JamiiForums imenifanya tuamue maamuzi haya mimi na wife

Mboju

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2021
Posts
200
Reaction score
339
Wakuu habari za asubuhi, jana nimefungua uzi kuelezea sisi tusio kuwa nacho maisha tunayopitia mpaka kukosa chakula na kuishia kula mlo 1 tu kwa siku nawenyewe kwa mbinde

Wapo walioguswa na kutoa ushauri mzuri nini cha kufanya pia wapo walio kejeli ( hawakosekanagi hawa ) pia wapo walioponda badala ya kutoa maoni ya kujenga

Wakuu narudi kwenu ni hivi tumeamua wife kuanzisha biashara ya dagaa wa bukoba japo tuanze na ndoo moja au mbili kwasababu ana koneksheni kule, kwann dagaa kwanza ni mboga inayotumiwa sana mtaani tulipo pia wife akanidokeza kuwa anaweza kuwa anatembeza hasa kwenye migahawa ya mama ntilie ile midogo midogo na akapata wateja nami nikaona ni wazo zuri

Shida inakuja ni ile ile mtaji, kianzio katika kupiga hesabu mtaji na usafiri inakuja kama elfu 60 hivi na faida unaweza kutoa 40k japo sina uhakika mpaka tufanye

Mimi kwa upande wangu nitaendelea kuhangaika hapa na pale ila plan yangu ni kufungua library japo ya kawaida tu ndogo kwasababu nina esperience nayo.

SIMULIZI YANGU MPAKA LEO NIKO HAPA

Nitawapa simulizi kidogo ya maisha yangu wenda kuna kitu mtajifunza.
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 31-35 kadiria humo, nimeoa nina watoto 4 wawili wa kike wawili wa kiume mtoto mkubwa ana miaka 8

Katika kukua kwangu mpaka najitambua (+18 ) nimejikuta katika mikono ya baba yangu mkubwa (R.IP) alishatangulia mbele ya haki na alikufa akiwa anajua simjui mama yangu hii nitailezea mbele huko kwani mma nimekuja kumuona baadaya miaka kama 20 japo upendo ni mdogo mno kulingana na yaliyotokea na sababu alizonipa niliona hazina mashiko pia hajawahi hata kwenda nyumbani kushukuru kwa kumlelea mwanaye ( nitalieleza huko mbele) baba yangu mzazi pia alishatangulia mbele za haki ( R.I P ) alinipenda sana mshua wangu

Mwaka 2002 nilibahatika kupata nafasi katika shule moja ya private hii ni baada ya jitihada za baba mkubwa na sista angu ambaye alikuwa kama mchepuko wa mwenye shule nahisi hii ndo ilinisaidia kupata nafasi pale pia nakumbuka hii kitu ilileta ugomvi mkubwa kati ya ma mkubwa na na mkubwa mama mkubwa akimlaumu na kumtolea maneno ya shombo ba mkubwa kuwa kwann kanichukua mimi wakati na yeye ana watoto.

Nilijitahidi kusoma kwa bidii sana huku nikijua maisha yangu mm ndo nitakaye yabeba. Nakumbuka ilifikia kipindi baba mkubwa yeye ndo alikuwa ananifulia unifomu zangu wakati ana watoto wakubwa tu na kipindi hicho walikuwa shule pia ingawa shule za serikali hii ni kutokana na ile ishu ya ma mkubwa kusema kuwa kwann mimi ndo nichukuliwe shule ya private ( wakuu hapa kuna kitu niwambie baba mkubwa alikuwa ni mgonjwa wa kifua kikuu yaani kukohoa mpaka unamuonea huruma na ndo kilicho muua maana dawa zimekuja hivi majuzi tu zimekuta tayari yeye kifua kisha chakazwa lakini alikuwa anainama ananifulia hadi nguo kwasababu wanae walikuwa wanagoma ikumbukwe bado nilikuwa mdogo nisingeweza kufua mwenyewe hasa uniform zikatakata )

Basi bhana nimesoma nikajitahidi darasani kufanya vizuri kiukweli darasani nilikuwa vizuri sana, hatimae mwaka 2008 nikamaliza darasa la 7, tukaanza maisha ya mtaani kwa miezi 3 huku tukisubiri matokeo ya mtihani wa darasa la 7 mungu si Yuda matokeo yakarudi nikiwa nikiwa nimefaulu kimbembe kikaanza naendaje shule kiukweli pale nyumbani kulikuwa hamna mtoto yeyote aliyewahi kwenda elimu ya sekondari hii ni kwasababu ya kipato baba mkubwa akachekecha kichwa ikabidi arudi kwa mfadhili wangu yule aliye nisomesha primary nitampa jina la Y( R.I.P ) naye alisha tangulia mbele za haki kuna watu nawamisi ila ndo maisha.

Mzee hakuwa na hiyana akasema atanipeleka kwenye shule za kata nakumbuka kipindi hicho hizi shule zilikuwa kama na miaka 3 au 4 kama sikosei zimeanza. Rasmi 2009 nikaanza kidato cha kwanza kama kawaida nikajitahidi kusoma sana huku nikisaidiwa na yale masomo ya shule za private si unajua kule mnakula msuli vyakutosha.

Basi bhana baada kama ya miezi 6 mzee akaona maendeleo yangu ni mazuri akasema inabidi anihamishe anipeleke shule za private pia ikabidi ufanyike utaratibu bhana we sijui nini kilitokea hadi wa leo sijuagi, ni hivi siku ya kwenda shule nakumbuka niliamka saa 11 asubuhi make shule ilipokuwa ilikuwa lazima nisafiri yaani kutoka wilaya x kwenda wilaya y mzee akamwambia mtoto wake ndo anichukue akaniandikishe shule na amalize taratibu zote bhana we ile tuko kwenye gari tumetoka kama lisaa limoja simu ikapigwa inabidi turudi hii sikuwahi kujua sababu ni nini, basi bhana mi nilikuwa nafata maelekezo, ikabidi turudi kitu kipya ni kuwa sikurudishwa nyumbani hapana nilipelekwa kwa mzee nikaanza kuishi kwa kijana wake hukh nikisubiri maelekezo mengine, ebwana wee mwezi wa 1 ukakata 2, huo wa 3 nao huo hapo sasa nimekuwa kama mtoto wa huyo kijana yaani nafanya kazi zote, nakumbuka nilikuwa naamka napika uji wa mke wake, chai ya watoto, nadeki nyumba, napika chakula cha mchana baada ya hapo kazi zilizobaki yaani za jioni kuna binti mmoja naye alikuwa anasaidiwa na huyo mzee na alikuwa anaishi kwa kijana wake kama mimi sasa yeye alikuwa anaenda shule asubuhi jioni ndo anarudi kwahyo kazi zote za jioni alikuwa anafanya yeye mimi kazi yangu ya jioni ilikuwa ni kuhakikisha maji hayakosekani pale japo kwa wakati ule nilichukulia kama mateso lakini vitu vimenisaidia ktk maisha yangu.

Sikumbuki vizuri ilikuwa mwezi wa ngapi ila nahisi mwezi 8 mzee alikuja pale kwa kijana wake na kumwambia kuwa kesho nijiandae naenda shule nilifurahia mno nilijiandaa hatimae nikaenda shule mazingira hayakuwa mabaya sana au mazuri sana nikakabidhiwa pale huyo kijana akaondoka sasa nimekaa pale make ilikuwa ni boarding school nakuja kugundua kuwa ni zile shule za Wale watu wanaotaka balance masomo yaani ulifeli somo fulani unataka ulirudie kwahiyo mimi pale nilipokelewa kama mwanafunzi wa Qt baada ya kuelewa sikuwa na kinyongo mimi nikasema nitakomaa ila nilikuja kugundua kwann mzee alinipeleka pale sababu kuu ni mzee aliona mbele maana kuna kipindi ilikuwa inafika sina karo narudi home ( kwa yule kijana nakaa tena kama miezi 3 ndo narudi shule hii ziwezi mlaumu mzee make mambo yake yalienda kombo kipindi hicho mpaka ikapelekea shule yake kuuzwa kwa roman catolik na hii nahisi ndio iliyomfanya mzee anafariki maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana)

Basi bhana pamoja na purukushani zote nilifanya mtihani wa QT nikawa nimefaulu vizuri hivo mwaka 2012 nikafanya mtihani wa form 4 ikumbukwe mazingira yangu ya masomo hayakuwa mazuri sana kutokana na ukosefu wa karo hapa ilinidi niruke yaani form 3 sikuisoma niliunganisha masomo ya form 2 na 3 kwa pamoja mwaka 2012 mwaka wa historia sitamsahau yule mma alikuwa waziri wa elimu kipindi hicho aisee alichotufanyia hatutamsahau kwanza picha linakuja nimesoma kwa kuunga unga pili matokeo yanatoka mara2 japo katika yote cheti changu cha form 4 ninacho mzee wangu ( aliyenisomesha ) kipindi hicho alikuwa tayari kafilisika vibaya mno aisee asikwambie mtu kama ulishawahi kushika pesa ikachomoka aisee hii isikie kwa jirani yako mma mwantumu na sio kwako hivo nilishindwa kuendelea na masomo ingawa nilikuwa nimefaulu japo sio kivile ( hapa kuna kitu sijawambia nikiwa shule pale kulikuwa kuna somo la compyuter hivo poket money yangu nilikuwa nikilipa kwenye somo la ziada la kompyuta na nilifaulu vizuri mno na cheti cha kompyuta ninacho pia)

Rasmi baada ya kumaliza form 4 nikaanza harakati za mtaani kutafuta na kujitafuta aisee hapa ndo kuna mengi mnoo ndo nilikuja kuanza kumtafuta mama, kupelekwa polisi na mengine mengi mnoo narudi mda si mrefu kuendeleza simulizi fupi ya life langu.....

Inaendelea
Mtanisamehe mmi sio muandishi mzuri wa simulizi hivo someni hivo hivo lengo ni kujifunza

Tulipo ishia, nimemaliza form 4 rasmi naanza maisha ya mtaani

Nilikuwa mtafutaji wazee kwanza niliingia mtaani kusaka kazi, nilibahatika kupata kazi ya kumfundisha mtoto wa jamaa mmoja kompyuta,nakumbuka nilikaa pale kwa muda wa miezi kama 4 make alikuwa na duka la nguo na vifaa vya umeme na simu baada ya kijana wake kuelewa mafundisho ilibidi mkataba wangu uishie pale huyu baba pia ni mtoto wa yule mzee aliyenisomesha imagine familia hii ilivyonitendea natamani na mimi siku moja niwalipe wema walio nitendea hata kama ni kwa vitukuu vyao naamini mungu ni mwema ipo siku.

Baada ya mkataba kuisha ikabidi nirudi home nikaanza kumshinikiza baba mkubwa anioneshe au kuniambia mama yangu mzazi alipo na anipe kisa cha mama yangu kunitelekeza mzee alikataa kata kuniambia kisa na alisema anayejua mama yangu alipo ni mwanaye mkubwa ndo aliwahi kuishi naye kwa baba yangu mzazi. Huyo dada kipindi hicho alikuwa mwanza kwenye utafutaji nikasema siku akija nitamuomba anipe stori kuhusu mama yangu

Kama nilivyosema awali mungu sio Yuda dada alikuja pale nyumbani kusalimia ilikuwa ni kipindi cha sikukukuu kijana nikajitahidi kumfurahisha dada yangu ili anipeleke anapohisi mama atakuwepo nakumbuka kipindi hicho tayari nishapata compyuter naingiza muvi na muziki na hii ilikuwa ya jamaa yangu ( hii biashara ilikuja kuharibika baadae baada ya compyuter kuungua tukakosa vifaa make ilibidi vifatwe mjini )

Basi baada ya dada kumaliza siku zake pale akaaga nakuondoka ila tukaondoka wote kwenda kumtafuta mama bhana, sister angu huyu ni genius kwenye kumbukumbu aisee alikumbuka maeneo tukayapitia yote huku tunauliza jina kizuri mama hakubadili jina wazee hapo nina hamu sana ya kumuona mama yangu yaani upendo kama wote ila kichwani pia nina hamu ya kumuuliza maswali yangu hasa kwanini aliamua kunitelekeza kwa miaka zaidi ya 20 na alipo kuwa sio mbali kwamba utavuka mikoa 5 bado hata kama ingekuwa 5 alishindwa nini kufatilia kama nipo au nilikufa.

Basi bhana baadae tukafanikiwa kuelekezwa nyumba alimo kuwa anaishi ile tumeenda sista akamuona na kweli wakajuana ni nimefanana na maza kinoma hawezi nikataa basi bhana wakuu ule upendo niliokuwa nao sijui ulienda wapi nilijjkuta nakasirika mpaka wote wakaniuliza kulikoni nikavunga, nilisalimiana na mama kikawaida yaani utafikiri ni mtu nimetoka kuonana naye jana au juzi tu, baadae sista aliaga na kuondoka mi nikabaki pale nikatengewa maji ya kuoga nikaoga chakula ya mchna ilikuwa tayari baada ya hapo tukaufinya msosi, nikasema leo ngoja nivunge ila kesho nitauliza maswali yangu.

Kesho yake nilipata wasaaa wakuongea na mama swali langu la kwanza nilimuuliza kwanini hakuwahi kunitafuta wakuu huwezi amini mama aliniambia kuwa sababu ni baba yangu nikamuuliza mbona mpaka baba yangu anakufa hakuwahi kuniambia kitu chochote kuhusu wewe hata familia nilikokulia hawajawahi kuniambia chochote kuhusu ww walikuwa wanasema utaniambia ww na ww unasema sababu ni baba yangu.

Wakuu nilijikuta naanza kumchukia maza pole pole baada ya kumbana sana akanipa stori kamili ni hivi baba alipooana na mama kwao na mama hawakupenda hili maana mama yangu ni muislamu baba yangu ni mkristo so wakasema mtoto wao hawezi olewa na kafiri kama wasemavyo wao nikaichanganua hiyo hoja nikaona ni sawa ( hii nilikuja kulipiza baadae tutaona mbele ) nikamuuliza je walimkataza hadi kuja kuniona au kunitembelea au kunijulia hali hapa ndo ikawa kimbembe alikaa kimya akaanza kufoka foka nikasena barida isiwe tabu mimi nilichotaka ni kukujua kama upo hai mengine wacha yapite, nilikaa pale kwa maza kama miezi 2 hivi, nikarudi home ikabidi nijiingize kwenye masuala haya ya usajili wa line ikumbukwe upendo wangu kwa mama haukuwa mwingi kivile yaani hapa niwe mkweli hadi leo mama yangu amekuwa ni kama mtu baki sijui nielezeeje yaani upendo mwingi upo kwa upande wa baba yangu huko ujombani kuna watu wengine nahisi hawanijui afu ni watu wa kujitenga tenga yaani kujiona sana mimi sifagilii hizo mambo

Basi bhana nimenza kusajili line, nikapata mtaji pale nyumbani ikabidi nifungue kibanda kama kiduka flani hivi baba mkubwa hakuwahi kuniacha hasa kunipa ushauri na mambo mengine kiukweli nilikuwa nampenda sana (R.I.P) kweli bhana faida nilikuwa napata pia kazi yangu ya usajili line sikuiacha baada ya muda kibanda kilijaa kabisa nikaanza kuwa natoa chochote home ili waendeleze harakati

Kwenye swala la kusajili line, nilikuwa nina mwavuli na meza kuna jamaa alikuwa na duka na alikuwa anashona nguo nilimuomba niwe nakaa mbele ya duka lake na kimwavuli changu huyu jamaa mpaka sasa bado ni rafiki yangu ingawa ni mtu mzima jamaa baada ya kuona napata wateja wengi akaleta wazo la kufungua mpesa pale yaani mimi niwe nafanya niksema poa, kweli akatafuta line maana alikuwa na document zote hatimae nikaanza kazi piga kazi piga kazi matunda yakaanza kuonekana make kuna kipindi tulikuwa tunalipwa hadi laki 7 jamaa tulikuwa tumeelewana kuwa atakuwa ananilipa kutokana kam commision ilivyoingia

Aisee baada ya miezi kadhaa jamaa alipatwa na matatizo ikabidi asepe kwa muda so kazi ikaishia pale pale ila bado nyota yangu ilikuwa inang'aa akaja jamaa mwingine naye akanipa line za mpesa na mtaji tukaanza kupiga kazi kipindi hicho line za mpesa zilikuwa 2, ya kupigia kazi na ya kupokea malipo japo sidhani kama mpaka sasa ni hivo, aisee kumbe jamaa alikuja na target zake siku moja nipo kwenye job jamaa akaja anadai anataka line zake zote kuna kitu anaenda kufanya wazee hapa ndipo mzozo ulipoanzia nikampa line ile ya kupigia kazi maana ya kupokea commsion alikuwa anakaa nayo yeye si akanigeuka akasema yeye alinipa line zote mbili nikamuuliza kama ulinipa line zote mbili comision ulikuwa unapokeaje au unaonaje jamaa akaanza kuwaka na kuleta mambo mengi mara hao mgambo nikajikuta kituo cha polisi khaa nikaona lishakuwa tatizo hili kama unavyojua mikwara ya polisi japo nilimkuta mdada ndo alikuwa kama incharge namkumbuka hadi leo alikuwaga mkarimu mno mungu ambariki popote alipo

Mwisho mi nikasema sina hiyo line we ndo unayo ila amua ww unatakaje jamaa akasema nitoe hela tukaiswap hiyo till nikamuuliza gharama aisee alinitajia gharama sijui alikuwa ananikomoa sijui ni ushamba wangu wa kutokujua mambo ni kweli till ambazo zilikuwa hazina majina yako ilikuwa ni gharama kuzi renew ila sio kwa ile gharama
Ilibidi niwe mpole nikamwambia jamaa mi nakuachia kibanda chote na vilivyomo nakumbuka niliuwa nimeweka sola ya wats 20 na betri yake pia jamaa akakubali.

Kila kitu kilivoenda nilimuambia baba mkubwa yangu alinishauri kutoka kata tamaa akanishauri kwajinsi anavyoyajua mazingira ya home inabidi niondoke make nikikaa nitajikuta napagawa na nikweli aliniona maana nilikuwa na mawazo mengi mno ikabidi nimuambie naenda kwa mama ingawa sikuwa na ukaribu naye sana, then nitajua cha kufanya hii ndo ilikuwa mara yangu ya mwisho kumuona baba yangu mkubwa kipenzi sikuju...

Inaendelea...

Hapa tutaona jinsi nilivyokutana na mke wangu mwaka 2015, Baba yangu mkubwa alivyo fariki mpaka nikakosa nauli ya kwenda home kuzika nikaja kusaidiwa na mtu kutoka kwenye mtandao wa x zamanni twitter, mpaka leo sijawahi kumjua maana hakutaka hivo na njia aliyotumia kutuma pesa hakutumia no yake... kuanza mishe za kwenda upande wa pili aisee nyie
 
Wakuu habari za asubuhi, jana nimefungua uzi kuelezea sisi tusio kuwa nacho maisha tunayopitia mpaka kukosa chakula na kuishia kula mlo 1 tu kwa siku nawenyewe kwa mbinde

Wapo walioguswa na kutoa ushauri mzuri nini cha kufanya pia wapo walio kejeli ( hawakosekanagi hawa ) pia wapo walioponda badala ya kutoa maoni ya kujenga
Wakuu narudi kwenu ni hivi tumeamua wife kuanzisha biashara ya dagaa wa bukoba japo tuanze na ndoo moja au mbili kwasababu ana koneksheni kule, kwann dagaa kwanza ni mboga inayotumiwa sana mtaani tulipo pia wife akanidokeza kuwa anaweza kuwa anatembeza hasa kwenye migahawa ya mama ntilie ile midogo midogo na akapata wateja nami nikaona ni wazo zuri

Shida inakuja ni ile ile mtaji, kianzio katika kupiga hesabu mtaji na usafiri inakuja kama elfu 60 hivi na faida unaweza kutoa 40k japo sina uhakika mpaka tufanye

Mimi kwa upande wangu nitaendelea kuhangaika hapa na pale ila plan yangu ni kufungua library japo ya kawaida tu ndogo kwasababu nina esperience nayo.

Please kwa atakayeguswa au kutusupport katika mwanzo wetu huu unaweza kutuma chochote kwenye airtel money 0787414221 au kama una kitu tutapokea namaanisha unaweza kununua mzigo ukatusapoti kwa kutupa mzigo na sio pesa kama utapenda hivo.

