Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Serikali ya mapinduzi Zanzibar

Hii reply inaitwa mtazamo kimo cha mbilikimo ni wapi nimesema muunganiko ni mbaya ama uvunjwe!? Usikurupuke tulia soma kitu ukielewe kabla hujakimbilia kujibu! Una haraka gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Usipoteze mda,tumia fursa,nenda mji wenye bandari ya bahari ukaone,jinsi watu wanavyochanfamkia fursa ya pesa.Na wewe utabaki kupigs kelele.Mwalimu Nyerere,aliona mbali,hii biashara,ni nzuri sana,ya mazao ya wakulima,kupeleka Zanzibar,au wanunuwe wao kutoka kwako.Acheni ubivu,changamkieni biashara za mazao ya kilimo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mahali utahoji uhali wa muungano ama ukandamizwaji wa Zanzibar ama Tanganyika alafu ndani yake usitaje dini uwe uislamu au ukristo. Andiko lako ni kweli hujataja dini lakini ndani ya hoja yako mtazamo utakaopatikana ni wa dini hizi mbili.

Na habari ya muungano wa Tanganyika na zanzibar base yake ndio iko hapo. Utamkumbuka Lukuvi na hofu aliyobainisha nyakati za nyuma.
Zanzibar kuna fursa nyingi za biashara kutoka bara,kule mahotel ya kitalii,kuna watu binafsi,wote hawa wanataka kule.Kuke kunatakiwa Mchele,viazi,maharage,vitunguu saumu,vitunguu maji,maharage,karoti,hoho,nyanya nk.Wajanja nafasi wanaitumia,wanapeleka hizo bidaa.Nyinyi mwakalia kulaumu.
 
Hakuna mahali utahoji uhali wa muungano ama ukandamizwaji wa Zanzibar ama Tanganyika alafu ndani yake usitaje dini uwe uislamu au ukristo. Andiko lako ni kweli hujataja dini lakini ndani ya hoja yako mtazamo utakaopatikana ni wa dini hizi mbili.

Na habari ya muungano wa Tanganyika na zanzibar base yake ndio iko hapo. Utamkumbuka Lukuvi na hofu aliyobainisha nyakati za nyuma.
Mimi hoja yangu iko wazi
Utambulisho wa Tanganyika kishapo serikali ya Tanganyika ili kuwe na uwiano sawa yanapikuja maswala ya muungano na yasiyo ya muungano

Hoja yako ina walakini mkubwa kwakuwa Tanganyika ni ya watu wa imani zote na hata wakati wa chaguzi viongozi huchaguliwa na watu wa imani zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hoja yangu iko wazi
Utambulisho wa Tanganyika kishapo serikali ya Tanganyika ili kuwe na uwiano sawa yanapikuja maswala ya muungano na yasiyo ya muungano

Hoja yako ina walakini mkubwa kwakuwa Tanganyika ni ya watu wa imani zote na hata wakati wa chaguzi viongozi huchaguliwa na watu wa imani zote

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe endelea kufunga maneno tu alafu useme uko wazi. Nashukuru kuwa uko wazi katika hoja zako.
 
Yote haya ni nyerere na ccm iliyokuwepo hapaView attachment 2702840
Mwalimu Nyerere aliona mbali.Kule Zanzibar kuna mahotel mengi ya kitalii na watalii ni wengi.Hawa watalii na wananchi wa kawaida wana bidhaa wanataka,kama Michele,viazi,malimao,machungwa,nyanya,vitunguu maji,saumu,karoti,tangawizi ,nafaka,karanga,wajanja wasio wavivu,wanalima,wananunua na kusafirisha Zanzibar.Kwa nini huku bara,tusipanue mashamba yetu,na kulifanyia kazi hili soko.Bado sijagusa mifugo,!ng'ombe,mbuzi,!kuku nk.Kazi kulalamika bila kuangalia fursa.Tunachoweza ni kulalamika,ukilalamika,fursa kwa mjanja.
 
Mimi hoja yangu iko wazi
Utambulisho wa Tanganyika kishapo serikali ya Tanganyika ili kuwe na uwiano sawa yanapikuja maswala ya muungano na yasiyo ya muungano

Hoja yako ina walakini mkubwa kwakuwa Tanganyika ni ya watu wa imani zote na hata wakati wa chaguzi viongozi huchaguliwa na watu wa imani zote

Sent using Jamii Forums mobile app
Amini na kwambia msingi wa hii hoja ni hizi DINI mbili kataa ukubali lakini huo ndo ukweli japo wenzetu wametupiga bao hakuna mkristo atakaye ende zanzibar kutawala lakini wao wana vuka maji wanakuja kututawala .... naamini hata wew kimoyo moyo unakubali
 
Amini na kwambia msingi wa hii hoja ni hizi DINI mbili kataa ukubali lakini huo ndo ukweli japo wenzetu wametupiga bao hakuna mkristo atakaye ende zanzibar kutawala lakini wao wana vuka maji wanakuja kututawala .... naamini hata wew kimoyo moyo unakubali
Lakini kungekuwa na serikali huru ya Tanganyika mambo yangekuwa tofauti sana na sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakuwa ndipo tofauti ama ombwe linapoonekana kwa uwazi zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Muungano hata ilivunjika,huku bara kwa sensa ya 1958 Kuna waislam 66%..Kama mnadhani muungano ukivunjika waislam hawatoshika hatamu mnajidangany,na Tena zenji itakua kituo kikuu Cha pilika za waislam,yaani chaka Tanganyika chaka zenji,wazee wenu walioamua kuibaka zenji siyo wajinga
 
Waliochanganya mchanga na mchanga umeshawafukia
Tukio la kuchanganya udongo wa Muungano na miujiza yake



Uteuzi na kupende-kezwa majina ya vijana 100 kutoka Zanzibar ambao waliungana na wenzao wa Tanganyika ulifanywa na Halmashauri Kuu ya ASP Youth League,
wiki moja kabla ya siku ya Muungano walichezeshwa gwaride la Muungano, nyakati za asubuhi na jioni wakiongozwa na Bi Mwakemwa.

Kazi ya kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar ilianza saa tatu asubuhi na kulikuwa na miujiza mingi.

Zanzibar. Wakati Watanzania wakiadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, siku ulipochanganywa udongo wa pande mbili za Muungano kulikuwa na mazingira ya ajabu na mabadiliko ya vipindi vya hali ya hewa vilivyowababaisha na kuwashangaza watu wengi waliohudhuria sherehe hizo.

Sherehe za kuchanganya udongo wa pande mbili uliowekwa kwenye vibuyu viwili tofauti zilifanyika Aprili 26, 1964 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Mwalimu Nyerere alichanganya udongo kwa kuumimina ndani ya chungu kuashiria Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mmoja kati ya watu waliobeba udongo wa Zanzibar na kuchanganywa na ule wa Tanganyika, Hassan Omar Mzee (66) akihojiwa na Mwananchi nyumbani kwake huko Kibweni nje ya Mji wa Unguja, anaitaja siku hiyo ilikuwa ya aina yake atakayoikumbuka maishani. Wakati wa tukio hilo alikuwa na umri wa miaka 16.

Hassan anasema kazi ya kuchanganya udogo wa Tanganyika na Zanzibar ilianza saa tatu asubuhi na kukiwa na manyunyu ya mvua, jua lisilounguza likiwaka na kupotea na mawingu yaliyokuwa na kivuli cha ubaridi yakiwa yametulizana juu ya anga huku ukimya ukitawala eneo la uwanja.

Anasimulia kuwa lilikuwa tukio la aina yake ambalo liliwashangaza viongozi wengi wa nje na ndani, waliohudhuria na kushuhudia kitendo hicho cha kijasiri na cha kihistoria kilichofanywa na viongozi wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume (wote kwa sasa ni marehemu).

Mshangao huo unatokana na mazimio ya harakati za vikao vingi vya viongozi wa Kiafrika, walikuwa na lengo la kuungana baada ya kujikomboa kutoka kwenye ukoloni, lakini maazimio hayo yaliwashinda viongozi wengi pia Nyerere na Karume walitekeleza kwa vitendo.
Anasema siyo Mwalimu Nyerere wala Mzee Karume walionekana kuwa na hofu ya kupoteza madaraka ya nchi zao, hawakutaka kuendekeza fahari ya vyeo vyao na badala yake walichokitanguliza mbele ni nia na azma ya kujenga umoja wa kitaifa wa watu wao.

Jamhuri ya watu wa Zanzibar na ile ya Tanganyika ndipo zilipokufa. Mabeberu na wakoloni wakipigwa na butwaa kuona kitendo hicho kikitokea na viongozi wa pande mbili wakiwa na nyuso za furaha na bashasha pia wananchi wengine wakionekana kutokwa na machozi ya furaha kutokana na tukio hilo.

Akielezea tukio hilo, Hassan anawataja wenzake wengine watatu walioshiriki katika kazi ya kubeba udongo wa pande mbili za Muungano ni Hassan Kheir Mrema na Sifaheri Kunda kutoka Tanzania Bara na Khadija Abbas kutoka Zanzibar.

Wenzao wanawake walibeba vibuyu vidogo na vikubwa vyenye udongo na wanaume walibeba chungu kimoja kilichochanganyiwa udongo, tukio lilifanyika katikati ya Uwanja wa Taifa ambako jukwaa maalumu lilijengwa.

“Siku hiyo tuliamka mapema tukiwa tumepewa mavazi maalumu, wanaume tulivaa shati na suruali zilizoshonwa kwa vitenge, wenzetu wa kike walivaa mavazi maalumu ya khanga zilizozingatia utamaduni wa Mwafrika,” anaeleza Hassan.

Anasema kabla ya kazi hiyo kufanyika, kulikuwa na mazoezi ya vitendo wiki moja nyuma yake, jinsi ya utaratibu mzima utakavyokuwa hadi kuchanganywa udongo wakiongozwa na Bi Mwakemwa, ndiye aliyekuwa mwenyeji wao tokea walipowasili Dar es Salaam na kupiga kambi Uwanja wa Taifa. Hassan anaeleza ilipofika saa tatu juu ya alama wananchi kutoka Tanganyika na Zanzibar walikusanyika na kukaa kwenye jukwaa la Uwanja wa Taifa kwa utulivu, wakisubiri kuona na kushuhudia tukio la kihistoria likifanyika ili kuziunganisha nchi mbili kuwa Taifa moja.
Anaeleza baada ya kazi hiyo kukamilika, akiwa na wenzake waliondoka hadi kwenye jukwaa kuu wakiwa na vifaa vilivyotumika kubeba udongo na baadaye kwenda kukaa sehemu waliopangiwa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Ikulu ya Dar es Salaam.

Anaeleza walipofika Ikulu kulikuwa na tukio kubwa la kihistoria na ulipandwa mti wa mwembe wa kumbukumbu ya Muungano, uliopandwa na Mwalimu Julius Nyerere akishirikiana Mzee Karume, ukapewa jina la mwembe wa Muungano.

“Mimi nilimkabidhi galoni lililokuwa na maji Mwalimu Nyerere ili kuumwagia mti uliopandwa, Hassan Kheri alimkabidhi Mzee Karume galoni jingine na kuumwagia mwembe huo, hadi leo mwembe huo upo, ni mkubwa kuliko yote ndani ya uzio wa Ikulu,” anasema Hassan akiwa bado anaonyesha kuwa na hamu ya tukio hilo.

Baada ya kumalizika kazi hiyo, sehemu ya udongo uliobakia na vifaa vilivyotumika vilipelekwa kwenye Makumbusho ya Taifa, hadi leo vitu hivyo vinaoonekana na kushuhudiwa na wanaokwenda kuitembelea makumbusho hiyo.

“Udongo wa Zanzibar uliochanganywa na ule wa Tanganyika ulitoka eneo la Kizimbani hapa Unguja, ule wa Tanganyika ulichotwa maeneo ya Dar es Salaam, udongo toka maeneo hayo sasa umeliunganisha taifa zima na mipaka yake, sasa tuna Taifa moja la Tanzania na kiti kimoja Umoja wa Mataifa, ” anasema Hassan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Serikali huru ya Tanganyika (hii iko wapi?)
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda kuna umuhimu mkubwa kuanza kuuhoji muungano huu. Kuna kitu kilikosewa ama kilisahauliwa kwa makusudi na kamwe hakijawahi kuhojiwa popote!

Kwanza lazima tukubaliane hakuna uhuru wa Tanzania bali kuna uhuru wa Tanganyika.. Maana tuliungana tayari Tanganyika ikiwa huru

Baada ya muungano/muunganiko wa mataifa haya mawili nchi huru ya Tanganyika na nchi huru ya Zanzibar kukazaliwa taifa liitwalo TANZANIA.. Kwa maana ya kwamba serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar zilikufa rasmi na kuundwa serikali moja ya Tanzania iko wapi hii?

Hili kosa kubwa na la wazi ndio linatusumbua mpaka leo hii
Baada ya muungano wa haya mataifa mawili, taifa la Zanzibar likabaki na utambulisho wake kama taifa, lakini taifa la Tanganyika likaukana utambulisho wake asilia

Kwa taifa la Zanzibar kubaki na utambulisho wake kama taifa kukawapa nguvu ya kuunda serikali yao inayojulikana kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Kwa kuukana utambulisho wake asilia kama taifa, serikali ya Tanganyika ikakosa nguvu ya kuunda serikali yake ambayo ingeitwa serikali huru ya Tanganyika

Kilichotokea ninini sasa badala ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika kukawa na serikali ya jamhuri ya Tanzania ambayo kwayo ni sehemu ya muungano..
Serikali ndio chombo cha kiutawala kinachoendesha nchi

Zanzibar ana faida mbili tayari ndani ya muungano
1. Utambulisho wake upo
2. Ana serikali yake
Kwa hiyo linapokuja swala la kuamua mambo yake ya ndani kiutawala.. Zanzibar ina chombo chake huru cha kufanya hivyo. Na linapokuja swala la kuamua mambo ya muungano ipo serikali ya Jamhuri ya muungano

Hapo ndipo Tanganyika alipopigwa bao la kisigino kwenye huu muungano.. Ndio maana leo hii watu wa Zanzibar wanaweza kuvuka maji na kuja kuwa viongozi Tanganyika kwa kofia ya muungano lakini mtanganyika kamwe hawezi kuvuka maji na kwenda kuwa kiongozi kule!

Muungano ni mzuri, kuungana kuna faida nyingi, USA ni muungano wa majimbo, UAE ni muungano wamajimbo pia.. Tunaziona faida za kuungana.. Lakini ni lazima uwe ni muunganiko wenye mizania sawa..
Suala la dpw litutoe sasa kwenye hii ganzi tuliyopigwa itutoke tuwe na mwanzo mpya sasa hasa kwenye huu muungano. Tungekuwa na utambulisho wetu wa Tanganyika ina maana tungekuwa na serikali yetu huru na hili suala la bandari lisingeamuliwa na serikali ya Muungano na kutufikisha hapa tulipofikia

Tuurejee mkataba wa muungano upya! Utambulisho wa Tanganyika uwepo ili tupate nguvu ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika... Tukiliacha tena hili...TUTAHUKUMIWA NA WAKATI

Sent using Jamii Forums mobile app
Natamani kukuambia "kunywa Coke baridi nitakuja kulipa". Umeandika "point" tupu.

Andiko hili na limfikie kila anayehusika.
 
Huu muungano uje ufe tu hakuna faida yoyote.

Msukuma hawezi miliki ardhi Znz
Mzanzibar anawez miliki ardhi pale Shinyanga.

Mnaona jinsi gani huu Muungano ni wa kishoga.

Juzi hapo walikataza baadhi ya mazao kupeleka kule vitu vikaoza bandarini.

Mzenji hana SARAFU, hana Bank, hana JESHI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom