Jamani wadau naomba ushauri wenu

Jamani wadau naomba ushauri wenu

kapelevele

New Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
4
Reaction score
0
Nimebahatika kuwa na mke pamoja na watoto wawili, na sisi wote mimi na mke wangu wazazi wetu wapo hapa Dar es salaam nasi twaishi hapa. Chakushangaza kila siku za sikuku mke wangu hupenda kwenda kujumuika chakula na wazazi wake na wakati mwingine hupenda kuchukua watoto na msichana wa kazi wakiambatana kwenda kwa wazazi wake, nimeshamshauri vya kutosha kwamba aandae chakula ili nao ( wazazi ) waalikwe hapa kwangu naona imekuwa ngumu kwake.....wadau manaonaje suala hilo, maana hata hivi sasa mimi nipo nyumbani na wanangu, maana ikabidi tule sehemu baada ya kutoka church.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom