Kwakweli limekuwa ni jambo la kushangaza sanaaa, katika nyakati za sasa, kwa kuona wanawake si wasichana tu bali hata watu wazima hata wengine wameolewa, wanapapalika na kufuga kucha zao za mikononi hata za miguuni hadi ziwe ndefuuuu hata kufikia urefu wa sm 1 hata zaidi, na wengine wananunua na kubandika mikucha ya bandia. Wanafanya hivyo kwa mitazamo tofautitofauti, japo wengi wao ni urembo. Kwakweli huku ni kukosa ufahamu wa kutosha.
Mimi nakumbuka enzi hizo tunasoma somo la sayansikimu tuliambiwa baadhi ya yafuatayo;-
1. Kucha ndefu huhifadhi uchafu
2. Kucha ndefu zinaweza kusababisha ajali kwoko mwenyewe kwa kuhatarisha ukucha mzima
Kufumuka,
3. Ni hatari kwa wenginge, unaweza ukamkwaruza au kumchoma mtu mwingine.,
Lakini pia hata katika masuala ya imani;- kucha ndefu huwa ni moja ya kiungo cha shetani na mapepo na majini. Ndiyo maana popote ikichorwa picha yenye taswira ya shetani lazima utaona mamikono yake yana vidole vyenye mikucha mireeeeeefu.
Sasa, hebu nirudi kwenye suala zima la kucha ndefu na uchafu.
-kimsingi wanawake ndio hasa tunaowategemea kuwa wao ndio wazingatiaji usafi namba one. Lakini mambo yamekuwa ni tofauti. Kwa sababu ukiwa na kucha ndefu lazima uchafu ufichame humo tu, halafu utahitaji kula, inakuwaje, je! Mkienda chooni mnajisafishaje? Haya ifikapo wakati wa kufua nguo hata kuoga tu, mnafanyeje kazi hizo na hiyo mikuchaaaa., haya; na wewe mama uliyeolewa unalalaje na mmeo, au ndio unataka utie jikucha la jicho??
Sina shaka kusema maono ya kufuga kucha ndefu kwa wanawake hata baadhi ya wanaume ni maono ya kuzimu, kwa sababu hayana faida yoyote zaidi ya hasara mwanzo mwisho.
Kama mmenielewa, basi kakate hiyo mikucha yako na acha kubandika ile ya bandia pia. Usiwe kichaka cha devil. Kama utakaidi na kuona mikucha yako mirefu ni mali, basi; iache ikue halafu uitumie kuitembelea kama miguu. Tafadhari badilikeni katika fikra zenu. Na mungu awasaidie mumhofu yeye.
Kwa maana,
Kumcha bwana ni chanzo cha maarifa, bali wapumbavu hudharau hekima na adabu
Mithali 1:7.

Paper
imagine na yale mauchafu marefu anatawaza vipi huko?