Jamani ZAIN challenge!

"Thinking outside the box" Nafikiri hapa kuna tatizo la kutojiandaa, wenzetu wanaandaliwa na Lecturer kwenda kutangaza vyuo hivyo. Vyuo vyetu havijagundua hilo, Maswali yale siyo magumu bali wanafunzi wanaoenda pale wanakuwa hawawezi ama hawajatayarishwa vizuri . Ukiuulizia process ya kuwachagua washiriki huku kwetu utakuwa hakuna bali watu wanaokotwa kwa kujuana tu. Wenzetu ni Mchujo toka mwanzo na Best ndiyo wanaenda. Lazima tujue “Poor preparation……….. “

Mdau mwingine ameongelea EA community ni kwamba hapo ndo tutalia si kwa sababu wenzetu ni wazuri, bali wao wanajipanga. Toka Mwanzo wao hasa Wakenya walikuwa na Wizara, sisi hatukuwa nayo, wao wakija kwenye Mijadala wanakuwa wamejitayarisha na kuweka mambo yao sawa sisi sifuri. Msingi mbaya tutaumia tu, na wana-SIHASA wetu wanataka waitwe "President, Minister, etc of EA country". Mseveni alisema hawezi kuachia uraisi hadi pale atakapokuwa RAIS WA KWANZA WA AFRICA MASHARIKI


Mdau aliyeulizia juu ya “Communication barrier” kizazi cha st.yyyy kinaanza kuondoa tatizo hilo.
 
Sina uhakika lakini hata kama hawapewi kuna maandalizi ya binafsi unatakiwa kuwa nayo kabla ujajitosa kwenye hiyo competition sio suala la kwenda kuuza sura huko kwani inatia aibu hata maswali mengine yalikuwa ni common sense tu. Ni vizuri kabla ya watu kushiriki wajipime na uelewa wao. Maswali mengi yahitaji mtu ambaye anapenda kujisomea sana vitu vya aina mbalimbali, historia Science, Magazeti, mdadisi, Mtazamaji wa TV mwepesi wa kujibu maswali haraka etc. etc. lakini ukiwa ni mtu wa kujifungia sio rahisi . Naomba iwe ni somo kwa wengine otherwise tunatia aibu
 
That is not the case mzee, maana Kiingereza kinachotumika sio kigumu kiviile mtu akashindwa kuelewa!! ni upeo mdogo tu wa mambo ya kidunia!!
Ama kuna ka phobia flani ka studio lighting na cameras, coz am sure that the participants are not in any way less intelligent than the rest, its just that kuna kale kauoga flani they experience when participating in the program. It happens to the best of us, in interviews, exams, where you can go blank after being asked something you are conversant with...
 
si ajabu wanaowachagua wawakilishe wenzao nako kuna tatizo labda wanachaguana kwa kujuana maswali mengine kwa kweli ni marahisi sana.
 
hapo kwenye kibluray ndo nimepaka rangi



Kimey 'bite you tongue' (sijui ni ki-noname hicho)...
ile wee unaona si tatizo lakini nakwambiaje lugha ni kikwazo....believe you me!!
nilimshuhudia graduate wa sheria chuo fulani alikwenda kuomba attachment kwenye law firm......jamani unaweza kulia!!! wewe unaesikiliza unatamani kuingia chini ya meza!!!!

pamoja na hayo nadhani upeo wetu bado ..tunahitaji kukaza buti zaidi am sure we can bana kwani nini!!!
mbona wale wa jana ki bluray chao kilikua shwari tu...nilicho note jana ni kua hawakua wanajua majibu hasa yule mdada wa MD 4th year!! unajua kwenye ile zain challenge kuna mambo mawili ili uweze ku win...moja ni kua na good timing ya kubonyeza na pili kuelewa swali!! sasa kwa jana jamaa wa Tumaini yote walikosa!! ilikua mshike mshike!
 
hivi kati ya wana JF hakuna ambae ni mhusika(mwanachuo) atueleze kidogo nini tatijo bana.

mi naona aibu kuona vyuo vya nchi angu vikipigwa kumbo. you can imagine wenzetu wa kenya kama jana wao ndo wametawala mchezo.inafika kipindi wanapoint 495 sisi tuna 95,,,,, jamani hii gepu duuuh.

hadi wakati mwingine nikisikia wiki ijayo ni chuo cha Tz naanza kuomba umeme ukatike ili hata nisiangalie. maana nikiangalia naumia roho tu.
 
si ajabu wanaowachagua wawakilishe wenzao nako kuna tatizo labda wanachaguana kwa kujuana maswali mengine kwa kweli ni marahisi sana.
May be kwa wao wanona sawa tu apite asipite anondoka na dolar 1000, bila kufikiria kua wanakipaka matope chuo chao!!
 
si ajabu wanaowachagua wawakilishe wenzao nako kuna tatizo labda wanachaguana kwa kujuana maswali mengine kwa kweli ni marahisi sana.

wasiwasi wangu uko hapo hapo
sijui vigezo gani vinatumika
au ndo magumashi mjini as usual....
 
nakumbuka mashindano haya mara ya kwanza Mzumbe walifikia nafasi ya tatu so taratibu tutafika wala hakuna haja ya kuwa na wasi wasi, tuongeze bidii ktk maandalizi.
 
mbona wale wa jana ki bluray chao kilikua shwari tu...nilicho note jana ni kua hawakua wanajua majibu hasa yule mdada wa MD 4th year!! unajua kwenye ile zain challenge kuna mambo mawili ili uweze ku win...moja ni kua na good timing ya kubonyeza na pili kuelewa swali!! sasa kwa jana jamaa wa Tumaini yote walikosa!! ilikua mshike mshike!

Meku walikosa yote????
aaaaah tafadhali bwana.....

ndo maana mi nasema pamoja na ukweli kuwa tuna tatizo la lugha lakini pia kuna kitu hakipo sawa mahali.......
 
Ama kuna ka phobia flani ka studio lighting na cameras, coz am sure that the participants are not in any way less intelligent than the rest, its just that kuna kale kauoga flani they experience when participating in the program. It happens to the best of us, in interviews, exams, where you can go blank after being asked something you are conversant with...
Hii nayo inaweza kua one of the reason....
 
Wanajisomea magazeti ya udaku ndo maana wana knowledge za kiu:wink:dakudaku! Zero kabisa!!!!!
 
Meku walikosa yote????
aaaaah tafadhali bwana.....
ndo maana mi nasema pamoja na ukweli kuwa tuna tatizo la lugha lakini pia kuna kitu hakipo sawa mahali.......
Acha tu wangu hebu ulizia marudio lini then utakuja kunipa feeback!! unajua kuna kupitwa kwa timing ila kwa jana gap ya point ilikua inatisha!!
 
Naona Tuwe tunajitoa mapemaaa ili kukwepa hii aibu. Inatoa picha mbaya kwa Taifa kwa ujumla. Wanapoenda intaneti waangalie websites za elimu na general knowledge, sio kutizama picha za NGO + NO!!!!!!!!
 
marudio yake angalia channel 112 DSTV. soma kwenye monthly program handout utaona kinarudiwa lini
 
English is not reachable in their minds, thats all they remain silent even they know what should be the answer. Sometimes they feel shy may be, i just try to mention.!
 
Siyo kwamba hawana elimu, tatizo ni confidence ndo inakosa, mara nyingi ndugu zetu wanakuwa na inferiority complex katika kujibu!
 
Uwoga, ushamba, lack of confidence, lack of preparation all in one. This things are not automatic lazima wafanye mazoezi and that is where Zain kama sponsor needs to come in. Kuwapa access to internet and reading material ili waweze kujitayarisha vizuri. Halafu wanatakiwa washindanishwe na wenzao at 3 times kabla hawajaenda kwenye mashindano. Nimesomea vyuo vya Kenya na hawa watu are serious about this competitions. Kila wiki timu iliyochaguliwa kurepresent chuo wanashindanishwa na wenzao kama part ya matayarisho so by the time wanaenda kwenye mashindano confidence zao ni za hali ya juu. Hapa nadahani tatizo linaanzia kwenye selection kwani if you mess up there even the team that you will send to represent will mess up. Zain wao wanafacilitate mashindano lakini hawajihusishi sana na maandalizi ya teams zilizochaguliwa na this gives them a bad negative association kwani there's no return on the investment. Lakini hawana budi kuendelea na sponsorship hii since ni ya karibu bara zima but i'm sure wenzao huwa wanachekelea coz every year our teams are the laughing stock.
 
Back
Top Bottom