JamiiForums imeleta mapinduzi makubwa Tanzania

JamiiForums imeleta mapinduzi makubwa Tanzania

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,554
Reaction score
12,513
-Jukwaa hili hutoa nafasi kwa mtumiaji wake yeyote kuchapisha, mambo mbalimbali, kama vile habari, mijadala, na mafunzo mbalimbali, na hivi ndivyo ninavyolijua jukwaa hili.

Aidha, jukwaa hili pamoja na kuwa ni chombo cha habari pia huweza kutumika kama sehemu ya mijadala au mafunzo mbalimbali, nikuwa na maana mtu akiwa na ujuzi wake anaweza kuufundisha kupitia jukwaa hili kwa kuchapisha na chapisho hilo likadumu na kuwa msaada mkubwa kwa jamii ya sasa inayohitaji kujua mambo hasa kupitia program tumishi kama vile Google.

Ninapo andika chapisho hili nakumbuka miaka kadhaa nyuma miaka kama 8 hivi niliwahi kujiuliza nani hua anaandika Google? Kwanini vitu vinapatikana Google? nani huwa anaviweka?

Haya ni maswali yaliyonisumbua sana kila nilipotafuta kitu google kipindi hicho nipo sekondar na tekno zile ambazo ulikuwa ukiserch kitu picha inakuwa blue, haha.

Nakumbuka nilivyokuwa natamani kuandika namimi kitu kitokee google haha kunawakati nilifikiri vitu vyote vilivyomo google hupostiwa kupitia Facebook na nilikuwa najaribu kupost Fb kisha narudi kukiserch google kama kinatokea.

sikupata mahali pakupost ili kitu kitokee google! Hadi pale nilipogundua Google ni program tafutishi. Na hatimaye nilikuja kugundua sehem za kupost na Jf ni miongoni

Watu wengi wanatamani kupost makala zao zakuelimisha, kuburudisha, nk. Jamii furum inatoa nafasi hiyo kwa wadau wake, hivyo naweza kukiri kuwa ni maendeleo makubwa ya kitehama na kama jukwaa hili litatumika ipasavyo linaweza kuwa chanzo kikubwa cha maarifa, burudani, habari, n.k

Kazi kwenu wadau tumieni jukwaa hili kuelimishana na kufunzana mambo, usiwe mchoyo wa maarifa, fikiria kwamba kama kila mtu angekuwa mchoyo Leo hii ata ungetafuta kitu Google usingekipata.

Pia ninyi wenywe ni mashahidi kuwa kiswahili bado hakijaandikwa sana, na ndio maana kunavitu vingingine itakubidi kuvitafuta kwa Kichina au kingereza maana kiswahili bado hakuna aliyeandika mtandao ni kuhusiana.

Wito wadau andikeni
Gawana maarifa na kizazi kijacho!
Leo Mimi siandiki sana
 
Hakika JF ni jukwaa linalotoa uwanda mkubwa wa kuelimisha, kuburudisha na mijadala ya tafakuri. Lakini nimekuja gundua wanasiasa na wanaharakati wengi wameikimbia JF pamoja na kuwa na accnt zao humu. Uzuri wa JF kuwezesha uwanda mpana watumiaji kujadili mambo kwa undani umewafanya watu hao kukimbilia Twitter ambako hakuruhusu uandishi wa zaidi ya idadi fulani ya maneno.

Wanasiasa na wanaharakati wameona huko ndio salama kwao dhidi ya GT's, sababu hakuna detailed arguments ku counter attack post na propaganda zao za para moja.

JF itabaki kuwa sehemu ya wanaotaka kuujua ukweli sababu ukidanganya kuna mtu atakuja na maelezo ya kina kukanusha uongo wako.
 
Kazi kwenu wadau tumieni jukwaa hili kuelimishana na kufunzana mambo, usiwe mchoyo wa maarifa, fikiria kwamba kama kila mtu angekuwa mchoyo Leo hii ata ungetafuta kitu Google usingekipata. [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji109][emoji109][emoji109][emoji109][emoji109][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]

Katika hili mimi nimetimiza wajibu wangu na ninajivunia... Natambua kuna siku sitakuwepo... NITAKOMA KUWA lakini maandishi yangu yatakuwepo[emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
 
Masshele,
JF ni chuo chenye mafunzo ya kila somo.

Binafsi nimejifunza mengi katika ukumbi huu elimu ambazo nisingeweza kuzisoma mahali popote.
 
Ni kweli Jf imetusaidia wengi sana na wengine kama ungeiondoa katika historia zetu pengine sijui tungekuwaje. Mbarikiwe members wote mnaoanzisha thread kwa ku_share elimu na experiences zenu za kimaisha maana zinawasaidia wengi.
 
Back
Top Bottom