Jamhuri ya Muungano ya Walalahoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamhuri ya Muungano ya Walalahoi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Aug 25, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Oktoba ndiyo hiyo ina karibia na baada ya takribani miezi miwili Tanzania ina piga kura. Tofauti ni kwamba huu siyo uchaguzi wa kawaida. Hapana! Tuna chama kimoja chenye nguvu zinazo pungua lakini bado kina nguvu za kutosha na pia tuna chama chenye nguvu zinazo ongezeka lakini bado hakina nguvu za kutosha. Ni imani yangu kwamba chama chenye nguvu bado kita shinda uchaguzi huu lakini matokeo yake yata kuwa fundisho kubwa kwao. Fundisho hilo lita kuwa ni kuto dharau wapiga kura walalahoi ambao wamesha choka na hali iliyopo lakini bado hawaja jua haswa wakimbilie wapi.

  Walalahoi ndiyo waku leta mabadiliko. Nasema hivi kwa sababu ukiacha walalahoi (ambao kwa Tanzania ni zaidi ya 80%) Tanzania kuna baki makundi mawili. Kuna wale maslahi yao yata kayo lindwa na hali kuendelea ilivyo na kuna wale ambao kwao haijalishi nani yuko madarakani. Sasa je raia wa hii jamhuri ya walalahoi wata pigaje kura 2010?

  Nadhani jamhuri hii ya Walalahoi ina matatizo. Iweje Walalahoi ambao ni zaidi ya asilimia 80 waendelee kupiga kura vile vile miaka nenda rudi huku waki baki kuwa walalahoi? Ni kwamba hawajui ulalahoi wao na uongozi wa kisiasa una uhusiano wa karibu? Je ni hulka ya Walalahoi kudhani kwamba hali yoyote mtu aliyo nayo ni mapenzi ya Mungu ndiyo ina waponza? Au katika nchi ya wapiga porojo ni vigumu kwao kujua haswa nani ata kuwa mtetezi wa maslahi yao na nani anaongea tu majukwani?

  Kwa idadi yao tu hawa walalahoi wana weza kufanya mabadiliko makubwa. Wana nguvu kubwa katika umoja kuliko wajuavyo. Tatizo ni kwamba 1) Hawana umoja na 2) Hawa jui nguvu yao kutokana na propaganda ambazo wame lishwa miaka nenda rudi.

  Wengine wote wata piga makelele wanavyo penda ila bila Walalahoi wenyewe kutaka mabadiliko hamna kitakacho haribika. Bila wao kutetea maslahi yao wenyewe Tanzania haita songa mbele. Tanzania ni Jamhuri ya Muungano ya Walalahoi na nyakati hizi tuna hitaji Walalahoi kuliko wakati wowote ule. Maana asilimia 20 iliyo baki haiwezi kuleta babadiliko peke yake na hata kati ya hao asilimia 20 kuna ambao hali iliyopo wao wame ridhka nayo na wangependa iendelee. Tuombe Mungu raia wa jamhuri hii waamke la sivyo miaka nenda rudi tutaendelea kuimba mwimbo ule ule pasipo mafanikio.
   
Loading...