James Mbatia, kama Mulugo

James Mbatia, kama Mulugo

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,229
Reaction score
17,659
Wakuu, Politicians ni watu wa maneno mengi.
Kwa waliomsikiliza Mbatia kwenye kipindi cha Dakika 45, jana atanielewa zaidi.

Mbatia aliongea uongo aliposema
Uingereza ilihama kutoka kwenye Ukabaila kwenda kwenye Ubepari (Feudalism to Capitalism) mwaka 1948...!!

What is this? Anatofauti gani na Mulugo aliyesema Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili Visiwa vya Zimbabwe na Pemba?

Wanasiasa lazma wawe makini hasa wanapo Ongea kwenye Vyombo vya habari ambapo Watu wanafuatilia,
 
Kwanza alianza kusema Tanzania ni nchi ya pili Duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya Utalii kitu ambacho si cha kweli..
Kwa Africa tu, Tanzania inashika nafasi ya Kumi kutembelewa na watalii kwa takwimu za 2013 kutoka (UNWTO) United Nations World Tourism Organization..

Yeye anaongelea vivutio wewe unaongelea kutembelewa.

Hebu weka sawa hapo.

Hata hivyo, ukishakuwa UKAWA akili zako haziwezi kuwa sawa. Kutaka kuhatarisha amani ya nchi iliyopiganiwa kwa miaka mingi ni laana kubwa.
 
mimi huwa nawashangaa sana wanamsifia mbatia wakati jamaa fulani zembe tu hajui hata anachofanya kabisa.
 
Wakuu, Politicians ni watu wa maneno mengi.
Kwa waliomsikiliza Mbatia kwenye kipindi cha Dakika 45, jana atanielewa zaidi.

Mbatia alizungumza mambo mengi sana kuhusu uchumi as long alikuwa anasimama kama Waziri wa Kivuli wa Fedha..

Kwanza alianza kusema Tanzania ni nchi ya pili Duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya Utalii kitu ambacho si cha kweli..
Kwa Africa tu, Tanzania inashika nafasi ya Kumi kutembelewa na watalii kwa takwimu za 2013 kutoka (UNWTO) United Nations World Tourism Organization..

Kama sisi ni wa pili Australia na Switzerland ni za ngapi?

Hapa lazima tufikirie nje ya box..

Mbatia aliongea Uongo mwingine aliposema
Uingereza ilihama kutoka kwenye Ukabaila kwenda kwenye Ubepari (Feudalism to Capitalism) mwaka 1948...!!

What is this? Anatofauti gani na Mulugo aliyesema Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili Visiwa vya Zimbabwe na Pemba?

Wanasiasa lazma wawe makini hasa wanapo Ongea kwenye Vyombo vya habari ambapo Watu wanafuatilia,

Maneno "Kuwa na vivutio vingi vya utalii" na "Kutembelewa na watalii wengi" hayana tofauti ? Kumbuka unaweza kuwa na vivutio vichache duniani, lakini ukaongoza kwa kutembelewa na watalii kutegemeana na jinsi unavyojitangza na ulivyoboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na ukarimu wako (customer care) kwa wageni ili wanaporudi makwao wasimulie wenzao au wao wenyewe watake kurudi tena (repeat tourists)
 
Wee jamaa mbulula kweli kwelu. Labda sie Tanzania hatujitangazi ndo maana hatutembelewi sana ila haiondoi dhana kuwa tunavyo vivutio vingi ikiwa ni pamoja na ww usijeweza tofautisha kati ya 'uwingi wa vivution' na 'kutembelewa sana'

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Kwanza alianza kusema Tanzania ni nchi ya pili Duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya Utalii kitu ambacho si cha kweli..
Kwa Africa tu, Tanzania inashika nafasi ya Kumi kutembelewa na watalii kwa takwimu za 2013 kutoka (UNWTO) United Nations World Tourism Organization..
Kama sisi ni wa pili Australia na Switzerland ni za ngapi?

Mkuu uwe makini siku nyingine unapojaribu kufafanua kauli iliyotolewa na mtu mwingine...

Kwa namna tu ulivyoandika hapa ni dhahiri kuwa uelewa wako wa lugha ya Kiswahili una mushkeli...

