James Mbatia: Vyama vya siasa ndio vimeharibu kwa kuingilia uchaguzi wa Serikali za Mitaa

lukindo,

Sio kwa vile huo ni wa Uganda ndio lazima uwe bora dhidi ya wa kwetu. Ninaamin yetu ni bora zaidi ukiondoa huu unazi wa kivyama uliopitiliza.
Usibeze kila kitu
 
lukindo,
Tunaanzia kitongoji then kijiji kwa halmashauri za wilaya, majiji, Manispaa na miji tunaanzia mtaa, then Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa n.k. Tuko vizuri na wengine wanakuja kujifunza kwetu.
 
Msingi wa chama chochote kushinda uchaguzi mkuu huanzia kwenye kujiimarisha kwenye chaguzi ndogo (Mitaa) ili kujijenga kimkakati. Uwepo wa chaguzi za mtaa unatoa taswira ya haswa chama gani kinamtazamio mkubwa wa kuweza kushinda chaguzi za ngazi ya juu (ceteris peribus). Kuondoa kabisa chaguzi na kutegemea zisimamiwe na wananchi wenyewe huku serikali ikiwa ni ya chama inaamaana unakipa chama nguvu ya kujitengenezea misingi mizuri inayoweza kuwafanya washinde hata chaguzi za juu. Ushindani ni lazima uwepo pale pale kuanzia huko, watu washindane kwa misingi ya kiitikadi, mshindi atengeneze wafuasi wengi watakaowezesha chama hicho kukubalika kwenye ngazi nyingine.
 
Tatizo la huu uchaguzi ni pale pale Magufuli mwenyewe na genge lake wanapolazimisha ionekane yeye na ccm wanakubalika kwa uchapakazi kazi. Basi kupitia madaraka yake analazimisha ccm ipite kwa namna yoyote, lengo ni yeye kujiwekea mazingira ya kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Ndio hapo tunapoona sheria na kanuni zikivunjwa wazi wazi kwani hakuna wa kuwajibishwa maana ni maagizo yake.
 
Sio kwa vile huo ni wa Uganda ndio lazima uwe bora dhidi ya wa kwetu. Ninaamin yetu ni bora zaidi ukiondoa huu unazi wa kivyama uliopitiliza.
Usibeze kila kitu
Sio kubeza bali tuna share experience na wengine. Uganda inaweza kutupa experience ya uongozi zaidi ya sisi tunavyoweza kuwapa maana hata viongozi wetu wakuu wengi waliosomea huko walikuwa na ushawishi hwalivyorejea.
 
lukindo,
Ubinafsi wa mali na madaraka ndio unaolitafuna hili taiga.
Umoja na mshikamano inatoweka kwa kasi ya 5G.
Jitahada za byama vya siasa kijiimarisha, na chama chenye nguvu kuamua linavyoona inafaa kwa maslahi yake, si taifa kimepelekea mauaji, familia 'kutengana', kususiana misiba, ....
Ikiwa kama namna ya kuwapata viongozi wa Mitaa/Vijiji haitobadilika; usalama wa jamii upo mashakani.
Katika familia, mambo yanapoharibika baba hawezi kukosa kujibia na 'kuhujumiwa'. Kwa hali taifa lilipofika, CCM isikwepe kulaumiwa.
Niwaombe wazee wetu (Mwinyi, Mkapa, Kikwete .......) waone namna bora ya 'kuwakalisha' vijana wao ili kupata namna bora ya kufanya chaguzi, kuheshimu maamuzi ya watu, hasa hao wanaitwa 'maskini' wanapowachagua maskini wenzao.
 
Sio kwa vile huo ni wa Uganda ndio lazima uwe bora dhidi ya wa kwetu. Ninaamin yetu ni bora zaidi ukiondoa huu unazi wa kivyama uliopitiliza.
Usibeze kila kitu
Utumiage akil kidogo na wewe. Huu mfumo wetu ndio kila mwaka tunavutana na kutoa damu. Saiz jafo ndio ameheuka kuwa mfumo sasa unasemaje ni bora kuliko huo ambao jamaa ameelza na kuonesha kama unamapungufu basi ni nafuu. Sikia sio kutetea kila ujinga wa tanzania ndip uzalendo sawa.
 
Duh! Kwa visa kashaa ulivyo viorodhesha hapa naona kuna weza kuwa Giza Nene mbeleni ,,,Serikali ione kuwa huu ni mda muafaka wa kutengeneza!!
 
Hili nakubaliana nalo kwa sehemu kubwa , yaani kungetafutwa utaratibu viongozi wa serikali za mitaa na vijiji wasidhaminiwe na chama chochote bali wana jamii wawapate viongozi wao kwa namna nzuri uliowekwa na jamii husika. Mfano Kijiji kipendekeze majina ya watu sita kwa mfano wazee wawili, vijana wawili na wamama wawili. Hawa wanapigiwa kura na anayepata kura nyingi anakuwa ndiye mwenyekiti wa kijiji, mwanamke (Mama )anayefuata kwa kura anakuwa makamu mwenyekiti.

Mapungufu ya mfumo huu wa sasa ni kumomonyoa misingi ya amani na utulivu katika jamii. Uchaguzi wa vyama vijijini na mitaani umeleta ufa kubwa sana miongoni mwa wanajamii. Mfano kijijini kwetu kuna ukoo uligawanyika vibaya sana kwani mgombea wa CDM na CCM walitokea kwenye ukoo huo , matokeo yake wakagawa ukoo kabisa (uchaguzi wa mwaka 2014) . Katika uchaguzi huo huo baadhi ya waumini wa kanisa la RC ya pale kigangoni kwetu walisusa kanisa baada ya katekista kuwa ndiye mpiga debe wa CCM hatimaye waliojiengua wakaanzisha kanisa lao.

Uchaguzi huu ndiyo umekuwa balaa zito , naambiwa mtendaji anaishi kama digi digi kwa kujificha baada ya kumuengue mgombea ambaye vijana waliapa kumpa uenyekiti, Sasa maisha haya hayafai kijijini yaani huko kwetu mtu anaibiwa mifugo watu wakijua ni wa ccm au wa chadema wengine hawatokei kusaidia kisa eti huyo si wa chama chao. Hali itakuwa tete sana kwa siku zijazo
True ila awamu ndo imeleta hizo chuki awamu zilizopo ayakuwepo hayo.Hao watendaji ndo chanzo cha mpasuko na uvunjifu wa amani mfano yule wa kinondoni angetimiza wajibu wake akwilina asingeuwa na polisi hivo ni sahihi kwa mahakama ya jamii kuwatenga kuwasusia kwenye shuguli za jamii kuanzia kuuza na kununua misiba sherehe nk kuwabagua na kuwanyooshea vidole ili wavune walichopanda hii takuwa funzo za kuambiwa changanya na .....
 
Sitaki kuamini kama mama tz kafilisika hivyo
Nimemsikiliza Mbatia kwa makini. Japo kaongea upotofu ule ule wa wenzake waliosusa kuna jambo moja limegusa akili yangu. Ingefaa asikilizwe.

Mbatia anasema hivi: vyama vya siasa ndio vimeharibu kwa kuingilia uchaguzi wa local government! Anasema huu uchaguzi ungepaswa kuachiwa jamii kama ilivyokuwa zamani. Jamii ndio inawajua watu wanaofaa mtaani na kitongojini. Tume ya uchaguzi ingeendesha uchaguzi bila kushirikisha vyama vya siasa.

Tungeepuka mivutano ya kisiasa isiyo na mantiki.Tungewaepusha wanajamii kupoteza nguvu kwenye siasa badala ya kuzitumia kwenye Maendeleo. Tusipandikize mihemko ya vyama vijijini, vitongojini na kwenye mitaa. Tuache vyama vilumbane bungeni.

Mbatia anadai vyama vya siasa vishiriki uchaguzi mkuu tu.

Mimi nakubaliana na hoja hii. Wewe je?
 
