Jamhuri ya Wachuuzi

Jamhuri ya Wachuuzi

singojr

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
5,315
Reaction score
6,896
Uchaguzi umekwisha kwa namna yake ya ajabu ambayo kila mmoja ameondoka na moja kichwani. Kwa aina ya Rais tulie naye ambaye ni king'ang'anizi na hana mjadala kwenye aliloamua, tunajua fika baada ya mbilinge za uchaguzi kuna baadhi ya vikwazo vitakuja na hata kubali kuwa mnyonge.

Uhakika wa vikwazo kuja upo wazi wazi lakini tumejipanga vipi kuvikabili. Kama ilivyokuwa kwa corona Je, tutaibuka kidedea. Kama tukiwekewa vikwazo na tukashinda basi tutakuwa taifa huru linalojitegemea kiuchumi kama tutaanguka basi tutakuwa tumerudi nyuma sana kama taifa.

Kama tumedhamiria kusimama na kujitegemea ni wakati sasa wa kuachana na uchumi wa kuchuuza vitu. Ukitembea kwenye masoko, stendi za mabasi na pembezoni mwa barabara utakutana na meza lukuki zimejaa vitu kutoka China vingi vikiwa na ubora hafifu.

Sekta za kilimo na viwanda zinakufa, vijana wengi wamegeuka wachuuzi. Vijana wengine wasomi wenye taaluma mbalimbali wamekuwa wachuuzi wa online. Je, tutaweza kuhimili vikwazo? Tuna taifa ambalo vijana hawajui wimbo wa taifa lakini wanajua nyimbo za Diamond.

Tuna taifa la wambea na lisilo la wachapakazi, juzi mchezaji wetu Samatta amesitishiwa mkataba na club ya Aston Villa.

Umati wa watu waliojaa kutoka Tanzania wakilaani ilionyesha ni kiwango gani watanzania wako kwenye mitandao muda mwingi kuliko kufanya kazi, ukilinganisha hata na taifa la Uingereza watu wake wakiwa kwenye lockdown ya Covid19.

Ili kuweza kuhimili vikwazo vinavyokuja lazima tuwe tayari kufanya kazi lazima tuwe na viongozi wanaowaza na kupanga mipango kwa umakini. Kama tukijipanga karata hii ya vikwazo tukaitumia vizuri inaweza kuwa mwanzo wa kusimama kama taifa.
 
Hizi taarifa za vikwazo kwa nchi yetu umezipata wapi?
 
CCM HAWAELEWI KUWA KILA KIFAA NI CHA CHINA...

Vijana hawana ajira. WANASOMA ELIMU YA KUCHORA PANZI NA INZI.

....ULAYA HAKUNA INZI SIJUI KUCHORA INZI KUNAWASAIDIAJE KWENYE MAISHA.
 
Sheria na kanuni za vikwazo zipo wazi na tumekiuka vingi sana. Hakuna namna tunaweza kukwepa vikwazo
 
CCM HAWAELEWI KUWA KILA KIFAA NI CHA CHINA...

Vijana hawana ajira. WANASOMA ELIMU YA KUCHORA PANZI NA INZI.

....ULAYA HAKUNA INZI SIJUI KUCHORA INZI KUNAWASAIDIAJE KWENYE MAISHA.

Tunasoma nadharia nyingi ambazo haziko applicable kwenye maisha
 
Huu uziwako nakwenda kuufanyia binding, ni bonge la study na unafaa kutumika kutolea lectures katika vyuo vikuu.....

Asante mkuu, lakini utaona vijana wengi wanakimbilia kwenye jukwaa la burudani kudiscuss kuongeza nguvu za kiume na kutafuta video za "koneksheni"
 
Uchaguzi umekwisha kwa namna yake ya ajabu ambayo kila mmoja ameondoka na moja kichwani. Kwa aina ya Rais tulie naye ambaye ni king'ang'anizi na hana mjadala kwenye aliloamua, tunajua fika baada ya mbilinge za uchaguzi kuna baadhi ya vikwazo vitakuja na hata kubali kuwa mnyonge.

Uhakika wa vikwazo kuja upo wazi wazi lakini tumejipanga vipi kuvikabili. Kama ilivyokuwa kwa corona Je, tutaibuka kidedea. Kama tukiwekewa vikwazo na tukashinda basi tutakuwa taifa huru linalojitegemea kiuchumi kama tutaanguka basi tutakuwa tumerudi nyuma sana kama taifa.

Kama tumedhamiria kusimama na kujitegemea ni wakati sasa wa kuachana na uchumi wa kuchuuza vitu. Ukitembea kwenye masoko, stendi za mabasi na pembezoni mwa barabara utakutana na meza lukuki zimejaa vitu kutoka China vingi vikiwa na ubora hafifu.

Sekta za kilimo na viwanda zinakufa, vijana wengi wamegeuka wachuuzi. Vijana wengine wasomi wenye taaluma mbalimbali wamekuwa wachuuzi wa online. Je, tutaweza kuhimili vikwazo? Tuna taifa ambalo vijana hawajui wimbo wa taifa lakini wanajua nyimbo za Diamond.

Tuna taifa la wambea na lisilo la wachapakazi, juzi mchezaji wetu Samatta amesitishiwa mkataba na club ya Aston Villa.

Umati wa watu waliojaa kutoka Tanzania wakilaani ilionyesha ni kiwango gani watanzania wako kwenye mitandao muda mwingi kuliko kufanya kazi, ukilinganisha hata na taifa la Uingereza watu wake wakiwa kwenye lockdown ya Covid19.

Ili kuweza kuhimili vikwazo vinavyokuja lazima tuwe tayari kufanya kazi lazima tuwe na viongozi wanaowaza na kupanga mipango kwa umakini. Kama tukijipanga karata hii ya vikwazo tukaitumia vizuri inaweza kuwa mwanzo wa kusimama kama taifa.
Tumeruhusu mshenzi ashike nchi tutajuta.
 
Narudia tena nchi ilikuwa Jamhuri ya wachuuzi wa biashara za Uchina.Je taifa linafaidika vipi?
 
Back
Top Bottom