Jambo gani umewahi kusingiziwa likakudhalilisha kwenye jamii?

Nilisingiziwa kubaka mtoto (13) na jamaa (ndugu) kisa aliona wivu maendeleo yangu. Miaka 30 sio mchezo. Nililala polisi siku moja, ikaonekana ni uwongo nikaachiwa huru. Huyo jamaa kumsamehe ni mpaka Mungu amsamehe shetani.
Hili swali fikirishi, Hivi kwani Mungu ana kisasi na shetani?
 
Kwa ss kuna jamaa tunafanya nae kazi amenisingizia na kunichafua sana kazini kulitokea hitilifu nikapoteza kazi ya mteja bahat mbaya mteja alivokuja ofisin akawajaza maneno ya uongo nilichofny nikarudsha hela kwa yule mteja lkn bdo jamaa anaendelea kunichafua nimemuonya mara kadhaa lkn anakataa kua hafany hvyo lkn ushahid nnao wa sauti na wa picha (screenshots) maana anaowaambia maneno mabaya huwa wananiambia...nmejaribu kumuepuka lkn bdo ananifatilia tu na kuendelea kunichafua JE NIMFANYE NINI HUYU MTU?
Muachie Mungu,yeye hujibu kwa wakati, Usijaribu kumjibu.
 
Shetani alifanya kosa dogo (kujilinganisha na Mungu) akatupwa duniani kulingana na waliosuka hii hadithi.
 
Duuuh nshawahi kusingiziwa mambo mengiii ila katika yoote haya ya wanawake yananikeraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mpaka leo.

1. Nilishawahi kuwa karibu sana na dadangu mmoja bhasi muda nikiwa free lazima nipitie shop kwake na lazima ataniacha na chochote mfukoni, bhasi kipind nipo form6 sikufanikiwa kurudi home na wazazi wakawa wamehamishiwa sehemu nyingine kikazi bhasi nimemaliza form 6 nimerudi home (makazi mapya ya wazazi) tukawa tunawasiliana kawaida tuu na sista mwezi wa nane binamu yangu(wakiume) akanipigia simu "OYA VIPI MWENZIO AMEJIFUNGUA" nani? "DADA AKO ....." Nikamkatia simu simu nukaruka kwa DADA vipi nasilia una mtoto? ,jibu lake "POLE KWANI HUJUI KUWA WEWE NDIO BABA MJOMBA? , KILA MTU ANASEMA ETI WEWE NDIO BABA MTOTO" bhasi kwa kuwa alikua sista angu sana nikachukulia poa ila mpaka mtoto amekua ndio watu wamekuja kujua sio mtoto wangu.

2.Katika makazi mapya tulikua na beki tatu anaimba kwaya bhasi akawa na mchizi wake yupo kwenye kwaya humohumo bhasi kuna siku usiku huyo jamaa akaja home na kademu, akamuomba beki tatu kale kademu kalale pale home beki tatu akaniita, Binafsi nikaona sio shida kwa usiku mmoja tuu kakalala na beki tatu kesho yake pia kakabaki pale home ila siku ya tatu kakaondoka bhasi kalipoondoka kumbe beki tatu alikapatia namba yangu kuwa wakitaka kuwasiliana kapige kwangu, Siku moja usiku nikaona call kupokea nikauliza nani? MIMI FULANI NATAKA KUONGEA NA ..... nikampelekea simu wakamalizana baada ya siku kadhaa tena kakapiga simu nikapeleka simu wakamalizana huko, baada ya simu kurudi nikatumiwa sms SIO KILA NIKIPIGA SIMU NATAKA NIONGEE NA .......(JINA LA BEKI TATU) nikajibu poa ila nilikua nimekapiga gepu sana nikikachukulia kama mdogo, BAADA YA SIKU KADHAA KAKANIPIGIA SIMU KUWA KAPO arusha kidogo tena kakaniomba hela ya nauli maana kanaumwa halafu kapo DAR nikakapotezea zikapita wiki tatu nikatuma sms WEWE MZIMA AU ULISHAKUFA? bhasi t6atzo lilianzia hapo kwnye hiyo sms, kumbe jamaa aliyeniombe kalale nyumbani siku moja alikapangia gesti na akaandika na mke wake jamaa kapiga show mpka demu kajaa mimi kisa sms NIKATUHUMIWA NIMEKAPA UJAUZITO, bhasi ishu ikavuma hadi kanisani kila mtu akawa ananinyoshea kidole ila mwaka jana jamaa amekaweka ndani na wanamtoto tayari, baada ya miaka mitano ukweli ndio unajulikana

3.Hili ndio limenifanya kuandika mimi sio mwandishi mzuri wala sio mchangiaji ila kuna madhira unapitia inakubdi tuu kutoa la moyoni, baada ya kupitia changamoto kadhaa za maisha niliamua kujichimbia bushi fulani ili kufanya kilimo bhsi mwanaume nikakomaa kwa kilichonipeleka, Nilipanga geto la nje kwnye nyumba yenye mabinti wawili bhasi kuna siku nimetoka shamba nikamkuta binti wa mwnye nyumba anatoka geto kwangu aliponiona akanikimbia sikutilia maanani sana maana nilishahisi kuna mtu huwa anaingia mle geto na tunashare nae mafuta ya kupakaa sikuona shida sanaaaa juu ya hilo ila siku nyingine asijue nipo ndani aliongea neno moja linaukakasi sana "kwa kilugha" na aliekua anazungumza nae akamtonya kumwambia kuwa unaemsema anaelewa hiyo lugha bhasi akamuuliza kwani yupo? akamjibu nilisikia mlango umefunguliwa bhasi dogo akaja kuthibitisha akasukuma mlango ukawa umefungwa kwa ndani, jion yake nikaenda kwa jamaa mmoja nikamuuliza hichi kijiji nasikia akija mgeni huwa haondoki kuna ukweli hapo? akaniambia usijaribu kumtaka binti yoyote hapa kjijini watakuloga utaishia hapahapa nikaonyweshwa na mifano ya watu waliokuja pale mwisho wa siku wakabaki kama walivyokuja baada ya kujichanganya na hizo ammbo, bhasi toka hapo nikawa najichunga sna hata kula nakula kwa mawenge labda nikipata time ndio napika mwenyew, siku moja sina huili wala lile nasikia binti wa yule mama ni mjamzito duuuh na tetesi inasemekana ni mimi ndio nimefanya hyo kazi kwamba huwa nawahi kutoka shamba ili nimlale hyo binti, Duuuuh hiyo kaul iliniumiza sana ukichanganya na maisha ninayopitia bahsi nikaunganisha dot na kauli aliyoongea kwa kilugha yule binti nikawa nimepata jibu nusu bhasi nikisubiri mazao yangu yakomae ndio nisepe kimyamya, siku moja nachukua boxer nikaoge nakuta mpangilio niliouweka sio ule na boxer zote zimefukiwa na kukunjwa vizuri kitu amabcho kilinifilisha sanaaaa, nikarudi kitaa kukusanya data jamaa wakaniambia wanawake wa hicho kijiji wanatumia sana nguo za ndani kuloga wanaume bhasi niatupa boxer zooooote nikavuna matitikiti niksepa mazima ila niliacha nyanya zangu sijavuna.