Kuwa na vivutio vingi ni suala moja, kutembelewa na watalii wengi ni suala jingine kabisa...

Unaweza ukawa na vivutio vingi lakini huvitangazi, sasa sijui hapo utapataje watalii wataokutembelea!!! Na pengine huu ndio ulikuwa msingi wa hoja ya Bw. Mbatia.
 
Mbatia aliongea Uongo mwingine aliposema
Uingereza ilihama kutoka kwenye Ukabaila kwenda kwenye Ubepari (Feudalism to Capitalism) mwaka 1948...!!

Hili bila shaka lina utata kidogo maana si kama ambavyo vitabu vya kumbukumbu za kihistoria vinabainisha...

Kwa mujibu wa mwanazuoni/mwanafilosofia maarufu Bw. Marx, capitalism huko falme za uingereza ilianza mnamo karne ya 18 na ilikuwa ni mabadiliko kutoka feudalism.

Na hii ndio aina ya kwanza kabisa ya capitalism ambayo kimsingi inasemekanika imegawanyka katika vipindi vikuu vitatu.
 
Wewe utakuwa unatumiwa na Lyatonga Mrema kama wewe si mwenyewe.Tambua yeye alizungumzia wingi wa vivutio na si wingi wa watalii. Jua Afrika mashariki mwaka jana tumeongoza kwa watalii kwa kuipiku Kenya.
 
Yeye anaongelea vivutio wewe unaongelea kutembelewa.

Hebu weka sawa hapo.

Hata hivyo, ukishakuwa UKAWA akili zako haziwezi kuwa sawa. Kutaka kuhatarisha amani ya nchi iliyopiganiwa kwa miaka mingi ni laana kubwa.

Mkuu usisome mambo kwa kukurupuka wewe, hivyo vivutio vingi ni katika level gani?
Hizo nchi zinazotembelewa ni nini kinasababisha hadi zinatembelewa?
 
Mkuu uwe makini siku nyingine unapojaribu kufafanua kauli iliyotolewa na mtu mwingine...

Kwa namna tu ulivyoandika hapa ni dhahiri kuwa uelewa wako wa lugha ya Kiswahili una mushkeli...

Kuwa na vivutio vingi ni suala moja, kutembelewa na watalii wengi ni suala jingine kabisa...

Unaweza ukawa na vivutio vingi lakini huvitangazi, sasa sijui hapo utapataje watalii wataokutembelea!!! Na pengine huu ndio ulikuwa msingi wa hoja ya Bw. Mbatia.

Asante mkuu kwa kuona kitu, ila katika maelezo yangu ya awali nimesema lazima tufikirie kidogo nje ya box..
Jaribu kuipitia jiografia ya Dunia tuliyomo halafu pima tu,
 
Wewe ndio Mulugo kama hauwezi kutofautisha nchi yenye vivutio vingi na iliyotembelewa na watalii wengi

Unaamini kuwa Tanzania ni nchi ya Pili kwa kuwa na Vivutio vingi Duniani?
au nawewe ni wakufuata mkumbo tu ?
 
Wewe utakuwa unatumiwa na Lyatonga Mrema kama wewe si mwenyewe.Tambua yeye alizungumzia wingi wa vivutio na si wingi wa watalii. Jua Afrika mashariki mwaka jana tumeongoza kwa watalii kwa kuipiku Kenya.

Kuna Afrika Mashariki kuna Afrika na kuna Dunia..
Je, na wewe unaamini kuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na Vivutio vingi Duniani?
1...........
2 Tanzania?
3...........
4..........

At the same time tuwe wa
109......
110 Tanzania
111...........

kutembelewa na Watalii Duniani?
 
kama watalii wanakabwa.kama wanaibiwa mahotelini.kama wenyewe tunajitia nuksi za ugaidi.kama hatujitangazi.unategemea watalii watakuja huku tz
 
Kujitangaza ni muhimu sana mkuu!
Ila kutia nyongeza nyingi haina maana..
 
kama watalii
wanakabwa.kama wanaibiwa mahotelini.kama wenyewe tunajitia nuksi za
ugaidi.kama hatujitangazi.unategemea watalii watakuja huku
tz

suala sio watalii ni watalii wa aina gani? hatuhitaji watalii kama wa mombasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom