Jamani wataalam naomba kusaidiwa tafsiri ya ndoto hii

Greatthinker47

Senior Member
Sep 24, 2021
122
183
Ni kama harusi ila namuona Baba yangu amependeza hajavaa suti Mwl Haule aliyekuwa mama yangu wa kambo kabla ya kuachana na Baba yangu pia akiwa amependeza hajavaa mavazi ya harusi(Shela) ila anatembea akicheza.

Mbele akiwa na Tumain Moto wake wa kike ameshika vitu kama maua na Mimi natokea katika chumba tofauti ambako ndiko nilikuwa navaa Nimevaa suti ya rangi ya kaki kubwa inayoonekana kubwa kwangu naenda kupanga mstari kwenye watu ambao naona kama wahusika wakuu au watu maalum zaidi katika sherehe ile sambamba na ndugu zangu tofaut tofaut ninaowafaham na wengne sikuwa nikiwafaham.

Lakini baada ya kutawanyika naonekana kutengwa na wale wote niliokuwa nimepanga nao mstari ila napelekwa chumba cha pili ambacho kina ngazi nyingi zinashuka Hadi kufika walipokaa watu ndani ya chumba kile nakutana na watu wengii marafiki ninaofahamiana nao wote wakiwa na shauku ya kusalimiana nami huku nikionekana kama mtu mhusika zaidi katika kusanyiko lile.

Nachagua kukaa sehemu ya nyuma zaidi desturi yangu hata nilipokuwa nasoma kwenye kusanyiko lolote lile huwa sichagui kukaa mbele kule nakutana na rafiki yangu mkubwa nilie nae hadi sasa yeye pia akiwa katika suti nyeusi yenye mistari mistari inayounda draft nying kweny sut yake juu na chin katika chumba kile Sisi pekee ndio tuliovaa suti ila mim naonekana kuwa mhusika zaidi.

Kila mtu kutaka kuzungumza nami ila hawakuweza maana katika chumba kile ni kama kulikuwa na utaratib flan unaofanya watu wasiwe na movement za hapa na pale...ila kuna rafiki angu ambae anafahamika Kwa kuwa na masihara na utani sijui ilikuaje lakini nilimuona akitishia kukimbia na wallet yangu huku akicheka, ambayo sijui aliichukua vipi kwangu Jambo lililopelekea watu wengi katika chumba kile kucheka Sana.

Alipoona simfuati anirudishie huku nikimwambia tu nikiwa pale nilipokaa anirudishie wallet yangu akanirudishia...baadae rafiki yangu yule wa suti nyeusi nikamwambia Mim au yey akaniambia turudi juu kwenye sherehe kuu tukapanda ngaz zile nying zenye Hadi juu pale rafk angu akapotea.

Mimi nikataman kurud kule chin maan kulkuwa na washkaji nikarud tena chini mara hii nikawakuta wako bize bizee sikupenda Hali ile nikazugazuga nikarud juu. Nilipofika juu nikakumbuka marafik wa kike warembo nikarudi tena ila nyakati zote wakat wa kurudi chini nilikuwa nikirudi Kwa shida kama mtu anaeogopa kuanguka maana ngazi zilikuwa ndefu na sikuwa nikipenda ni kama nilikuwa nikilazimishwa na matamanio yangu au nguvu fulani Hadi nilikuwa nikiwapisha watu waliokuwa wakishuka Kwa Kasi kana kwamba ni wazoefu kushuka ngazi zile kuliko Mimi.

Ile nataka kuingia ambako marafik wamekaa nikamuona mdada mmoja ambae nilipokuwa chuon darasan week ya kwanz nilitokea kupend kampan yake alikuw amejtenga kweny chumba chenye viti viwili vilivyotengwa na meza katikati huku yeye akiwa katika kiti kimoja kiti kingine kikiwa hakina mtu basi nikaenda kukaa Mim katika kile kiti ili nipate kuzungumza nae Ile nimekaa nataka kuzungumza akaja msimamiz wa eneo lile akasema haturuhusu mazungumzo ya faragha basi bila kuniaga Yule dada akainuka na kuondoka huku akiniacha namuangalia na suti yangu yeye akiwa amevalia suruali nyeusi huku ameikunja kidogo miguuni kama wavaavyo mabint siku hiz.

basi na Mimi nikamfuata ila sikumuona Bali nikajikuta tena nimeungana na marafik zangu wale ambao safari hii walikuwa wakiniangalia kana kwamba naenda juu na kurudi nikipanda ngazi na kushuka ili nionekane Kwa watu...mim pia nilikuwa nikijiskia vibaya maana nilijihisi ni kama najionyesha kwavile sherehe inanihusu pia nimevalia suti nzuri wao hawajavaa suti kwaio nikawa najistukia..

Ile nawaza hayo mara watu wote wakatoweka akatokea rafiki yangu pamoj na ndugu yangu mmoj na mtu mwngn ambae ckumfaham...akiniambia umechelewa kwenda katika sherehe na Jambo muhimu zaidi katika familia yako.

Hapo nikakumbuka kuwa ni sahihi bas nikakimbia ngazi Hadi juu kurudi juu ilikuwa rahisi mara zote kuliko kushuka ila safari hii huku nakimbia nilipofika katkat nilihis uchovu kidogo ila nikajitahidi Hadi juu.

Ile nafika katika chumba walichokuwepo watu wa familia yangu tukakuta ni patupu pasi na mtu hata mmoja ikiashiria kwamba sherehe imeisha nikabaki na majuto nimekosa sherehe muhimu katika familia yangu...
 
Ulikua unaaga ndugu na jamaa bila kujielewa.. It maybe baada ya kuwaaga ukaenda kwenye chumba (makazi ya milele) hukuwakuta.. Inaweza kua Ina maana ya kuna kifo cha one of your familiy members au wewe kabisa...fanya sala tu ndugu..
 
Muombe Mungu kama ni kitu kibaya kikuepuke, japo sijaisoma yote, wewe muombe Mungu kama ni jema basi lidhihirike kwenye maisha damu na nyama, lakini kama ña mabaya kemea kabisa yaondoke.
 
Mkuu nimeshindwa kusoma hadi mwisho. Hii ni ndoto au series? Ila kwa tafsiri ndogo ni kwamba wewe utamla mama wa kambo kimasikhara
 
Muombe Mungu kama ni kitu kibaya kikuepuke, japo sijaisoma yote, wewe muombe Mungu kama ni jema basi lidhihirike kwenye maisha damu na nyama, lakini kama ña mabaya kemea kabisa yaondoke.
Ahsante daah sijaelewa kabisa
 
Back
Top Bottom