4.Huu wa mwisho ndio bado nipo nao, nipo maeneo fulani na kikubwa kilichonileta huku ni biashara bhasi nilikua naenda church kusali nitatoakea kuwa na mazoea na dada mmoja na nilikua nahitaji connection za vijiji fulani wanalima sana mpunga, bhasi yuile adada akaniambia poa tutakua pamoja, sikuwa najua kazi yake ila nilihisi ni mfanyabiashara kumbe ni beki tatu ila yupo huru kufanya mambo yake, katika mazoea na ukaribu kumbe demu alikua anajitangaza natoka nae na tunampango wakuoana ila alifanya bila mimi kujua, baadae nikawa simuelewi yaani analeta mapenzi m,engi afu nikimwambia anipe hizo connection anazingua utafikiri yeye ndio kanipa mtaji bhasi nikaona hatuendani nikaachana nae akipiga simu sipokei, demu mwngne wa mule church akanipa connection ila sababu ya ugeni na nilikua nimeshakaa muda mrefu hapa hela ikawa imepungua nikamuomba huyu dada anitafutie mkopo afu mimi nitakua narejesha taratibu kupitia yeye dili likafanikiwa bhasi ikabd niwe close na huyu dada ili kujenga uaminifu, Kumbe hili demu ambalo ni beki tatu linaujauzito na lengo l;ake linipakazie mimi niulee, bhasi mimi bilka kujua nashangaa siku naitwa na katibu wa kanisa AKANIULIZA KIJANA UNAMAHUSIANO NA HUYU BINTI ? "ambaye amenidhamini kwenye mkopo " nikajibu HAPANA NI UKARIBU TUU WA BIASHARA NIKAMUONESHA NA SMS ZA MAREJESHO YA HELA, AKANIULIZA TENA VIPI NA YULE BINTI ULIEMPA UJAUZITO MBONA UMEMTELEKEZA? ikabd nimuulize binti yupi tena akaniambia mliekua karibu siku za nyuma NILIKOSA JIBU MAANA NILIKUA SIJUI KAMA NII MJAMZITO, anyway tulipoachana na katibu wa kanisa nikampigia simu demu nikamzingua sana, kumbe bhasi mimba ni ya boss wake mume wa dada yake wanakaa naye na mimba ni kubwa hawezi kuitoa miezi6 ila alitaka kuitoa ikiwa na miezi mitano dadaake akamzingua, akaona suluhisho ni kujiua bhasi akanunua sumu kainywa halafu kanitumia sms mimi kuwa " UNAYACHUKUA MAISHA YA MTU HII DAMU ITAKULILIA MILELE" jioni napigiwa simu na huyo demu alienidhamini ananiambia kimbia ondoka kabisa hapa, ...... amekunywa sumu na sasa yupo ICU nadhani sms yake uliipata so wanakutafuta nikamwambia sikimbii wala siondoki wakitaka waje au hata mimi mwnyw nitawapigia simu, MUNGU NI MWEMA demu alipona hajafa na mimba haijatoka ila bado demu amebaki na msimamo wake kuwa mimba ni yangu na jamii inaniangalia kwa jicho baya eti nimekataa mimba na nimesababisha mtu atake kujiua, ANYWAY BIASHARA IMESIMAMA NA KESI IMEISHA IJUMAA ILIOPITA TUNASUBILI MTOTO TUPIME DNA THEN MENGINE YATAFUATA ILA KWA HILI LIMENIUMIZA KULIKO YOOOOOTE NA SIONI NAMNA YA KUMSAMEHE HUYU DEMU KUNA MUDA NATAMANI NIMNUNULIE SUMU INAYOUA MAPEMA ILI ATANGULIE TUU MAZIMA MAANA AMENICHAFUA NA AMESABABISHA UCHUMI WANGU UMEYUMBA NA DENI LIMEONGEZEKA. YAANI HAPA NI STRESS TUUU
 
Kuna jamaa alipanda lift (Elevator) na demu, gorofa inayofuata demu kashuka kumbe amejamba, jamaa kufika gorofa inayofuata demu mwingine kapanda kakuta lift inanuka kijambo. alijaribu kujielezea kwamba sio yeye nani anakuamini na hakuna ushahidi.
 
hapo sawa mkuu

Mama mkubwa pamoja na watoto wake wawili wa kiume walikimbilia nyumbani kwetu baada ya mama mkubwa kugombana na mume wake na kutimuliwa. Basi wakakaa pale kama miezi mitatu hivi wakati huo mi naendelea na shule, hao watoto wake walikua wameshamaliza std 7 na hawakuendelea na masomo wapo wapo tu.

Sasa pale home kulikua na baiskeli tumeiweka stoo maana ilikua haitumiki mda mrefu tu, japo ilikua nzima kabisa. Siku moja nimeingia stoo kutafuta nini sijui, nika notice kwamba baiskeli haipo! Uliza kila mtu anasema hajaichukua. Mshua aliporudi nikamueleza kwamba baiskeli siioni na hatujui nani ameichukua. Cha ajabu mama mkubwa pamoja na wanae wakaungana na kumuambia mshua kwamba mimi ndio niliitoa baiskeli na kwenda kuiuza na kwamba wana ushahidi maana waliniona kabisa! Aisee aisee aisee... nilijitahidi kujitetea kwa kila njia lakini wao wamekomaa kwamba ni mimi. Mshua alini mind kinomaaa maana alikua ananiamini. Nakumbuka nililia sana siku hiyo na nikatamka maneno "haya machozi yangu yatawarudia"

Baadae mamkubwa alikuja kurudiana na mume wake lakini baada ya miaka kama mitatu mtoto wake mmoja akakurupushwa kwa wizi, wananchi wenye hasira wakampa kichapo hevi na kumtoboa jicho moja. Yule wa pili akaja kugundulika anajihusisha na ushoga. Yule mwizi aliendelea na wizi hadi alipokuja kupigwa sana akafia hospitali. Shoga alikuja kufa pia miaka michache baadae baada ya kuugua mda mrefu.
 
daah noma
 
Mwaka mmoja niliwahi "kuzushiwa" nimegonga mke wa mtu. Ukweli ni kwamba niligonga (nilishatubu) maana yule dada aliniganda sana na mme wake alikuwa Ulaya kimasomo. Nasema nilizushiwa kwa sababu ilikuwa siri ya watu wawili tu,na tulienda kufanyia mbali watu wa karibu wasione. Sasa hawa wazushi walijuaje
Inauma sana
 
Mama mkubwa pamoja na watoto wake wawili wa kiume walikimbilia nyumbani kwetu baada ya mama mkubwa kugombana na mume wake na kutimuliwa. Basi wakakaa pale kama miezi mitatu hivi wakati huo mi naendelea na shule, hao watoto wake walikua wameshamaliza std 7

Sasa pale home kulikua na baiskeli tumeiweka stoo maana ilikua haitumiki mda mrefu tu, japo ilikua nzima kabisa. Siku moja nimeingia stoo kutafuta nini sijui, nika notice kwamba baiskeli haipo! Uliza kila mtu anasema hajaichukua. Mshua aliporudi nikamueleza kwamba baiskeli siioni na hatujui nani ameichukua. Cha ajabu mama mkubwa pamoja na wanae wakaungana na kumuambia mshua kwamba mimi ndio niliitoa baiskeli na kwenda kuiuza na kwamba wana ushahidi maana waliniona kabisa! Aisee aisee aisee... nilijitahidi kujitetea kwa kila njia lakini wao wamekomaa kwamba ni mimi. Mshua alini mind kinomaaa maana alikua ananiamini. Nakumbuka nililia sana siku hiyo
pole sana mkuu bt mungu tayari kashakujibia.
 
Mwaka mmoja niliwahi "kuzushiwa" nimegonga mke wa mtu. Ukweli ni kwamba niligonga (nilishatubu) maana yule dada aliniganda sana na mme wake alikuwa Ulaya kimasomo. Nasema nilizushiwa kwa sababu ilikuwa siri ya watu wawili tu,na tulienda kufanyia mbali watu wa karibu wasione. Sasa hawa wazushi walijuaje
Inauma sana
mkuu hapa hukusingiziwa sema siri ilivuja, kusingiziwa ni kile kitendo hujafanya kisha unalazimishwa umekifanya
 
Nilisingiziwa nakula mke wa mtu hadi akaachika kwa mumewe! Lakini ukweli anaujua Mungu sukuwahi kumgegeda hata mara moja! Ndugu zake yule mama hawataki hata kunisikia
 
Mama mkubwa pamoja na watoto wake wawili wa kiume walikimbilia nyumbani kwetu baada ya mama mkubwa kugombana na mume wake na kutimuliwa. Basi wakakaa pale kama miezi mitatu hivi wakati huo mi naendelea na shule, hao watoto wake walikua wameshamaliza std 7 na hawakuendelea na masomo wapo wapo tu.

Sasa pale home kulikua na baiskeli tumeiweka stoo maana ilikua haitumiki mda mrefu tu, japo ilikua nzima kabisa. Siku moja nimeingia stoo kutafuta nini sijui, nika notice kwamba baiskeli haipo! Uliza kila mtu anasema hajaichukua. Mshua aliporudi nikamueleza kwamba baiskeli siioni na hatujui nani ameichukua. Cha ajabu mama mkubwa pamoja na wanae wakaungana na kumuambia mshua kwamba mimi ndio niliitoa baiskeli na kwenda kuiuza na kwamba wana ushahidi maana waliniona kabisa! Aisee aisee aisee... nilijitahidi kujitetea kwa kila njia lakini wao wamekomaa kwamba ni mimi. Mshua alini mind kinomaaa maana alikua ananiamini. Nakumbuka nililia sana siku hiyo na nikatamka maneno "haya machozi yangu yatawarudia"

Baadae mamkubwa alikuja kurudiana na mume wake lakini baada ya miaka kama mitatu mtoto wake mmoja akakurupushwa kwa wizi, wananchi wenye hasira wakampa kichapo hevi na kumtoboa jicho moja. Yule wa pili akaja kugundulika anajihusisha na ushoga. Yule mwizi aliendelea na wizi hadi alipokuja kupigwa sana akafia hospitali. Shoga alikuja kufa pia miaka michache baadae baada ya kuugua mda mrefu.
Daah noma sanaa
 
Nilisingiziwa nakula mke wa mtu hadi akaachika kwa mumewe! Lakini ukweli anaujua Mungu sukuwahi kumgegeda hata mara moja! Ndugu zake yule mama hawataki hata kunisikia
pole mkuu, alafu ubaya wa mambo ya kusingiziwa huvuma haraka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom