Jambo gani umewahi kusingiziwa likakudhalilisha kwenye jamii?

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,109
9,407
Natumai hamjambo wakuu.

Katika maisha tunakutana na mengi, kuna wakati unaweza kusingiziwa jambo hata likakudhalilisha katika jamii wakati hujafanya wala hukuwahi kukusudia kulifanya.

Miaka ya nyuma kidogo nilikua na rafiki yangu ambae alikua na duka la HARDWARE, mara nyingi nilipotoka job nilikua nampitia kurudi home kwa sababu tulikua tunaishi mtaa mmoja.

Siku moja nikiwa nimempitia alikuja bwana mmoja akiomba chenji ya msimbazi, rafiki yangu akampa kumbe yule bwana aliondoka na pesa zote kimazingara, wakati jamaa anataka kufanya hesabu afunge duka kwenye draw ya pesa hamna kitu.

Kwakuwa mimi ndo nilikua pale dukani huyu bwana akanituhumu kumuibia kimazingara, dah! Nikamuambia mbona siku zote napita pale sijawahi fanya vile? Jamaa hakunielewa akadai atafuatilia kwa wataalam wa kienyeji na ikiwa ni mimi atanifanyia kitu mbaya.

Mtaani akanitangaza nimemuibia lakini alipokuja kuujua ukweli aliniomba samahani, nilimsamehe japo sikutaka ukaribu naye tena.

Je, wewe jambo gani uliwahi kusingiziwa likakudhalilisha?
 
Kuna jamaa alipanda lift (Elevator) na demu, gorofa inayofuata demu kashuka kumbe amejamba, jamaa kufika gorofa inayofuata demu mwingine kapanda kakuta lift inanuka kijambo. alijaribu kujielezea kwamba sio yeye nani anakuamini na hakuna ushahidi, kwenye lift upo pele yako, unajiteteaje hapo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom