Jamani wanawake wataadilika lini?

PAMBANA

Member
Oct 21, 2010
73
21
Salamu ndugu zangu wana JF,
Naomba kuanza na swali lifuatalo kuwa "Wanawake wa nchi hii watabadilika lini na wao kuwa chachu ya mabadiliko yanakuja katika nchi yetu?Nimeamua kuuliza swali hili kwa sababu karibu 90% ya wanawake wanakisupport chama cha cha Mapinduzi (CCM) wakati wao ndio wanaokumbana na matatizo kibao katika maisha haya ya kila siku.Kwa mfano tu tembelea wodi za akina mama wajawazito katika hospitali za serikali na vituo vya afya unaweza kulia kutokana na huduma mbovu wanazopata huko wanalala chini tena kwa kujibana au kujiegesha,yaani mama mjamzito mmoja analala huku mwingine akisubiri mwenzake anyanyuke na yeye aegeshe mgongo angalau naye alale (Nenda hospitali ya Mount Meru utajionea hali ilivyo mbaya mpaka utawonea huruma. huo ni mfano tu wa mambo wanayoyapitia hawa mama zetu.

Suala la huduma ya maji.Ninafahamu ya kuwa suala la kupata huduma ya maji safi ni haki ya kila mtanzania mahali popote pale alipo katika ardhi ya nchi hii na ni wajibu wa serikali kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya maji safi.Lakini kuna maeneo mengi katika nchi hii ambapo wanawake wanaamka alfajiri na mapema kufuata maji umbali mrefu sana pengine zaidi ya km 7 na maji yenyewe si safi kwa ajili ya matumizi ya binadamu.Kwa mfano tu kuna baadhi ya wilaya za mkoa wa Mwanza kama vile Sengerema kuna maeneo wanawake wanatembea umbali wa zaidi ya km 10 kutafuta maji na wilaya hiyo ni kiwakilishi cha maeneo mengine mengi tu ambayo wanawake wanapata dhahama hii ya kukosa maji safi.

Pia wanawake wengi ni wamama wa nyumbani kwa maana ya kwamba wanabaki nyumbani kutegemea kuhudumiwa na waume zao kwa mahitaji yao ya msingi.Kwa wengi waliopo mijini wanategemea waume zao kwaachia fedha za matumizi lakini wanapoachiwa fedha kidogo wanalalamika.

Pamoja na hayo yote na mengine mengi ambayo sijataja,wanawake ndio waa kwanza kuitetea na kuisupport CCM wakati kwa muda wote ambao CCM imekuwa mdarakani imeshindwa kutatua haya matatizo ambayo yamekuwa sugu kwa nchi hii.Tembea sehemu nyingi utaona wanawake wamevaa vilemba vya CCM pamoja na kanga.

Hivi ndugu zangu hawa mama zetu watafunguka lini na kuacha kuwatetea hawa wakoloni weusi wanaoendelea kuinyonya nchi hii? Naomba nisaidiwe kujibiwa swali langu.
 
Mpango wa wanawake kupiga kura katika mfumo demokrasia ni mpango kabambe wa nchi za magaharibi kuweza kuzinyonya nchi zinazoendelea kwa urahisi. Unajua wanawake ni watu wasiopenda mabadiliko na ni watu ambao hufuata sana mkumbo. Kimsingi hili la wanawake kushabikia maghamba linaweza kupungua kama wanawake watapatiwa elimu ya kutosha. Na si elimu ya uraia tu, ni elimu ya ujasiria mali, na elimu ya kujitegemea, hilo likifanikiwa wao wenyewe watakumbana na magamba katika utafutaji na kwa njia hiyo watawakataa wenyewe. Lakini katika kipindi hiki ambacho wanawake ni kupe kwa waume zao, hali bado ni ngumu sana. Hata kile kidogo wanachofanya tunapaswa kuwapongeza kwani kimsingi wengi wao hawana elimu na hata hawaelewi. Siku moja wakati najaribu kueleza ufisadi wa kuilipa Richamond akina mama mmoja alisema bilioni 94 ni nini mbona ni fedha kidogo tu. Ilibidi nimweleze kwa kutumia mfano wa ng' ombe wa shilingi lakin tatu. Baada ya kumweleza ni sawa na ng' ombe 3000 na kitu ndo akaanza kuelewa kwamba hawa magamba kweli wanaiba. Jamani ni ngumu sana. Kinachofanywa na uongozi huu hakieleweki kwa wananchi wengi yaani unamweleza haelewi hata kidogo. Ni kama unaanza kumweleza sheikh au padre kuhusu theory of evolution!
 
Chanzo kikubwa ni exposure,na wanaume wengi wamekuwa ni chanzo kwa wake zao kutojitambua.

Mwanamke kama chombo dhahifu,anatakiwa kujengewa uwezo wa yeye kujitambua,siyo hivyo tu,ajengewe ujasiri wa kujiamini.

Wanaume wengi wamekua vigezo vya kuwadhohofu na kuwatia hofu wanawake wao.

Tuwape nafasi wanawake wetu,na daima tuwajengee ujasiri na kuwaambia wanaweza,zaidi tuwapende kwa vitendo ili wajiamini.
 
Back
Top Bottom