa kwenye simu utajua cha kuwadanganya. Na kuachiwa mtoto wakati huna jinsi ya kumlisha ni mtihani mkubwa; sielewi huyo mama alikuwa anawaza nini kukuachia mtoto wakati anajua huna kazi. Hapo mawazo yake ni kuwa hutafuti kazi makusudi kwa sababu majukumu yamemuelemea. Pia hatarajii kutoka kazini aje halafu arudi nyumbani kufanya kazi za nyumbani wakati wewe ulibaki nyumbani. Huko kurudi saa 11 si kuwa alikuwa kwa mchepuko. Si ajabu dadake alimshauri akufanyie hivyo maana kwao wewe huna maana kwa sababu huna kitu.

Halafu waswahili wanasema hakuna msiba usio na mwenzie. Umepoteza kazi, ukaja msiba wa kupoteza heshima, ukaja msiba wa kutenganishwa na familia. Si ajabu ukaingia kwenye msiba mwingine mkubwa maana ushasema uko tayari hata kufanya kazi isiyo ya halali ilimradi upate hela. Unaweza kufikiri suluhisho ni kupata kazi lakini navyojua mimi kupata kazi mpya si rahisi, hata ukipewa haitadumu kama muda wa mtihani haujaisha. Na kama suluhisho la tatizo lako lingekuwa ni kazi basi usingepoteza kazi yako hapo mwanzoni. Kuna mambo ya msingi mnayotakiwa kuyaweka sawa wewe na mkeo. Kuna mtu kati yenu anatakiwa kunyooka (kushushwa kiburi) au ninyi wote ila kila mmoja kwa njia yake.
 
Kumbe Una mastress yakoee ndo mana Kule PM ulikuwa unaongea utumbo mwanzo mwisho, subir nimtafute huyo bidada nkampeleke kwa dokta akapate sindano yetu ilee
acha kisirani wewe ardhi ya vichaka
 
KOMAA UPATE KAZI. (UWE NA KIPATO CHAKO MWENYEWE ) itakupa heshima nyumbani. Ukirudi unarudi kula kule na manyanyaso yataongezeka na hakika utateseka zaidi. Watoto wakihitaji kitu wataambiwa mwambieni baba yenu alafu huna uwezo na utanyanyasika utatamani kujinyonga. Kama una damu ya kule milimani
 
japo nimechelewa kusoma huu uzi ila umeniuma sana.
 
Back
Top Bottom