Jamani wanaume heshimuni sana wake zenu

Huwa nawashangaa sana nyie wanaume kila mnapokuwa na vidumu sababu zinakuwa za mwanamke inamana nyie mmkekamilika kwa 100% mbona wenzenu wanatulizana.
Nadhani ni hulka zenu tu na hamjajizowesha kutulia kwenye ndoa zenu.Inatakiwa mfikie kipindi na nyie wanaume mtambue thamani na umuhimu wa wake zenu na sio kuwadhalilisha. Lait angejua thamani ya mke wake asingefikia hadi anamvua nguo
 
Mimi nafikiri alipigwa kwa sababu alipiga! !
Alidhalilishwa kwa sababu alimdhalilisha tena mwanamke mwenzie. Maana alijiona yeye ndio polisi na kila kitu. Labda nikukumbushe kitu " usitende unyama ili ulipwe pepo, migogoro inataratibu zake kuitatua, zifuateni bila shurti, wala sheria haitokuhurumia kwa kuwa yule alikuwa mumeo kama pale mumeo alivyoshindwa kukuvulia kwa kitendo cha kushambulia kwa kuwa ni mkewe. Jitafakari !!!
 
Michepuko ndio inajua thamani ya mume wa mtu ila mke wa ndoa hujui thamani ya mumeo.
 
Nivibaya sana mwanaume kumpiga nakumdhalilisha mwanamke yoyote yule ila pia nivibaya sana kwa mwanamke kumletea jeur mwanaume.Kwajins ninavyowafaham wanawake weng walivyo na mdomo nadhan uyo mwanamke yeye mwenyewe ndo chanzo chakupigwa maana niwanaume wachache sana wanaweza kuvumilia kero za maneno ya wanawake zao hasa kwenye tukio kama ilo.Ata ivyo dunia ya leo wanawake wengi wanadhalilika kwasababu hawajiheshim,hawajithamin nawanataka kupambana na wanaume au kua sawa na mwanaume kitu ambacho hakiwezekani maana nature ndo ilivyoamua ivyo.Kwaiyo wanawake wasifanye jeur kwakutegemea huruma kwasababu eti wanabeba ujauzito au kuzaa kwa uchungu namengine ya jinsi iyo maana ayo nimatakwa ya nature.Ila kitakachomfanya mwanamke aishi akiwa na thaman ni heshima na unyenyekevu.Swala la mwanaume kua na mchepuko ilo sio swala lakukufanya utumie nguvu maana mwisho wa siku atakae umia ni mwanamke.Pole sana mama uliyepigwa ila naamin atakua kajifunza kitu.
 
Bahati mbaya laana zako kwa wanaume hazitawafikia

Sifurahishwi na wanaume wenzangu wanaopiga wake zao .

Ila msitafute ujiko kupitia wanaume

Mtuache
 
Mara nyingi ni hivyo..mfano kwetu ndugu zako wakimkuta mumeo kwa kibajaji wala hawana neno naye ila wananeno na wewe.utajieleza mbele ya shangazi na bibi kama ulisikiliza walichokuelekeza au ulienda fanya yako,wanaume ni watoto wakubwa ujue hawana ujanja ki viiiile tunawakweza tu.
 
Mimi nilifikiri mumewe anafanya umalaya kumbe anafatilia kadada kamoja tu ? Hapa shida iko wapi ?

Labda mkewe kuna vitu anamiss jamani michepuko inajua kuteka wame zawatu nyie acheni tu
 

Mwisho wa siku atarudi na maradhi sijui utusemaje na hukumkemea
 
Bahati mbaya laana zako kwa wanaume hazitawafikia

Sifurahishwi na wanaume wenzangu wanaopiga wake zao .

Ila msitafute ujiko kupitia wanaume

Mtuache

Sa Ujiko gani sasa nawewe nawee!!???!!?!
 
Nikimuangalia mnmke mwnzngu ambae hajaolewa nakuta ana raha ya maisha kuliko hat mim nilieolewa... Hakuna tunachoenjoy zaid tunatunza watoto wetu tu wakue. Mungu tubariki wanawake
 
Mume hulindwa kwa maombi ya mkewe.
Kumlinda kwa kumfuatilia physically mshahara wake ndo huo.
Siungi mkono alichokifanya huyo mume lkn siungi mkono 'ulinzi' wa huyo mke kwa mumewe
 
Mwisho wa siku atarudi na maradhi sijui utusemaje na hukumkemea
Ikiwa huyo mwanamke mpaka kafikia hatua anavuliwa nguo kisa fumanizi sidhani kama hakuwahi kumkemea hizo tabia za ajabu ajabu , pia zinapozidi ni bora zaidi kuangalia mambo mengine ya msingi.
Mana hakuna haja ya kuongea jambo hilohilo kila siku bila mafanikio ni bora kukaa kimya ila akili kichwani.Mpaka huyo mwanaume anadiriki kuwa na michepuko sio kwamba hajui kuna maradhi bali ni hulka mbovu hivyo ukishindana na kumpa nasaa kila siku itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…