SIMULIZI YANGU MPAKA LEO NIKO HAPA

Nitawapa simulizi kidogo ya maisha yangu wenda kuna kitu mtajifunza.
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 31-35 kadiria humo, nimeoa nina watoto 4 wawili wa kike wawili wa kiume mtoto mkubwa ana miaka 8

Katika kukua kwangu mpaka najitambua (+18 ) nimejikuta katika mikono ya baba yangu mkubwa (R.IP) alishatangulia mbele ya haki na alikufa akiwa anajua simjui mama yangu hii nitailezea mbele huko kwani mma nimekuja kumuona baadaya miaka kama 20 japo upendo ni mdogo mno kulingana na yaliyotokea na sababu alizonipa niliona hazina mashiko pia hajawahi hata kwenda nyumbani kushukuru kwa kumlelea mwanaye ( nitalieleza huko mbele) baba yangu mzazi pia alishatangulia mbele za haki ( R.I P ) alinipenda sana mshua wangu

Mwaka 2002 nilibahatika kupata nafasi katika shule moja ya private hii ni baada ya jitihada za baba mkubwa na sista angu ambaye alikuwa kama mchepuko wa mwenye shule nahisi hii ndo ilinisaidia kupata nafasi pale pia nakumbuka hii kitu ilileta ugomvi mkubwa kati ya ma mkubwa na na mkubwa mama mkubwa akimlaumu na kumtolea maneno ya shombo ba mkubwa kuwa kwann kanichukua mimi wakati na yeye ana watoto.

Nilijitahidi kusoma kwa bidii sana huku nikijua maisha yangu mm ndo nitakaye yabeba. Nakumbuka ilifikia kipindi baba mkubwa yeye ndo alikuwa ananifulia unifomu zangu wakati ana watoto wakubwa tu na kipindi hicho walikuwa shule pia ingawa shule za serikali hii ni kutokana na ile ishu ya ma mkubwa kusema kuwa kwann mimi ndo nichukuliwe shule ya private ( wakuu hapa kuna kitu niwambie baba mkubwa alikuwa ni mgonjwa wa kifua kikuu yaani kukohoa mpaka unamuonea huruma na ndo kilicho muua maana dawa zimekuja hivi majuzi tu zimekuta tayari yeye kifua kisha chakazwa lakini alikuwa anainama ananifulia hadi nguo kwasababu wanae walikuwa wanagoma ikumbukwe bado nilikuwa mdogo nisingeweza kufua mwenyewe hasa uniform zikatakata )

Basi bhana nimesoma nikajitahidi darasani kufanya vizuri kiukweli darasani nilikuwa vizuri sana, hatimae mwaka 2008 nikamaliza darasa la 7, tukaanza maisha ya mtaani kwa miezi 3 huku tukisubiri matokeo ya mtihani wa darasa la 7 mungu si Yuda matokeo yakarudi nikiwa nikiwa nimefaulu kimbembe kikaanza naendaje shule kiukweli pale nyumbani kulikuwa hamna mtoto yeyote aliyewahi kwenda elimu ya sekondari hii ni kwasababu ya kipato baba mkubwa akachekecha kichwa ikabidi arudi kwa mfadhili wangu yule aliye nisomesha primary nitampa jina la Y( R.I.P ) naye alisha tangulia mbele za haki kuna watu nawamisi ila ndo maisha.

Mzee hakuwa na hiyana akasema atanipeleka kwenye shule za kata nakumbuka kipindi hicho hizi shule zilikuwa kama na miaka 3 au 4 kama sikosei zimeanza. Rasmi 2009 nikaanza kidato cha kwanza kama kawaida nikajitahidi kusoma sana huku nikisaidiwa na yale masomo ya shule za private si unajua kule mnakula msuli vyakutosha.
Basi bhana baada kama ya miezi 6 mzee akaona maendeleo yangu ni mazuri akasema inabidi anihamishe anipeleke shule za private pia ikabidi ufanyike utaratibu bhana we sijui nini kilitokea hadi wa leo sijuagi, ni hivi siku ya kwenda shule nakumbuka niliamka saa 11 asubuhi make shule ilipokuwa ilikuwa lazima nisafiri yaani kutoka wilaya x kwenda wilaya y mzee akamwambia mtoto wake ndo anichukue akaniandikishe shule na amalize taratibu zote bhana we ile tuko kwenye gari tumetoka kama lisaa limoja simu ikapigwa inabidi turudi hii sikuwahi kujua sababu ni nini, basi bhana mi nilikuwa nafata maelekezo, ikabidi turudi kitu kipya ni kuwa sikurudishwa nyumbani hapana nilipelekwa kwa mzee nikaanza kuishi kwa kijana wake hukh nikisubiri maelekezo mengine, ebwana wee mwezi wa 1 ukakata 2, huo wa 3 nao huo hapo sasa nimekuwa kama mtoto wa huyo kijana yaani nafanya kazi zote, nakumbuka nilikuwa naamka napika uji wa mke wake, chai ya watoto, nadeki nyumba, napika chakula cha mchana baada ya hapo kazi zilizobaki yaani za jioni kuna binti mmoja naye alikuwa anasaidiwa na huyo mzee na alikuwa anaishi kwa kijana wake kama mimi sasa yeye alikuwa anaenda shule asubuhi jioni ndo anarudi kwahyo kazi zote za jioni alikuwa anafanya yeye mimi kazi yangu ya jioni ilikuwa ni kuhakikisha maji hayakosekani pale japo kwa wakati ule nilichukulia kama mateso lakini vitu vimenisaidia ktk maisha yangu.
Sikumbuki vizuri ilikuwa mwezi wa ngapi ila nahisi mwezi 8 mzee alikuja pale kwa kijana wake na kumwambia kuwa kesho nijiandae naenda shule nilifurahia mno nilijiandaa hatimae nikaenda shule mazingira hayakuwa mabaya sana au mazuri sana nikakabidhiwa pale huyo kijana akaondoka sasa nimekaa pale make ilikuwa ni boarding school nakuja kugundua kuwa ni zile shule za Wale watu wanaotaka balance masomo yaani ulifeli somo fulani unataka ulirudie kwahiyo mimi pale nilipokelewa kama mwanafunzi wa Qt baada ya kuelewa sikuwa na kinyongo mimi nikasema nitakomaa ila nilikuja kugundua kwann mzee alinipeleka pale sababu kuu ni mzee aliona mbele maana kuna kipindi ilikuwa inafika sina karo narudi home ( kwa yule kijana nakaa tena kama miezi 3 ndo narudi shule hii ziwezi mlaumu mzee make mambo yake yalienda kombo kipindi hicho mpaka ikapelekea shule yake kuuzwa kwa roman catolik na hii nahisi ndio iliyomfanya mzee anafariki maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana)

Basi bhana pamoja na purukushani zote nilifanya mtihani wa QT nikawa nimefaulu vizuri hivo mwaka 2012 nikafanya mtihani wa form 4 ikumbukwe mazingira yangu ya masomo hayakuwa mazuri sana kutokana na ukosefu wa karo hapa ilinidi niruke yaani form 3 sikuisoma niliunganisha masomo ya form 2 na 3 kwa pamoja mwaka 2012 mwaka wa historia sitamsahau yule mma alikuwa waziri wa elimu kipindi hicho aisee alichotufanyia hatutamsahau kwanza picha linakuja nimesoma kwa kuunga unga pili matokeo yanatoka mara2 japo katika yote cheti changu cha form 4 ninacho mzee wangu ( aliyenisomesha ) kipindi hicho alikuwa tayari kafilisika vibaya mno aisee asikwambie mtu kama ulishawahi kushika pesa ikachomoka aisee hii isikie kwa jirani yako mma mwantumu na sio kwako hivo nilishindwa kuendelea na masomo ingawa nilikuwa nimefaulu japo sio kivile ( hapa kuna kitu sijawambia nikiwa shule pale kulikuwa kuna somo la compyuter hivo poket money yangu nilikuwa nikilipa kwenye somo la ziada la kompyuta na nilifaulu vizuri mno na cheti cha kompyuta ninacho pia)

Rasmi baada ya kumaliza form 4 nikaanza harakati za mtaani kutafuta na kujitafuta aisee hapa ndo kuna mengi mnoo ndo nilikuja kuanza kumtafuta mama, kupelekwa polisi na mengine mengi mnoo narudi mda si mrefu kuendeleza simulizi fupi ya life langu.....

Inaendelea
Mtanisamehe mmi sio muandishi mzuri wa simulizi hivo someni hivo hivo lengo ni kujifunza
JINA LINAKUJA NANI?
Ukitumiwa mtaji usije kuweka screenshot (picha ya muamala) yenye jina la mtumaji hapa.

Mimi nitatoa sadaka yangu ya mwezi kwako, nakutakia kila la kheri ukafanikiwe na familia yako.
 
Sikia nikuambie kitu kijana, uli kurupuka kuingia kwenye suala la ndoa wakati uchumi wako wa tia maji.

Ndoa sio ngono na nakupenda pekee, ile ni taasisi inayo endeshwa na watu ili iwe imara.

So life likizidi kuwa gumu, mrudishe wife kwao. wewe pambana kwanza.
Hii sio solution kama ambavyo vidole havilingani hatuwezi kuoa/kuolewa kwakua na mafanikio tu,ndoa ni zaidi ya material things,upendo wakweli kuheshimiana na kushirikiana,ukiyaweza yote hayo hata kama mtalala njaa maisha yataenda tu
 
Mkuu kwenye maisha usi pende ku operate kwa hisia Sana, hilo unalo lizungumzia ni suala la back in the 70,80 huko.

sikatai wavumilivu wapo, ila hilo sio life tena ni escape from sobibor.
"Where people relay in miracles than facts kudadadeki.

Vipi waki umwa ghafla?, nani ata wachangia?, luku, dharura au jf ndio mtaji wenyewe!
 
Mimi nitatoa sadaka yangu ya mwezi kwako, nakutakia kila la kheri ukafanikiwe na familia yako.
Mboju Kwa kusema AMINA utakua umeiruhusu hiyo pesa ikafanye kitu jumlisha katika maisha yako.

Lakini pia mwenyezi Mungu atambariki alietoa katika namna ya ajabu.

Na pia Mungu anibariki mimi kwa kukueleza hayo.

Sema AMINAAAA
 
Sikia nikuambie kitu kijana, uli kurupuka kuingia kwenye suala la ndoa wakati uchumi wako wa tia maji.

Ndoa sio ngono na nakupenda pekee, ile ni taasisi inayo endeshwa na watu ili iwe imara.

So life likizidi kuwa gumu, mrudishe wife kwao. wewe pambana kwanza.
Jinsi nilivyomsoma huyo jamaa umaskini wake unatokana na lifestyle mbovu nawafahamu watu wa staili hiyo huwa wanastruggle kwa muda mrefu sana kupata hela kwa ajili ya kula tu na kulipa kodi ya nyumba,na hapo watoto wake wakianza shule ndio kisanga zaidi.
Kitu kingine pia kinachomtesa huyu jamaa anaonekana ni mzito kwenye suala la kufanya maamuzi hayuko proactive.
Yaani kwa mfano yeye anafanya kazi za kuuza nyimbo au CD halafu unaona haikulipi na una familia kubwa halafu bado unaendelea kuing'ang'ania badala ya kujiongeza na kubuni biashara nyingine itakayoendana na mazingira aliopo au kuachana na biashara kuangalia hata vibarua mahali vitakavyompa pesa za uhakika,kitu kingine pia ana mentality kwamba pesa ya msaada inaweza kumkwamua kimaisha kitu ambacho si kweli utatumia siku chache baada ya wiki njaa itarudi palepale.
Hizi mentality zake zitamchelewesha sana.
 
Asiye sikia la mkuu, asi lalamike aki vunjika guu.
 
Sikia nikuambie kitu kijana, uli kurupuka kuingia kwenye suala la ndoa wakati uchumi wako wa tia maji.

Ndoa sio ngono na nakupenda pekee, ile ni taasisi inayo endeshwa na watu ili iwe imara.

So life likizidi kuwa gumu, mrudishe wife kwao. wewe pambana kwanza.
Mkuu naona kama hauna Experience na haya mambo ndiyo maana unasema jamaa alikurupuka kuingia kwenye ndoa.

Iko hivi huyu jamaa ni mtu mzima na ni mtoto wa kiume hivyo ni wazi back in the days kabla yakuingia kwenye ndoa alikuwa anashiriki tendo na huyo mpenzi wake(mke Kwa sasa).

Inawezekana alimpa mimba akaona hawezi mtenga wacha waoane tu ili walee pamoja, Hivyo basi kajikuta ndoani sio kwa kupanga no ni kwasababu ya matokeo ya kushiriki tendo na hawezi kutoa mimba au kumkana/kumtelekeza binti aliye na mimba yake eti kwasababu maisha magumu au hajajipata NO.

They decide to fight together that is.
 
Mkuu jina lako ni facts only ila hapa una leta masuala ya ramli tu, yaani kijana wa 35 bado hajui kilicho bora kwake?

Ok mtoto wa 1 ni bahati mbaya, wa 2,3 hadi 4 nao tuseme vipi?
Think twice before coming with weak answers, ili kuthibitisha hoja yako.

Hivi una jukumu la baba kudadadeki?, au ndio I'd yako nyingine hii 🤔
 
Back
Top Bottom