James Mbatia: Yanayoendelea Tanzania yanatia wasiwasi mkubwa

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,354
2,000
Hana jipya huyo.
Kwa vyovyote atakuja kuunga mkono CCM na serikali yake kwa kibwagizo cha mama Tanzania.

Anasubiri kupewa ubunge wa viti maalum vya urais. Anapenda umama sana.
 
yomboo

JF-Expert Member
May 9, 2015
6,235
2,000
TAARIFA KWA UMMA​

Leo tarehe 12.11.2020 siku ya Alhamisi Majira ya saa 6 za Mchana katika ofisini za Makao makuu ya NCCR- Mageuzi M/Kiti wa chama Ndugu James Francis Mbatia atazungumza na Watanzania kupitia Vyombo vya Habari.

Imetolewa na:
Edward Simbeye
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma.
Huyu mama Tanzania kafia wapi??
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
10,463
2,000
Mama Tanzania usiwe na wasi wasi. Ccm wanakumbuka sana walipokupa jukwaa kuwananga chadema kule Mbeya chini ya ulinzi wa RC. Pia nakumbuka ahadi yako ya kuwa NCCR itakuwa chama kikuu cha Upinzani nchini.

Nyie mlienda kwenye uchaguzi kwa nia ya kushindwa ili muwe chama kikuu cha upinzani. Wenzenu walienda ili washike dola. Kwa hiyo matokeo mliyopata siyo mabaya kwa kuzingatia dhamira yenu toka mwanzo.

Pia usijali sana. Soon mwenyekiti wa ccm ambacho ni chama rafiki wa NCCR atakuteua kuwa mbunge hivyo utaendelea kuzuga zuga bungeni kwa miaka 5 kabla nccr kufa rasmi kibudu 2025 ambapo itaingia kwenye kundi la UPDP na TADE aka vyama visivyo na effects wala mvuto nchini.

Mwisho nikupe pole san Ndg Mbatia kwa yote mliyopitia. Najua mlijiandalia haya majanga kwa hiyo endeleeni kufarijiana huku mkitafakari Zaburi 22: 6-7

Cc John Paul Shibuda
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,507
2,000
TAARIFA KWA UMMA​

Leo tarehe 12.11.2020 siku ya Alhamisi Majira ya saa 6 za Mchana katika ofisini za Makao makuu ya NCCR- Mageuzi M/Kiti wa chama Ndugu James Francis Mbatia atazungumza na Watanzania kupitia Vyombo vya Habari.

Imetolewa na:
Edward Simbeye
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma.

========
James Mbatia:

Maneno hayatoshelezi hisia kutokana na yale tuliyonayo mioyoni mwetu kufuatia yaliyotusibu katika mchakato wa uchaguzi.

Tanzania tuliyoipenda sana si Tanzania tunayoiona sasa.

Hisia zetu kwa ujumla kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu haziwezi kuwasilishwa kwa maneno, lakini wote wenye nia nzuri na Mama Tanzania, kupitia nafsi zao, wanaweza kuelewa hisia za wengi kwa muda huu.

Hisia hasi zinanazokinzana na utu wetu, zinazokinzana na maadili yetu ya Kitanzania; zinazokinzana na tunu zilizopo kwenye wimbo wetu wa taifa – yaani Hekima, Umoja na Amani. Hisia hizi zinachoma kichaka kilichotuhifadhi sisi sote, yaani Mama Tanzania.

Licha ya kwamba kwa miaka takribani 59 sasa tangu tupate Uhuru, hatujaweza kumtumia vizuri Mama Tanzania ili tuweze kujipatia mahitaji ya msingi kwa wote na kuwa na furaha ya ndani, furaha ya kweli. Sasa tupo katika njia ya kumuangamiza.

Kuna waliopoteza Maisha, kuna waliochomwa moto, kuna waliomwaga damu, kuna waliokatwa viungo vyao vya mwili, kuna waliobakwa, kuna waliopigwa risasi na walioteswa kwa njia mbalimbali. Haya bado yanaendelea katika mazingira ambayo yanatia wasiwasi mkubwa sana.

Sisi NCCR Mageuzi, kwa zaidi ya miaka 28 sasa tumekuwa tukiimba wimbo wa Katiba mpya, yenye kubeba Tume Huru ya Uchaguzi. Kwaasasa tumetathmini gharama zimekuwa kubwa mno kwa miaka yote 28, gharama za kupoteza baadhi ya uhai kwa wenzetu ndani ya chama kwasababu ya kupigania haki-msingi.

Gharama zimekuwa kubwa kwa kupoteza utu kwa kuteswa kwa njia mbalimbali. Nakumbuka tangu miaka ya 1990’s yalikuwa yanatokea, ya umwagaji wa damu. Kila baada ya uchaguzi, damu! Ni chaguzi chache sana ambazo zimepita bila kumwagika damu – mwaka huu unasikitisha sana.

Maneno yetu yanasikika duniani kote kwani dunia imeshuhudia vitendo vinavyokiuka makubaliano yetu ya kitaifa kwa zaidi ya miaka 28, ambayo tulikubaliana kuwa maendeleo endelevu yatatokana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Huyo Mbatia ni msaliti wa mageuzi, hivi ni kweli alikuwa hajui kuwa jiwe ni muongo na tapeli wa kutupwa? Alipodanganywa na kuambiwa kiwa atakuwa KUB hakujua kuwa ni hadaa? Saa hii anamlilia nani wakati aliamua kumtumikia shetani? Kila siku yeye na Lipumba walikuwa wanasema rais ameahidi kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki, tukawaambia Magu sio mkweli bali wanawatumia tu. Mgombea wake wa urais kashakubali kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki, yeye anamlilia nani?
 
mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
3,790
2,000
Mama Tanzania pole Sana, watakukumbuka Tu wanajua wewe na Mrema tatizo lenu ni uhakika WA Kula Tu.
 
mr.London

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
3,120
2,000
TAARIFA KWA UMMA​

Leo tarehe 12.11.2020 siku ya Alhamisi Majira ya saa 6 za Mchana katika ofisini za Makao makuu ya NCCR- Mageuzi M/Kiti wa chama Ndugu James Francis Mbatia atazungumza na Watanzania kupitia Vyombo vya Habari.

Imetolewa na:
Edward Simbeye
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma.

========

Muhtasari wa aliyozungumza Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia:

Maneno hayatoshelezi hisia kutokana na yale tuliyonayo mioyoni mwetu kufuatia yaliyotusibu katika mchakato wa uchaguzi.

Tanzania tuliyoipenda sana si Tanzania tunayoiona sasa.

Hisia zetu kwa ujumla kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu haziwezi kuwasilishwa kwa maneno, lakini wote wenye nia nzuri na Mama Tanzania, kupitia nafsi zao, wanaweza kuelewa hisia za wengi kwa muda huu.

Hisia hasi zinanazokinzana na utu wetu, zinazokinzana na maadili yetu ya Kitanzania; zinazokinzana na tunu zilizopo kwenye wimbo wetu wa taifa – yaani Hekima, Umoja na Amani. Hisia hizi zinachoma kichaka kilichotuhifadhi sisi sote, yaani Mama Tanzania.

Licha ya kwamba kwa miaka takribani 59 sasa tangu tupate Uhuru, hatujaweza kumtumia vizuri Mama Tanzania ili tuweze kujipatia mahitaji ya msingi kwa wote na kuwa na furaha ya ndani, furaha ya kweli. Sasa tupo katika njia ya kumuangamiza.

Kuna waliopoteza Maisha, kuna waliochomwa moto, kuna waliomwaga damu, kuna waliokatwa viungo vyao vya mwili, kuna waliobakwa, kuna waliopigwa risasi na walioteswa kwa njia mbalimbali. Haya bado yanaendelea katika mazingira ambayo yanatia wasiwasi mkubwa sana.

Sisi NCCR Mageuzi, kwa zaidi ya miaka 28 sasa tumekuwa tukiimba wimbo wa Katiba mpya, yenye kubeba Tume Huru ya Uchaguzi. Kwaasasa tumetathmini gharama zimekuwa kubwa mno kwa miaka yote 28, gharama za kupoteza baadhi ya uhai kwa wenzetu ndani ya chama kwasababu ya kupigania haki-msingi.

Gharama zimekuwa kubwa kwa kupoteza utu kwa kuteswa kwa njia mbalimbali. Nakumbuka tangu miaka ya 1990’s yalikuwa yanatokea, ya umwagaji wa damu. Kila baada ya uchaguzi, damu! Ni chaguzi chache sana ambazo zimepita bila kumwagika damu – mwaka huu unasikitisha sana.

Maneno yetu yanasikika duniani kote kwani dunia imeshuhudia vitendo vinavyokiuka makubaliano yetu ya kitaifa kwa zaidi ya miaka 28, ambayo tulikubaliana kuwa maendeleo endelevu yatatokana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Kama taifa, tumekiuka hata makubaliano ambayo dunia ya leo (ya teknolojia na mitandao ya kijamii) tulikosa fursa ya kuitumia. Mitandao ya kijamii ilifungwa. Huo ni ukiukwaji wa juu sana wa haki-msingi za binadamu.

Sisis tumejisikiliza na tukajitafakari sana. Tumekuwa tukiimba Utu – itikadi yetu. Kweli utu ni itikadi yet una misingi yake yote ya Usawa, Maadili, Udugu, Imani, Uzalendo, Kazi, Endelezo – ya kuifanya Tanzania kuwa sehemu salama zaidi ya kuishi.

Itikadi yetu ni kati ya itikadi bora zaidi duniani na tumekuwa tukiitetea huko duniani.

Tanzania tunaihitaji Dunia kuliko Dunia inavyoihitaji Tanzania, hasa katika mabadiliko haya ya kasi ya sayansi na teknolojia.

Itikadi yetu inazungumzia Udugu. Na Mwl. Nyerere aliasisi Taifa hilimkwa kusema kuwa binadamu wote ni ndugu zangu. Sasa huwezi kufanyia ndugu yako haya ambayo yanaendelea katika nchi yetu sasa.

Tumemsikiliza Mwl. Nyerere alisema nini kabla hajaondoka duniani. Naomba nimnukuu:

“Naondoka nikiwa nimewaachia Taifa moja lenye Umoja na Amani. Ipendeni Tanzania kama mnavyowapenda mama zenu. Jueni hamna nchi nyingine zaidi ya Tanzania”

Leo Mwalimu angekuwa hai, hisia zetu zinatutuma kuwa angesema: “Hapana, hii siyo Tanzania niliyowaachia. Hii siyo Demokrasia. Jikusanyeni muanze upya.”

Hili siyo shauri la wanasiasa pekee. Ni la Watanzania wote. Hatuwezi kuangalia tu wakati mama anaamka na huzuni na analala kwa hasira.

Sisi NCCR Mageuzi tumetafakari na kukubaliana na msemounaosema: Utajiri upo kwenye ulicho nacho.
Alipoitwa Ikulu na rais na kusifiwa sifiwa alijihisi yeye ndio ashaula sasa anakuja na porojo za mama Tanzania, akapige magoti sasa ateuliwe ubunge halafu akawe mzee wa ndiyooo kwenye bunge bubu hili la chukua chako mapemba.
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
6,956
2,000
Mwanaume kama mwanamke.
Analia lia nini sasa mama afrika!
Haya ni matokeo ya usaliti wake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom