James Kisaka Hatunaye

James Kisaka Hatunaye

iNaLillah WaiNa iLaiyhi rajiun... Poleni kwa wote.. alazwe pema.AMIN
 
[h=3]RAMBIRAMBI MSIBA WA JAMES KISAKA[/h]

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka (57) kilichotokea leo asubuhi (Desemba 25 mwaka huu) katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa. Mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni Ndovu ya Arusha, Volcano ya Kenya na Small Simba ya Zanzibar.

Akiwa mwanafunzi Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam aliwahi kuchezea timu za Oysterbay Stars, Eleven Stars ya Msasani, Sigara wakati ikicheza Ligi ya Temeke na Nyota Nyekundu kabla ya kutua Simba.

Pia alikuwemo kwenye timu ya Taifa ya vijana iliyokwenda Zimbabwe kwenye sherehe za uhuru wan chi hiyo mwaka 1980. Vilevile alikuwa mmoja wa wachezaji waliounda kombaini ya Tanzania ya UMISSETA akiwa na akina Said George, Nico Njohole, George Kulagwa na wengine. Hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Benny Kisaka, James alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kufa ganzi na matatizo ya kutoona vizuri.

Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Mwisho (Kwa Yusuf), na anatarajia kuzikwa nyumbani kwao Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kisaka, klabu ya Simba na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Marehemu Kisaka ameacha mjane na watoto wanne. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

Boniface Wambura Mgoyo

Kaimu Katibu Mkuu

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF
 
Eeh Mwenyezi mungu amrehemu na amuweke mahala pema peponi AAMINA.
 
Haa hivi mtu anaweza kufa kwa kuumwa macho?
 
Tutu vengere toa tamko la kusikitishwa na kifo hiki
 
R.I.P.rafiki yangu JAMES KISAKA nitakukumbuka daima kwa ushauri wa hekima wakati tulipofanya kazi wote AFC (NDOVU), DULUTI S.CLUB.Mungu aipumzishe roho yako mahali pa amani.Amen!
 
RIP James Kisaka, thanks for good memories....Poleni sana wana familia wote kutokana na msiba huu mkubwa uliowafika.
 
Inasikitisha ila cha msingi tuzidi kuomba Mungu ampokee kwa Amani.
R.I.P Kisaka(kocha wetu)
 
Kisaka ya dunia umemaliza sasa pumzika kwa amani
 
rest in peace my uncle!!! james kisaka!! mbele yako nyuma nyuma yetu!!
 
Back
Top Bottom