Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Hili bandiko limejaa mambo mazito na umeandika kwa hisia sana mpaka mimi mwenyewe limenipa msisimko. Pole sana kiongozi kwa yale unayopitia ila ninaamini kwa upeo na uwezo ulio nao utayashinda.

Hawa binadamu wenzetu walinyimwa MUONO na hii ni tatizo kubwa kwao. Uwezo wa kung'amua jambo kiundani na kubaini kama lina hasara na hasa kama hasara hizo ni za muda mrefu hawana kabisa.

Wameletewa elimu(kitu ambacho ni kizuri) lakini elimu hiyo imekuwa twisted kwa namna fulani kiasi kwamba inawajenga wakati huo huo inawabomoa bila ya wao kujua.

Angalia leo hii mwanamke anasoma hili aje ashindane na mwanaume na sio kuja kushirikiana na mwanaume kwenye ujenzi wa jamii iliyobora. Na hili tunaweza kuliona hata hapa kwenye huu uzi, wao wanaona elimu ni nyenzo ya kupambana na mwanaume.. Inasikitisha kweli.

Sipingani na mwanamke kuelimika ila napingana na namna ambavyo elimu inatumiwa na mwanamke hasa kwenye ushirikiano wake na mwanaume kijamii. Wengi wanaweza wakaniona kama mtu fulani niliyechanganyikiwa kwa kuongea hivi lakini hapa kunaa tatizo na linahitaji kuangaliwa.

Mfumo wa haki sawa(gender equality) hapo awali ulikuwa na dhamira nzuri sana tofauti na ilivyo leo hii, ililenga kumpa mwanamke uhuru sawa na mwanaume na access ya mambo ya msingi kama elimu. Lakini haukulenga kumbadilishia mwanamke majukumu au kumpora nafasi yake ya asili.

Leo hiii mfumo huo jinsi unavyokuwa practiced ni kama umekuja kumfanya mwanamke kuwa mshindani wa mwanaume, na matokeo yake umetuvurugia familia na jamii nzima kwa ujumla.

Na kwa bahati mbaya sana hawa wenzetu wao hawalioni hili kama lina athari na badala yake wanaona ndio matokeo ya ukombozi wenyewe.

Waanzilishi wa huu mfumo wana ajenda zao za siri ambazo zinahitaji jamii iliyopalanganyika hili ziweze kupenyezwa kwa urahisi. Na mfumo huu ni nyenzo sahihi ya kutimiza ajenda hizo.

Ukiangalia jamii yetu ya sasa hivi sio sawa na zamani kimaadili na hata kuroho. Na kupitia mabadiliko haya kuna watu wananufaika bila ya tulio wengi kujua.

Siku hizi kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu yanaonekana ya kawaida tangu tuingie kwenye huu mfumo unaosemwa kwamba umeleta uhuru.

Acha tuendelee kuwakumbusha na wale ambao bado hawajajua nini kimaendelea kupitia forums kama hizi.
 
Wao wanaita ukombozi yaani Ukiskiliza fikra zao utafikiri labda wanaume ni wanyama fulani hivi wasiokuwa na uhuruma hata kidogo na muda wote wao ni kunyanyasa tu wanawake.

Yaani elimu inamfanya aone kwamba Mwanaume alikuwa ni adui yake na muda wote alikuwa amemuweka kwenye cage.

Wakati hao hao wanaume ndio wamekuwa waki sacrifice maisha yao kwa ajili ya wanawake tangu kuumbwa kwa huu ulimwengu.

Mwanamke mwenye fikra zilizopinduliwa na elimu yake hafai kuwa mke.
 
Kwa kweli nimejitaidi kupitia article yako vizuri, lakini nasikitika kusema sijaona uliposimama na hoja. Naona kama umekuja tu, kuendeleza mvutano usio na tija.

Anyway, tunakushukuru kwa mchango wako. Ni imani yetu, ipo siku isiyo na jina....mtaelewa vizuri athari za hiki, kinachoongelewa hapa.
 
Well said....thanks.
 
Mkuu Nyenyere kuna mada Fulani ulipost hapo nyuma na kwa kweli nilitofautiana sana na mtizamo wako(na mpaka sasa natofautiana na wewe)

Lakini kwa mada hii ya leo nakuunga mkono asilimia mia moja na naomba niongezee hoja kadhaa hapa chini kuunga mkono mada yako

Mkuu kwa sababu ya mapinduzi yalifofanyika na yanayoendelea kufanyika kila siku,leo hii tunapata familia na vizazi vibovu kuwahi kutokea,kwa nini?

leo hii baba na mama wote ni wafanyakazi kuondoka aubuhi kurudi usiku,watoto wameshakula wamelala,anayeshinda na watoto ni dada wa kazi ambaye haijulikani anashindaje na kuwatendeaje watoto,mama anapoondoka anaacha tu maagizo dada utampa mtoto uji,utamwekea katuni,utahakikisha anafanya homework,mtoto ni wa dada wa kazi?dada wa kazi anajua thamani ya yule mtoto?akiharibika dada ana hasara yeyote?na akiwa mtu mzuri kioo cha jamii,ni kwa namna gani dada wa kazi anafaidika hivi kwamba atajitahidi kwa kadri awezavyo kumlea mtoto ipasavyo?

kwa mfano huo mdogo tu wale ambao wamewahi kuona madhara ya aina hi ya Maisha wataelewa nachokisema ila kwa wale ambao wanaamini njii hii ya Maisha ni sawa si ajabu huko mbeleni watu watakuja kuconfess humu (painful ad regret Confession)

Kiasili na kulingana na uumbaji mwanaume aliumbwa kutafuta kwa maana ya kwamba mke alipaswa akae nyumbani atunze watoto muda wote baba anapokuwa katika mihangaiko ya kutafutia riziki mke na watoto wake,ni aina hii yamaisha iliyofanya familia kadhaa za miaka kadhaa kuwa bora na kutokeza vijana wa kiume na mabinti wa kike wenye kutegemeka na kujiheshimu,mama walikuwa wakitumia muda wao mwingi kutunza watoto wao na kuwafundisha lilo sawa na lilo na kosa pia,haikuwa rahisi kwa binti au kijana kuharibika na mama shindwe kuona mbadiliko hayo na kutoa ripoti kwa baba ambaye angeshughulikia hali hiyo kabla mambo hayajaharibika kabisa

lakini leo poor us kuna uwezekano mtoto kashaharibika sana tu (labda kawa mvuta bangi,katoa mimba za kutosha,kawa shoga,kawa mlevi) na bado mama au baba hajui kuhusu yote hayo,watajua saa ngapi wakati wote wako kazini bize kutafuta pesa?nani atampa mwenzie ripoti kuhusiana na maendeleo ya mtoto? dada wa kazi? dada wa kazi wanawajua vizuri watoto wenu? inauma lakini kutokana na aina yetu ya Maisha ya siku hizi,inakuja kujulikana kuwa mtoto kafikia stage ya point of no return na hakuna kinachoweza kufanyika kumsaidia tena just kwa sababu mama na baba wote walikuwa bize kuzitafuta pesa,what for? Maisha bora,,,,Maisha bora yapi?kupoteza watoto wenu mkiwa mmebaki na pesa zenu nyingi??
 
Good note mkuu Dutu J

kulingana na maandiko uliyoyataja hapo huo ni mgawanyiko ulio fair kabisa,na amini nakwambia yeyote anayeyaishi maandiko hayo,maisha yake ni mfano kwa wengine na kwao furaha ni kitu cha kawaida kabisa

be blessed mkuu
 
Kweli kabisa mkuu, tatizo ninaloliona kwenye nyumba za ibada ni mapato makubwa yanayotoka kwa wanawake. Kwa sababu ya uwezo wao mdogo kufanya reasoning, wamekuwa target ya watumishi wengi. Hii ni mbaya sana lakini ukweli inabido usemwe tu.
Hawa watumishi wenyewe ni perpetrators wa huu mfumo haribifu na una maslahi sana kwao sio wa kuwaamini kabisa.

Yaani hawa sijui wanasaiokolojia,wachungaji, wahamasishaji, wasululishi wa migogoro ya ndoa ni washirika wazuri sana wanao prolog huu unaoitwa ukombozi wa mwanamke.

Na tusigemee kabisa kama watasaidia hata kupunguza athari zitokanazo na huu mfumo maana unafaida kwao.

Uwepo wa matatizo yetu ya kijamii hususani ya mahusiano ndio uhai wa maslahi yao, siku matatizo hayo yakiisha hata maslahi yao pia yatakuwa hatarini.

Kama umewahi kuwafuatilia hawa akina Chris mauki,Eddy makenge na wengineo mara nyingi huwa wanaongea vitu ambavyo wanawake wanapenda kuviskia. Mara nyingi wanaongelea sana makosa ya wanaume na kufunika funika makosa ya wanawake na hata ushauri wanaoutoa ni ushauri unaoharibu zaidi kuliko kujenga sema wanajitahidi kucheza na saikolojia ya wanawake.

Na wanafanya vile makusudi kabisa ila wanachoangalia wao ni account zao kuongezeka unene.
 
ujinga huu, kama tukianza kufuata ujinga wa kizamani hata utumwa ulihalalishwa. Kma hutaki mwanamke afanye kazi wafanyie hivyo wanao wa kike, ni dunia huru hii, fursa sawa kwa kila mtu
Huko Ulaya kuna conservatives wanaoitwa far right ambao wana mawazo kama yako, wanashangaa pia kwa nini watu weusi wanapewa nafasi kubwa hadi wengine kuwa Rais kwenye nchi za wazungu, lakini hawashindi watabaki kuumia tu kama wewe unavyoumia
 
Asante mkuu,

Hakika umejazia mambo ya muhimu sana, hongera kwako chief.

Kikubwa tuendelee tu kukumbushana ya kwamba, waathirika wa hii kitu sio tu wanawake. Bali pia tufahamu kwamba, lipo kundi kubwa la wanaume wenzetu, walio-affected kwenye hili suala...!!

Hivyo tunavyojivalisha mabomu ya kuliteketeza suala hili, katika jamii zetu. Tunatakiwa tufahamu kabisa, tunaenda kupambana na makundi yote mawili ya waathirika (mwanaume & mwanamke).

Kwa msingi huo ni wazi tunaona kwamba, ili kufanikisha kuijenga jamii mpya, ni lazima tujidhatiti kwa hali na mali......a part from that, ni lazima TUTASHINDWA!
 
Ujinga uko wapi hapo?

Nani kasema hapa kwamba mwanamke asifanye kazi?

Umeelewa content ya mada lakini au umekurupuka tu kutoka huko ulipokuwa na kuja ku blab hogwash hapa?

Huko ulaya na Marekani conservatives bado wana family stability kuliko hata hao wapumbavu wa liberals ambao wanaonekana kukuharibu akili. Tafakari kuhusu hili
 
Upo sahihi kabisa, kiongozi.

Ni kweli huu uharibifu wa jamii zetu unaofanyika, una faida kubwa sana kwa baadhi ya watu! Na hii inajidhihirisha wazi, kutokana na mambo yanayofanywa/kuongelewa na watu hao, ambao wengi wao wapo kwenye makundi haya ya wachungaji, makungwi, wanasaikolojia, waongeaji n.k

Simply, still tuna safari ndefu....!!
 
Ujinga huo aliouandika
Nadhani wewe ndio hujamuelewa mleta mada, pengine kamsome tena
Dunia imebadilika, kila mtu ana haki ya kupata fursa ya elimu na kufanya kazi yoyote kama anaweza kuifanya
Kama hupendi pole, ndio mambo yalivyo na yataendelea kuwa hivyo, haturudi karne ya 19 tena
 
Nimepitia article yako vizuri, lakini nasikitika kupata ukakasi juu ya msingi mzima wa ufahamu...

Nadhani ni vyema, ukapitia tena uzi huu kiutaratibu na kwa umakini.....ili uweze kung'amua msingi mkuu wa kinachoongelewa hapa.

Asante.
 
Nimepitia article yako vizuri, lakini nasikitika kupata ukakasi juu ya msingi mzima wa ufahamu...

Nadhani ni vyema, ukapitia tena uzi huu kiutaratibu na kwa umakini.....ili uweze kung'amua msingi mkuu wa kinachoongelewa hapa.

Asante.
article yangu ipi? sijaandik article mimi, nime comment. Msingi wa kinachoongelewa nimekielewa, anasema mwanamke arudi kwenye majukumu yake ya ki traditional kama kupika na kulea watoto, na mwanaume ndio awe mtafuta kipato
 
Hapawezi kuwa na usawa kati ya mwanaume na mwanamke maisha yakaenda....
Wamama na wadada tunaweza kuwa na haki sawa ya kupata huduma za kijamii kama elimu, ajira, biashara, burudani etc lakini hatuwezi kuwa sawasawa na wanaume wala wanaume hawaezi kuwa sawa na wanawake kwani kila mmoja ana majukumu ambayo aliumbiwa

Kwenye imani zetu tumejifunza toka awali kabisa kwenye uumbaji mwanaume ni nani na mwanamke ni nani pamoja na majukumu yao. Pia desturi zetu hazikua mbali na imani zetu kuhusu hili.

Mambo yale ya Beijing tuyaache Beijing, sisi tuishi kwa asili yetu binadamu ilivyo na pia miongozo ya imani zetu

Maoni yangu binafsi
 
Safi, umenena vizuri sana!

Endapo kila kitongoji katika jamii zetu, kikawa na wanawake kama wewe kumi tu. Aiseeh bila ubishi tutapiga hatua kubwa sana za kimaendeleo, kuanzia kwenye msingi wa familia mpaka nchi kwa ujumla.

Asante sana Dada, ubarikiwe!
 
Umepoteana huelewi maudhui,by the way sina tabia ya kunuku kila kitokacho ulaya. Mmelishwa matango pori nasasa hamna furaha kama ilivyokuwa zamani. Kama unabisha angalia waliokimbilia upepo wa kisulisuli, ni aibu kwa janga mnalotengeneza wenyewe.

Habari ya ulayawaachie wenyewe, tujadili ya kwetu. Elimu haikupaswa kumwondoa mwanamke kwenye majukumu yake ya msingi, lakini kilichopo sasa ni nini? Naamini wazazi wako walikulea vema ingawa wewe hutaki kuwatendea hivyo wanao, ubataka walelewe na dunia. Ni upuuzi usiomithilika.

Kama unadhani mimi nanung'unika basi umepotea, mimi najaribu kushauri kuhusu maadili na sababu ya wanawake kujikuta wakiwa na wanyonge pale ujana wapo unapoondoka. Wanawake ni short sighted hata kama utabisha, wanasombwa hovyo na kila upepo unaokuja na ndio maana ni target kubwa ya kila jambo jipya, iwe fashion, urembo, mavazi, imani mpya n.k. Akili zao zinavutwa kila kinachoonekana ni kitamu machoni hata kama mwisho wake ni mchungu, hawana uwezowa kuchuja mambo. Ndivyo walivyoumbwa.

Starehe na kujidanganya hudumu kwa muda mfupi sana kwa mwanamke wa kizazi kipya, asiyeheshimu kuumbwakwake kama mwanamke, ambaye anadhani ushindani na walioumbwa wanaume ni jambo la kutukuzwa, lakini mwanamke anayeijua nafasi yakeana chance kubwa ya kuwana furaha idumuyo maisha yake yote. Mwanamke hakuumbwakushindana na mwanamume bali kumsaidia kufikia malengo ya maishawakiwa kama familia moja. Sasa wanawake waliojanjaruka kama wewe na kujiona ni wenye kupambana na wanaume hupigana na vivuli vyao wenyewe kwani watacheka mwanzoni, tena kwa muda mfupi sana, lakini mwisho wao huwa ni kilio na majuto makuu.

Elimu ilikusudiwa kumtoa mtu kwenye ujinga na kumpeleka kwenye hekima na busara, lakini badala yake imefanya kinyume chake. Wacha mtumike kwa starehe na kuwaburudisha walioharibika akili pia, lakini usisahau kuwawakati ukuta.

Amina.
 
Sasa unashauri wa kike wakizaliwa wasipelekwe shule wasubiri ndoa ama?.

What is your solution?.
Tatizo tumeliona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…