Kwa akili zako unafikri anaposema vyama vya siasa ndivyo vinavyoharibu kwa kuingilia uchaguzi unafikri anamaanisha vyama gani zaidi ya CCM?ambayo imetufikisha mahali tulipo mpaka sasa,na hata kama itaachiwa tume bila wananchi kuthaminiwa katika matakwa yao mambo yataendelea kuwa vilele kwa sababu tume ya uchaguzi ndio watendaji wenyewe,waliokua wanafunga ofisi wapinzani wanapotaka kwenda kuchukua form.

Ni makosa makubwa Sana kwa tume kuwachagulia watu viongozi badala ya watu kuwachagua wawatakao
 
Msingi wa chama chochote kushinda uchaguzi mkuu huanzia kwenye kujiimarisha kwenye chaguzi ndogo (Mitaa) ili kujijenga kimkakati. Uwepo wa chaguzi za mtaa unatoa taswira ya haswa chama gani kinamtazamio mkubwa wa kuweza kushinda chaguzi za ngazi ya juu (ceteris peribus). Kuondoa kabisa chaguzi na kutegemea zisimamiwe na wananchi wenyewe huku serikali ikiwa ni ya chama inaamaana unakipa chama nguvu ya kujitengenezea misingi mizuri inayoweza kuwafanya washinde hata chaguzi za juu. Ushindani ni lazima uwepo pale pale kuanzia huko, watu washindane kwa misingi ya kiitikadi, mshindi atengeneze wafuasi wengi watakaowezesha chama hicho kukubalika kwenye ngazi nyingine.
Hivi unajua serikali iligeuzwa tawi la CCM awamu ya Mwinyi?
Kwa nionavyo mimi pamoja na kuwa vyama mbadala havijasema hadhalani; ni wazi wanapigania kuitenganisha CCM dola na Serikali.
Changamoto ni pale watumishi wa serikali hawajitambui kuwa hawana sababu ya kujitanabahisha na CCM.
Fikiria hakuna DC, RC Mkurugenzi asiyetokana na CCM.
Nashauri tuwaunge mkono hawa wanaopambana na dola chama.
 
Kifikra upo sahihi sana, lakini kimtazamo wa uhalisia Serikali inayowekwa na chama ndo yenye dola, na watumishi wake kutokana na kuangalia maslahi inawalazimu kuvaa ukijana ili wale green pasture vizuri, ni ngumu kuliepuka hilo kwenye zama hizi za viongozi wa maslahi binafsi.
 
Kwa akili zako unafikri anaposema vyama vya siasa ndivyo vinavyoharibu kwa kuingilia uchaguzi unafikri anamaanisha vyama gani zaidi ya CCM?ambayo imetufikisha mahali tulipo mpaka sasa,na hata kama itaachiwa tume bila wananchi kuthaminiwa katika matakwa yao mambo yataendelea kuwa vilele kwa sababu tume ya uchaguzi ndio watendaji wenyewe,waliokua wanafunga ofisi wapinzani wanapotaka kwenda kuchukua form.
Nadhani hujaelewa wanachozungumzia hapa. Ni hivi: Uchaguzi wa serikali za mitaa usiwe unahusisha vyama. Uwe ni uchaguzi wa kuchagua viongozi bila kushirikisha vyama. Sasa unaposema anamaanisha CCM una maana ndicho chama cha siasa pekee kilichopo, kumbe viko vingi.
 
Mseven siyo dictator ila ukitaka kumtambua vizuri tangaza nia ya kugombea uraisi alllooooo utaisoma namba na ndo utamjua kuwa mseven ni nan
Hoja nzuri na cha msingi sio kwamba uchaguzi ni mbaya bali ile akili inayotumika ndio mbaya hiyo kupelekea matokeo mabaya kama tunayoyaona. Ukikubali kutumia akili vizuri daima haiwezi kutoa matokeo mabaya.

Mfano fikiria mtu kama M7 na 'udikteta' wake lakini amebuni mfumo bora wa kuwapata viongozi (local council). Hii taasisi wenyewe wamaiweka kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya (LCV) na zina wajumbe tisa ambao wanapatikana kwa uchaguzi wa pamoja kuanzia anayepata kura nyingi hadi yule wa tisa. Wakishachaguliwa (regardles vyama wanavyotokea) wale tisa wanakutana na kuchaguana maofisa (i.e. mwenyekiti, mweka hazina na katibu wao nk). Na wanaochaguliwa wenyeviti ndio wanawakilisha vijiji ngazi za kata hivyo hivyo hadi ngazi za wilaya.

Haya yote yanafanyika kwa kiwango kidogo cha uchakachuaji na ndio maaana migogoro mingi inaishia chini. Issue za kuiba kura zinakuwa zaidi kwenye ngazi za urais labda lakini wati wa chini (localities) wanakuwa wamesharidhika kwa maana wanatawaliwa na watu wanaowataka.

Tatizo sisi tiligeuza kila kitu siasa na kibaya zaidi siasa zetu hazina afya kwa maana tumeona pamoja na chaguzi zilizopita tukadhani tumejifunza kitu lakini ushahidi katika huu uchaguzi wa vijiji unaonyesha ujinga katika ngazi za maamuzi unaongezeka.

isome hapa:

=====
Local government structures in Uganda
The village

A village is the lowest political administrative unit. A village usually consists of between 50 and 70 households and may be home to anywhere between 250 and 1,000 people. Each village will be run by a local council – local council I (LCI) - and is governed by a chairman (LCI chairman) and nine other executive committee members. There are 66 villages in Katine sub-county.

The parish
The parish is the next level up from the village. A parish is made up of a number of villages. For example, in Katine parish – one of the six parishes in the Katine project area – there are seven villages, with a population of about 3,800. Each parish has a local council II (LCII) committee, made up of all the chairman from the village LCIs in the parish. Each LCII will elect, from among themselves, an executive committee. Today, LCIIs are largely involved in settling land distributes and mobilising the community for various activities. The parish is largely run by a parish chief – a government employee who provides technical leadership to the LCII. There are six parishes in Katine sub-county - Katine, Ochuloi, Ojom, Ojama, Olwelai and Merok.

The sub-county
After the parish comes the sub-county. A sub-county is made up of a number of parishes – in Katine, the number is six. The sub-county is run by the sub-county chief on the technical side and by an elected local council III (LCIII) chairman and his/her executive committee. The sub-county also has an LCIII council, a kind of parliament at that level, complete with a speaker and deputy speaker. The council consists of elected councillors representing the parishes, other government officials involved in health, development and education, and NGO officials in the sub-county. In towns, a sub-county is called a division.

The county
A county is made up of several sub-counties. Katine sub-county is one of seven that make up Soroti county. Each county is represented in the national parliament in Kampala by an elected member (an MP). In major towns, the equivalent of a county is a municipality (which is a set of divisions). LCIII executive committee members of all the sub-counties constitute the local council IV (LCIV). They then elect an LCIV executive committee from among themselves. These committees have limited powers, except in municipalities, which they run.

The district
A district is made up of several counties and any municipalities in that area. Soroti district, with a population of about 500,000, consists of three counties and one municipality – called Soroti. A district is led by an elected local council V (LCV) chairman and his executive. In Soroti, the chairman is Stephen Ochola. There is also an elected LCV council, with representatives from the sub-counties and technical staff in the district. The council debates budgets, decisions and bylaws. On the technical side, the district is led by a chief administrative officer, appointed by central government. The district also has heads of various departments such as education, health, environment and planning, which are responsible for relevant matters in the whole of the district. So, the district education officer of Soroti is responsible for education matters in the whole of Soroti, which includes Katine.

At present, Uganda has 80 districts, but the number keeps growing. When President Museveni captured power 23 years ago, after a five-year guerrilla war, Uganda had around 30 districts. The government says it creates districts to take services nearer to the people, but critics argue that the only thing more districts bring is poverty.
=====
 
Nakubaliana na wewe. Katika ngazi ya mtaa wakazi wanamjua nani afaa kuwa kiongozi wao na sio chama kipi kinafaa. Ni vema hata balozi asifungamane na chama. Watu waachwe wamchague wampendae kama ilivo vikao vingine vya kijamii kama ukoo, harusi nk.

Back
Top Bottom