Jambazi ageuka Mbuzi Naigeria!!

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054

Mbuzi mmoja nchini Nigeria alijikuta akifikishwa kituo cha polisi baada ya kushukiwa ni jambazi lenye silaha aliyetumia uchawi kujigeuza mbuzi katika jitihada za kutoroka baada ya kukamatwa akiiba gari.

Sungusungu nchini Nigeria walimkamata mbuzi mmoja na kumfikisha polisi kwa madai kuwa mbuzi huyo ni jambazi lenye silaha ambaye alitumia uchawi kujigeuza mbuzi katika kujaribu kutoroka baada ya kukamatwa akiiba akijaribu kuiba gari aina ya Mazda 323.

"Sungusungu walikuja kuripoti kuwa katika pitapita zao usiku wakilinda walikuta kundi la vijana waliokuwa wakijaribu kuiba gari" Tunde Mohamed msemaji wa polisi wa mji wa Kware nchini Nigeria alisema.

"Walipojaribu kuwakamata majambazi hayo yenye silaha, majambazi hayo yalifanikiwa kukimbia huku mmoja wao akijigeuza mbuzi" msemaji huyo wa polisi alisema.

Polisi hawakuthibitisha kama ni kweli jambazi huyo alijigeuza mbuzi ila walithibitisha kuwa mbuzi huyo aliswekwa jela katika kituo hicho cha polisi.

Taarifa zinasema kuwa mbuzi huyo aliwekwa ndani hadi pale mmiliki wake alipoenda kwenye kituo hicho cha polisi kumtoa mbuzi huyo.

Imani za kishirikina zimeenea katika miji mingi ya Nigeria. Mwishoni mwa mwaka jana baadhi ya watu nchini humo walikuwa wakilalamika kupotea kwa viungo vya siri baada ya kusalimiana na mwanaume waliyekuwa hawamfahamu aliyekuwa akitumia uchawi wake kupoteza viungo vya siri vya wanaume.

Sungusungu nchini Nigeria wamekuwa wakitumika katika maeneo mengi ambayo polisi huwa hawafiki nyakati za usiku.
 
Very interesting, kwa hiyo jamaa amekwenda polisi kumchukua mbuzi au jambazi amekwenda kumtoa jambazi mwenzie aliyedaiwa kugeuka mbuzi!!!?
 
I would have expected polisi wangempeleka mahakamani huyo mbuzi! na kesi ingekuwa hivi
Prosecutor:mbuzi-jambazi unakabiliwa na shtaka la kutaka kuiba kwa kutumia silaha, unakiri shtaka?
Mbuzi: meeee!!
Prosucutor :ndiyo au hapana?
Mbuzi:meeee....meeee
Prosecutor:nachukulia mee yako kuwa kukubali kosa
Mbuzi:meeeeeee!!!!
Hakimu:Nakufunga miaka thelathini na kazi ngumu
Mbuzi anaachia karanga za kutosha mahakamani.
 
Ha ha ha ha hivi mbona vituko hivi vya kishirikina ulaya hatuvisikii au ndio kwamba technologia hii iko Africa tu
 

Hawa ma 419 ni kaaazi kweli kweli. Sasa wanaamua kuwa Mambuzi. Polisi wakimgeuza kitoweo si itakuwa kazi.
 
I would have expected polisi wangempeleka mahakamani huyo mbuzi! na kesi ingekuwa hivi
Prosecutor:mbuzi-jambazi unakabiliwa na shtaka la kutaka kuiba kwa kutumia silaha, unakiri shtaka?
Mbuzi: meeee!!
Prosucutor :ndiyo au hapana?
Mbuzi:meeee....meeee
Prosecutor:nachukulia mee yako kuwa kukubali kosa
Mbuzi:meeeeeee!!!!
Hakimu:Nakufunga miaka thelathini na kazi ngumu
Mbuzi anaachia karanga za kutosha mahakamani.


Haaha heheh hiiii

Meeeeeeeee meeeeee
 
Siamini kwnye imani za Kishirikina,,kuamini ushirikina ni LACK OF KNOWLEDGE

Mzee we umezaliwa europa nn?
Haujasikia ile ya gongagonga ambaye amemega kijiji kizima watu bila kujua wanamegwa?
Endelea kubisha uone siku moja unaamka morning una angalia nyeti unajikuta flat au kinyume chake.
Kama haitoshi nenda pande za Swanga na ukafanye uharibifu uone unavyobeba ujawepesi hata kama we ni dume.
 
subiri siku gongagonga akunyatie ndo utajua kama kuna uchawi na hayo ya lack of knowledge ndo utayaona sasa

Halafu mkuu kuna makanisa ya kileo ambayo origin yake ni Nigeria. Wachungaji wake huwa wanaenda kutoa sadaka Nigeria kila mwaka na wakirudi wanarudi na nguvu za ajabu ambazo ni walakini?? Hebu niambie koti la mchungaji linatoa mapepo?? Pete ya mchungaji akikunyoshea kidole chake unatolewa mapepo au tuseme ile nguvu ya umeme inakukamata?? Hebu niambie mchungaji anakuwa na design ya mkono ambao unaitwa healing hand na kila muumini akiwa na matatizo anapewa mkono huo na kuupeleka nyumbani eti utakuondolea matatizo na unazunguka kwa waumini wa kanisa!! Siku za mwisho manabii wa uongo wataibuka. Je mambo haya yanaashiria siku za mwisho??

Nduguzanguni tuwe makini sana na mambo mengi ambayo origin yake ni Nigeria???

Aluta continua, nyumba ya upashanaji habari JF.
 
Back
Top Bottom