GE2025 James Mbowe aahidi Vijana Jimbo la Hai kufundishwa Kiingereza wakafanye kazi Mlima Kilimanjaro

GE2025 James Mbowe aahidi Vijana Jimbo la Hai kufundishwa Kiingereza wakafanye kazi Mlima Kilimanjaro

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Zingatia hizo sera za Mgombea Ubunge kutoka Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kisha zingatia Mavazi aliyovaa ni ya Makamanda wa CHADEMA

Jamaa kahama chama lakini bado itakadi za CHADEMA anatembea nazo hadi kwenye kampeni za CHAUMMA hii ni dharau tosha kwa CHAUMMA

Baasi tuendelee kuzingatia vijana kujua kingereza

-----------------------

Mgombea ubunge jimbo la Hai kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), James Mbowe ameahidi vijana wa jimbo la Hai kwenda kufanya kazi katika Mlima Kilimanjaro kwa asilimia 100.

Amesema kinachotakiwa kufanya Mlima Kilimanjaro si shahada wala elimu kubwa bali kupanda mlima sambamba na kufahamu lugha ya Kiingereza.

Kutokana na hilo amesema akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha vijana 50 katika kata zote za Hai wanafundishwa lugha ya Kiingereza wakafanye kazi kwenye mlima huo.

Ameyasema hayo mbele ya mgombea mwenza wa urais wa Chaumma, Devota Minja leo Jumatatu Septemba 22, 2025 alipokuwa Kata ya Masama Mashariki katika soko la Mula Jimbo la Hai.

"Tumepewa Mlima Kilimanjaro lazima kazi tuzifanye tunufaike nao mlima huu tuliopewa na Mungu," amesema James.

Akieleza zaidi James ameahidi kufuata nyayo za baba yake akitumia msemo wa mtoto wa nyoka ni nyoka hivyo atafanya maendeleo kama Freeman Mbowe.

Kwa upande wake Minja amesema watu wa Hai wampe James Mbowe afuate nyayo za baba yake za kuendeleza jimbo hilo, huku akisema aliyoyafanya Mbowe anastahili kujengewa sanamu.


 
Vipi ameshinda au maana INEC hawataki kuweka matokeo ya ubunge.
 
Back
Top Bottom