Mkuu sitakuamini hata kidogo katika hili la vivutio vya kitalii hata kidogo...
Nchii hii ina circuits tatu kama si nne kuu muhimu za kitalii, na hapa namaanisha pande nne zote za Tanzania....
Nchi kama Uswisi uliyoitaja kwanza kwa eneo la mraba ni ndogo mno wakati yenyewe ina eneo la kilomita za mraba 41,285 ...sisi Tanzania tuna kilomita za mraba 947,300 (sasa fikiria inaingia kwetu mara ngapi hapo).
Ukiacha hilo, ukiichukua Mbuga ya Wanyama ya Serengeti (14,763 kilometa za mraba) na ukaenda kuipachika katika nchi ya Uswisi, mbuga hii itajaza theluthi ya nchi ya Uswisi.
Hapo bado sijakutajia Hifadhi ya Wanyama ya Selous yenye eneo la kilometa za mraba 44,800. Yaani kwa kifupi nchi yote ya Uswisi ni ndogo kulinganisha na hifadhi ya Selous.
Hapo sijataja maeneo mengine yaliyobakia...Upo?????
Huyu Mwenzetu haeleweki.
Hata ukimpa takwimu hataelewa kwa sababu yeye hoja yake si alichoongea Mbatia bali ni Mbatia mwenyewe.
Nafikiri si lazima kila mara mtu afikirie kuleta Maada badala yake ni vizuri wakati mwingine kukaa kimya na kuangalia/kujifunza aina za maada ambazo utapata waungaji mkono wengi.