isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,562
| Jamhuri ya Kuba / Republic of Cuba / República de Cuba
Ni taifa linalopatikana bara la Amerika ya Kaskazini na uwanda wa juu wa Karibi 'Caribbean', katikati baina ya bahari ya Atlantiki, Karibi 'Caribbean' na ghuba ya Mexico
Kuba yenye ukubwa wa eneo zipatazo 110,860 Km[SUP]2 [/SUP]sawa na 42,803 Square Mile's ni nyumbani kwa watu takribani millioni 11,327,179 kufikia May 31, 2020
Bendera ya Jamhuri ya Kuba
Lugha rasmi ni Kihispaniola, pesa kuu ikiwa Peso ya Kuba ' Cuban Peso ' - Peso 1 ni sawa Centavos 100. Kauli kuu ya taifa (Motto) ni "!Patria o Muerte, Venceremos! | "Taifa au Umauti, Tutavuka"
Mji mkuu wa Cuba ni Havana pia ndio mji ulioendelea zaidi, miji mingine yenye maendeleo makubwa ni Holguín, Santa Clara, Guantanamo, Camagüey na Santiago de Cuba
Habana, Havana ©Jeod Neid
Taifa hili la kikomunisti lenye mlengo wa ujamaa, historia ya vita na mapigano, nyumbani kwa Ché Guevara na Fidel Castrol linafahamika vyema kwa oparesheni zake ndani ya mataifa ya Angola, Algeria, Libya, Msumbiji, Ghana, Congo DR "Zaire", Nigeria, Zimbabwe na Sanzibar kwa uchache.
Fidel Ajandro Castro Ruz
Oparesheni ya Angola iliyoacha historia baada ya Kuba kutuma wanajeshi takribani 400,000 kupambana dhidi ya waasi na makaburu katika ukanda wa kusini Afrika hali iliyochochea ukomo wa ubaguzi wa rangi ndani ya Afrika Kusini.
Oparesheni hiyo iliyoanza mwaka 1975 hadi 1991, ilishuhudia mapigano na mbinu za kimedani kutoka kwa wataalamu wa KiKuba waliotembeza kipigo kwa tekniki ya kusogea na miwa iliyowaacha waasi na makuburu midomo wazi hali iliyopelekea kukimbia peku wakipita jangwa la Namib na Kalahari wakipiga kelele za msaada "Tunakufa, Tunakufa!" na kutokomea kusikofahamika.
Kuba yenye ushirika na Urusi, Uchina, Uajemi, Uturuki, Venezuela, Belarus, Vietnam na Bolivia imekuwa tishio kwa misamamo yake dhidi ya mataifa ya magharibi.
| Uchumi, Biashara, Kilimo, Utalii, Maendeleo na Uwekezaji
Kuba inayofahamika na WWF kama taifa linalokuwa kiuchumi kwa kujitegemea kwa asilimia kubwa imekuwa ikijiendesha kutokana na kilimo, biashara na utalii.
Bonde la Vinalles © Jeod Neid
Kilimo ndani ya Kuba ni kipaumbele kwa taifa katika kilimo cha miwa, kahawa, tumbaku, maharage, mchele na viazi. Mwaka 2016 taifa liliweza kuzalisha asilimia 7% ya sukari yote iliyopakana duniani.
Cigar ©Swesta Photographia
Biashara ndani ya Kuba inategemea uuzaji wa tumbaku na sigara aina ya 'Cigar', mchele, madini ya Nickel na Kobati 'Cobalt'.
Baracoa, Santiago de Cuba ©Hoocl Yuj
Utalii unachangia pato la taifa hili kwa asilimia 15%, watalii wengi wanaotembelea Kuba hutokea Kanada, Uholanzi, Ureno, Uhispania, Uswidi, Uswissi, Uchina na Brasil kwa kiwango kiwango kikubwa. Hapo awali Marekani ndio ilikuwa na idadi kubwa ya watalii kabla ya zuio la wamarekani kuzuru Kuba.
Holguín © Vicenza del Rio
Asilimia 85% ya raia wa Kuba wanamiliki majengo/nyumba na hawalipi kodi wala tozo ya aina yoyote huku serikali ikiwa na jukumu la kufanya marekebisho na maboresho kwa asilimia 56%.
Havana © Spencer
| Elimu, Sayansi na Afya
Elimu ndani ya Kuba ni bure! Huku asilimia 99.8% ya waKuba ni wasomi na asilimia 36% ni wataalamu wa Afya na asilimia 26% wakiwa wataalamu wa kilimo.
Famasi ndani ya Jiji la Havana castrol Geo
Vyuo vikuu vyenye hadhi ndani ya Kuba ni Universidad de la Habana, Instituto Superior Politécnico José Antonia Echeverría na University of Santiago de Cuba.
Kuba ndio taifa la kwanza kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Ndio taifa lenye vumbuzi ya chanjo ya saratani inayofahamika kama 'CIMAVAX'. Huku ikiwa kinara katika mapambano dhidi ya EBOLA kwa ukanda wa Afrika Magharibi.
| Michezo, Muziki, Vyombo vya Habari na Sanaa
Michezo pendwa ndani ya Kuba ni baseball, mpira wa miguu, kriketi na mpira wa kikapu huku mchezo wa masumbwi ukihitaji kibali maalumu kutoka serikali kuu kwa shughuli maalumu (Shughuli maalumu ni kuliwakilisha taifa katika mashindano ya kimataifa) nje ya hapo ni marufuku.
Kuba ni nyumbani kwa waandishi nguli Zoé Valdés, Daina Chaviano, Guillermo Rosales na Leonardo Padura.
Serikali ya Kikomunisti ya Kuba ndio yenye kumiliki vyombo vya habari kwa asilimia 98% vyombo vinavyomilikiwa na Serikali ya Chama ni Cubavisión, Tele Rebelde, Canal Educativo na Multivisión.
| Muziki
Muziki wa Salsa, Mambo na Bachata ni asili ya Kuba ukitayarishwa vyema kwa kutumia marimba 'Marímbula'.
Muziki wa kisasa unawakilishwa na Ernesto Lecuona, X-Alfonso, Gloria Estafan, Jacob Forever, El Chacal, Descemer Bueno, Lenier, Diana Fuentes, Camila Cabello, Malú Trevejo na Gente de Zona.
Randy Malcolm (Gente de Zona)
Gente de Zona wanaotamba na nyimbo zenye mahadhi ya reggaeton na salsa ya KiKuba wanafahamika kwa kuachia vibao kama Si No Vuelves, La Gozadera na Muchacha.
Lenier anayetamba na Album Melisma iliyosheheni nyimbo kama Ay Ay Ay, La Buena y El Malo, Déjame na Yo Tengo Una Guitarra Que No Suena.
Camila Cabello aliyetamba na Havana na Hey Ma! | Diana Fuentes aliyezipasua ngoma za masikio kwa nyimbo kama 'Libre' na Te Toque Sin Querer.
Malú Trevejo
Malú Trevejo binti wa asili anayeitikisa dunia na nyimbo 'Nadie Como Yo', 'Luna Llena' na 'Pa La Calle'.
Hii ndio Jamhuri ya Kuba 🇨🇺