Jamii Iliyopotoka kimaadili

KasomaJr

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
367
139
Ni Tanzania pekee ambayo unaweza kuona haya toka Kwa viongozi wa chama(makada) waliojifunika shuka la u-serikali.

Ni aibu sana kwa jamii kuwa na viongozi ambao hawawezi kuweka na kuheshimu mipaka ya kiutendaji.

Ni katika awamu hizi mbili (2) za mwisho ndiyo tunashuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili ya viongozi tena Kwa Kasi ya ajabu Sana, yetu wapo viongozi wenye akili kabisa, wenye maadili kabisa, waliolelewa na kuongoka vyema kabisa, kuanzia taasisi za kidini, kiraia na hata kiserikali.

Haya yanatokea kukiwa na statesmen kabisa ambao hawakulelewa hivyo, wamekuwa viongozi Kwa miaka mingi na walijua wazi mipaka ya kimaadili ya Uongozi.

Hii naiona kama hatari kubwa Sana tunayo iendea, kuelekea taifa lisilokuwa na viongozi waadirifu, wasio na nidhamu wala heshima kwa yeyote yule isipokuwa mwanachama, Kada au kiongozi mwezake tena katika itikadi moja.

Maoni/Ushauri/Ufumbuzi
1. Viongozi wa kidini ambao wanajitambua (wasio na mlengo wowote wa kichama) watusaidie kuanzisha mjadara wa kitaifa wa nini tunapaswa kufanya kama nchi kuondokana na ombwe hili la Uongozi.
2. Statesmen watusaidie kupiga kuonya na kukemea haya yanatokea katika Jamii.
3. Madai ya Katiba mpya yatakayo ainisha maadili, wajibu na Uongozi unao fuata Sheria viwe vipaumbele vya mwanzo kabisa. Na viainishe adhabu kubwa ambayo kiongozi anayekiuka hayo anastahili kupata.
4. Ongezeeni...
Screenshot_20180917-101144.jpg
Screenshot_20180917-101216.jpg
Screenshot_20180917-101206.jpg
 
Back
Top Bottom