James Mbatia: Yanayoendelea Tanzania yanatia wasiwasi mkubwa

Hana jipya huyo.
Kwa vyovyote atakuja kuunga mkono CCM na serikali yake kwa kibwagizo cha mama Tanzania.

Anasubiri kupewa ubunge wa viti maalum vya urais. Anapenda umama sana.
 
Huyu mama Tanzania kafia wapi??
 
Mama Tanzania usiwe na wasi wasi. Ccm wanakumbuka sana walipokupa jukwaa kuwananga chadema kule Mbeya chini ya ulinzi wa RC. Pia nakumbuka ahadi yako ya kuwa NCCR itakuwa chama kikuu cha Upinzani nchini.

Nyie mlienda kwenye uchaguzi kwa nia ya kushindwa ili muwe chama kikuu cha upinzani. Wenzenu walienda ili washike dola. Kwa hiyo matokeo mliyopata siyo mabaya kwa kuzingatia dhamira yenu toka mwanzo.

Pia usijali sana. Soon mwenyekiti wa ccm ambacho ni chama rafiki wa NCCR atakuteua kuwa mbunge hivyo utaendelea kuzuga zuga bungeni kwa miaka 5 kabla nccr kufa rasmi kibudu 2025 ambapo itaingia kwenye kundi la UPDP na TADE aka vyama visivyo na effects wala mvuto nchini.

Mwisho nikupe pole san Ndg Mbatia kwa yote mliyopitia. Najua mlijiandalia haya majanga kwa hiyo endeleeni kufarijiana huku mkitafakari Zaburi 22: 6-7

Cc John Paul Shibuda
 

Huyo Mbatia ni msaliti wa mageuzi, hivi ni kweli alikuwa hajui kuwa jiwe ni muongo na tapeli wa kutupwa? Alipodanganywa na kuambiwa kiwa atakuwa KUB hakujua kuwa ni hadaa? Saa hii anamlilia nani wakati aliamua kumtumikia shetani? Kila siku yeye na Lipumba walikuwa wanasema rais ameahidi kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki, tukawaambia Magu sio mkweli bali wanawatumia tu. Mgombea wake wa urais kashakubali kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki, yeye anamlilia nani?
 
Mama Tanzania pole Sana, watakukumbuka Tu wanajua wewe na Mrema tatizo lenu ni uhakika WA Kula Tu.
 
Alipoitwa Ikulu na rais na kusifiwa sifiwa alijihisi yeye ndio ashaula sasa anakuja na porojo za mama Tanzania, akapige magoti sasa ateuliwe ubunge halafu akawe mzee wa ndiyooo kwenye bunge bubu hili la chukua chako mapemba.
 
Mwanaume kama mwanamke.
Analia lia nini sasa mama afrika!
Haya ni matokeo ya usaliti wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…