Jamhuri ya wajinga na falsafa za mabwanyenye, Biblia inasema Kinyonge hakitauona ufamle wa Mungu. "Anaongoza wanyonge?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Jamhuri ya Wajinga na falsafa za mabwanyenye.

_______________________________________________

Wanafalsafa wa Kifarao, Kilatini na Kigiriki kupitia kitabu chao cha kiroho wanasema wazi kuwa, Tujapopita katika bonde la uvuli wa mauti hatutaogopa mabaya, gongo lako na fimbo yako vitatuongoza ehe bwana kwa mkono wako wa chuma wa trilioni moja na nusu,

Njia ni pana iendayo upotevuni na wanaoiona ni wengi, bali njia iendayo uzimani ni nyembamba
na waipitao ni wachache. Wakati wewe unasema mithali za kidunia ya kizembe za "wengi wape", Falsafa ya kiroho inasema "wateule ni wachache". Huenda wateule ni ni walao na kusaza mezani pa Chakubanga kwa gharama ya mjinga mimi na wewe.

Amini kila unalolijua unajua, ni uongo, Dunia inaongozwa na kiumbe mwenye nguvu, lakini aweza kuwa mjinga kwani hata mjanja alizaliwa na mjinga, kinyonge kimezaliwa kupiga kura, na kuongozwa, na katika dunia ya kizembe kinyonge kimepewa nafasi tu ya kukibariki chenye nguvu kwa mtindo wa kura kula...

Filosofia ya kiroho kupitia kitabu kikuu cha kiroho imetanabaisha kuwa kinyonge hakitaiona pepo, siku ukipata kuiishi dunia yako utaamua juu ya yaliyo usoni pako.

Nami nakuambia wewe kiumbe dharimu na chukizo la dunia, si mwili na macho yako ya nyama vilivyokufunulia ... Wewe ni nan? Kwanini upo, amua sasa kuyafunua yaliyofichwa ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio halijapata kusikia.

Enyi watu wa Jamhuri ya Muungano wa Wajinga, nani kawaloga? Ni kweli hamjui ghala lenu la zabihu trilioni moja na ushee nani katweza? Hamjui mchezo wa haradari na lulu ulivyokuwa? Nani alikrimu kondoo wenu mliowapata kwa jasho na moshi wakaachia utwa na kuunga juhudi za kimweri? Hakika mwastahili kutoswa kwenye tanuri la moto.

Mjinga nashika tama nikitafakuri ujinga wenu kwa maumivu makali yanayogonga hadi utosini, eehe zee la madevu, nibariki mie kiongozi mwenye uchu wa madaraka na pesa! Naaam, Wakati silaha ya mjinga na mpumbavu ni madaraka, basi kwa yakini, Silaha ya mnyonge ni ukweli tu, Mnyonge anahitaji elimu tu hata ile ndogo tu yakuambiwa hiki ni uongo na ukweli wake ni huu. Kwa hakika silaha hii itamtoa mjinga na mpumbavu madarakani hata kama katika upumbavu wake aliziamuru mbingu na nyika kufunga na kufungua.

Himizeni mnyonge ajitambue, himizeni mnyonge amjue mpumbavu na mjinga, himizeni mnyonge atambue walioshiba si suluhu kwake. Himizeni mnyonge atambue mjinga na moumbavu hampigi kibaba cha unga kama fadhila bali ni wajibu wake unaopunjwa.

Mkifanya hayo mnyonge pekee ndio hulibadili Taifa, hubadili majina ya miji na historia, hubadili fikiriko na hubadili sheria. Walioshiba hawaleti mageuzi, walioshiba hawafanyi maendeleo, walioshiba hawafikiri juu ya kufa kwako, ni ukweli usio na shaka kwamba masikini tu ndio hufikiri juu ya kifo.

Enyi wanyonge mliotawazwa kwa unyonge wenu ili mpumbavu na mjinga ale mema ya nchi, amkeni sasa sikieni sauti za werevu wachache walioshushwa na maanani wakilisaka taji lenu la ushindi, amkeni unganeni nao, uongo mliolishwa karne na karne umekoma, simameni mhesabiwe.

Plato katika andiko lake la The Republic (Jamhuri ya Plato) anawasisitiza kwamba wanyonge ni daraja la wajinga na wapumba waliojitwalia madaraka. Na katika hili anaungana na Napoleon Hill katika andiko lake la "Outwitting The Devil" yeye akisema katikati ya wanyonge, wapo wajinga wachache ambao kula yao inategemea hisani ya watawala, hawa hawajui kuwa ni wajibu wa watawala, bali huamini ni hisani. Wapo tayari kumuua mnyonge yeyote apigae ukelele juu ya mtawala....

Aminini nawaambia, kenge wa masika wataibuka wengi kuzuia msifunguliwe ujinga wenu, kwakuwa kwa ujinga wetu mwanakondoo wa thamani ya trilioni moja na ushee, ameliwa kwa jasho la mjinga mie nawe

Acheni magumu yenu ya mtu moja moja, unganeni katika magumu ya umma,

Na Yericko Nyerere
 
Safari ni ngumu maana mawimbi ni makali na giza limetanda nikitizama kule namuona nahodha anasinzia lakini cha kushangaza ni kwamba abiria wanacheka na kushangilia ....! Ee mola tunusuru ...!
 
Well said! Wanyonge simameni tutee maslahi ya taifa letu. Mali na kodi zinafaidiwa na watu wajanja wajanja tu.


wanyonge tunakamliwa katika ulipaji kodi anaenda kula asiyejua ni namna gani tunahangaika huku mtaani.
 
Watu wanaitwa wanyonge halafu wanashangilia. Inatupasa kupaza sauti ili kila Mtanzania aujue kuhusu wizi/ufisadi huu. Naanza kuelewa kwanini walizuia Bunge LIVE.
 
Laiti kama kuna wawili watatu kule jikoni wakisoma bandiko hili na kulielewa hata kidogo basi tungepata hata robo jibu la zilipo! Lakini Mungu ni mwema kwani hata Yesu aliona yale matundu yaliyorobolewa ukutani mwa nyumba ya Zakayo kwa ajili ya kufichia fedha hata kabla hajaikaribia nyumba ya Zakayo na kumwamuru akazitoe na kuwagawia wahitaji! Hata hili kuna atakayeonyeshwa zilipo tu naamini!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom