Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,678
40,931
Mh. Rais Samia ,

Naamini unafahamu kabisa kuwa, Mwaka 2020 wakati tunampigia kampeni Dr. Magufuli, tulikupigia kampeni na wewe ukiwa mgombea mwenza.

Tuliwaamini nyote wawili kwamba ni watu sahihi kuliongoza Taifa letu.

Sasa wewe ni Rais wetu, hakuna ubishi katika hilo.

Sasa Mh. Rais napata ukakasi kidogo kwa kauli zako , Kila unapotusalimia,

Huyu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unayemtaja ni nani hasa,

Maana ninavyofahamu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayotokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa hakuna mtu, kitu, watu, vitu kwa jina hilo.

Ingawa naelewa kwamba unataka usionekane kuwa unapendelea Dini yeyote,

Lakini Bado Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Haina hadhi ya kutajwa Kwa jina.

Sio sahihi kuipa hadhi hiyo.

Serikali Haina dini, lakini sisi raia tuna dini zetu, na hatumfahamu huyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh. Rais, salami hii, inatufikirisha mno sisi wengi,

Unaweza usiambiwe ILA Kuna haja ya kuachana nayo.

Wasalaaam,

Stroke,

Dar es Salaam.
 
Unajua madhara ya kuambiwa ^Badilisha hiki, badili na kile pia. Ona, badilisha hapa. Badilisha kila kitu kabisa. Hakikisha the so-called legacy inasahaulika,^ ndiyo haya ya kusafiri bila kujua aendako.

Christians and people of faith must know that, kwa kuitikia salamu husika, basi ^mungu^ wao sasa ni JMT. Salamu ni kutakiana ama kukiri heri baada ya kukutana ama kutengana kwa muda. Na heri inatoka kwa Maulana, na wala siyo kwa JMT -- huyu ^mungu^ mpya wa Bi Mkubwa!!!
 
Unajua madhara ya kuambiwa ^Badilisha kila kitu alichofanya; hakikisha the so-called legacy inasahaulika,^ ndiyo haya ya kusafiri bila kujua aendako.

Christians and people of faith must know that, kwa kuitikia salamu husika, basi ^mungu^ wao sasa ni JMT. Salamu ni kutakiana ama kukiri heri baada ya kukutana ama kutengana kwa muda. Na heri inatoka kwa Maulana, na wala siyo kwa JMT -- huyu ^mungu^ mpya wa Bi Mkubwa!!!
jitoe ufahamu leta ujinga ndio utaijua jmt done!
 
Binafsi sioni kama kuna tatzo maana tumezoea kuona kila utawala ukija na SLOGUN yake kama;

A) Ujamaa na Kujitegemea...

B) Ruksa...

C) Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe...

D) Maisha bora kwa kila mtanzania....

E) Hapa kazi tu...

........ na hapo katikati tumekosa kosa MAISHA NA BATA...!!

F) Na sasa tunasalimiana ktk jina la jamuhuri ya muungano
 
Hapajaharibika kitu. Tunampenda Mama na tunaipenda nchi yetu. JINA la nchi yetu ni Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Kwa Kiingereza ni United Republic of Tanzania. Nchi yetu ni muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, lakini JINA lake sio Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwenye JINA Mama hajakosea.

Sasa kwenye salamu je? Ni kukwepa kuleta dini mkutanoni? Sidhani maana baada ya ukaribisho mara nyingi sala na swala zinafuatia. Ni dini hiyo mkutanoni. Hakuna ubaya sana. Naamini Mama anachukia UDINI lakini anapenda DINI. Mavazi yake tu ni kielelezo tosha.

Sidhani kama salamu za kidini kama za mtangulizi wake, za "Tumsifu Yesu Kristu! Bwana asifiwe! Asalaam Aleikhumu!" zina ubaya wowote. Na kwa kweli kuanza kwa salamu hizo ni kuanza kwa sala, na hakutakuwa na sababu tena ya kuwaita mbele viongozi wa dini wasali. Huwa wanasali kwa kutoa hotuba fupi, kitu ambacho si cha lazima.

Nashauri Mama asalimie tu kama alivyokuwa anafanya Rais Magufuli, na baada ya hilo aingie kwenye mada yake. Kama ni shida ya uchache wa matundu ya choo sehemu husika tuzungumzie hilo. Time is money.

Slogan yake inaweza kubakia "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!" Na sisi tunaitikia "Kazi iendelee." Kaipenda hiyo na ni nzuri tu. Hakuna matata hapo.
 
Jambo dogo mnalikuza ilimradi tu kuonyesha udhaifu wa mama... sijui mnapata nini?
Mkuu hii salamu Haina msingi wa kuitegemea.

Huyo Jamhuri hafahamiki ni nani.

Kwanini Rais anahofia kusalimia wananchi Kwa kuzitambua dini zao au tamaduni zao??

Kama anaona soni kusema Asalam Aleykum au Bwana Yesu Asifiwe basi aseme tu Habarini za saa hizi ma bibi na mabwana.

Huyo Jamhuri ndio nani??
 
Umri huo hata HUJUI VIBWAGIZO ?!!!

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio kila kitu....

Inasimamia USALAMA WAKO ,NDUGUZO ,WATOTO WAKO ,WAJUKUU ,VITUKUU.......

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania IMETUPA URAIA NA UTUKUFU juu ya mgongo wa ardhi.....

#KaziIendelee
 
Tunakwepa kutamka “Tumsifu Yesu Kristu “ na “Bwana Yesu asifiwe “.
Akwepe hayo kwa yapi haswa ?!!!

Mh.SSH anaeleweka na kufahamika vyema juu ya MIZANI yake juu ya heshima na utukufu wa makundi mbalimbali.....

JMT asemayo ni KIBWAGIZO chake na kinanoga mno....kikitukumbusha kuwa NCHI KWANZA kabla ya YEYOTE NA CHOCHOTE KISIASA NA KIUTAWALA......

#KaziInaendelea
 
Back
Top Bottom