DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), James Mbowe baada ya kutangaza kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) amesema atachukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.
James amejiunga na chama hicho leo, Jumatano Makao Makuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma Biafra jijini Dar es Salaam, huku akieleza amejiunga na jukwaa hilo ili kwenda kuwawakilisha wananchi wa Hai.
Katika tukio la kujiunga kwake aliambatana na kada mwingine wa Chadema, Yericko Nyerere wote wamekahidhiwa kadi ya chama hicho kipya wamejinasibu kuwatumikia wananchi kwa uadilifu kwa kuzingatia kasi na nguvu ileile waliyoitumia walikotoka.