Jamani Wa mjini tunalia hivi je wa Kijijini wanalia kilio gani???Serikali hiko wapi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani Wa mjini tunalia hivi je wa Kijijini wanalia kilio gani???Serikali hiko wapi??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaKiiza, Feb 19, 2011.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Mimi nimeshikwa na Butwaa!!!Mimi sijui kama nipo Tanzania Nchi yenye Serikali!au Nipo Somalia??Nchi inayojiendeshea kienyejikila kukicha!!Aiingii akilini kama kweli Nchi hii yenye utawala tena unaitwa utawala bora!!au ni Bora Utawala??Nijuzeni mbona nchi inamong'onyoka??watu mpo mmekaa maofisini hivi mpo kwa ajili ya wananchi???au vinginevyo??

  #Naanza na kupanda kwa bei ya vyakula je hili nijukumu la nani??hakuna idara ya kuregulate mfumko wa bei??kweli mnaacha sukari inayotengenezwa hapa nchini inafikia bei ya Sh 2000!!kwa kilo??imeshakuwa anasa!!

  #Mchele umefikia Sh1500-1850!Kweli mnataka sisi tulechenga za Shs 1000??Mchele wa vitumbua ļKweli Serikali mpo??Mimi siamini Najiuliza maswali sipati jibu je Wapwa zangu waliopo kule Kyamlaile,Kijuka,Minziro,Kakunyu,Mrongo,Buenda ngabo,Kigoma kule Kibondo,Kasulu,Nakwingineko kwingi hata kwa Mtoto wa Mkulima Kakaa kimya!!Nakukataa kwake VX hakujaleta tija ni bora angelichukua!!

  #Mbona Bei ya petrol ikipanda kidogo Wehura!!Sorry EWURA wana andamana??Kweli ni serikali iliyochaguliwa na wananchi kwa aslimia 70???Imewasahau wananchi wake??Viongozi mlioko madarakani tupieni macho kwa hili ni adhabu kwa mkulima na yule mwenye kipato cha chini japo anaweza kuwa mwajiliwa tusingoje maandamano!!

  #Wanachi wanapata taabu jaribu kuwaonea huruma SUKARI KUFIKIA SH 2000/NIKITANZI.
   
 2. Tidito L

  Tidito L Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Du! Bro unamawazo sana ata mi nalifiliaga hilo,cpati jibu.
  Wapo tu kuongezea vitambi maofisini hmn llt.
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana kwakuwa ukiangalia kiwango cha kufeli mitihani ya kidato cha 12 kwakuwa umasikini umeingia kwenye wananchi waliowengi na hawana uwezo wa twisheni ndiyo maana kiwango cha kufeli kimeongezeka!Na sababu kuu ni kuongezeka kwa gharama za maisha!!Hatuna serikali inayojali wananchi!Wanajali wananchi kwenye majukwaa na vipaza sauti!
   
 4. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sukari inazalishwa TZ, lakini umejiuliza mmiliki wa kiwanda ni nani? Vile vile wamiliki wa kampuni zinazoagiza vyakula kutoka nje? Kwa hiyo usishangae kuwa bei za vyakula zinapanda na serikali haiingilii kati. Kuna mtu alishachukuwa kamisheni yake, na bado viongozi wetu wanawanyemelea hao hao wenye viwanda na waagizaji kuwaomba "vijirushwa na vifadhila vidogo vidogo". Tena hapo mwananchi mwache afe, Watanzania tunazaa sana, watazaliwa wengine. Na kila ikiwa hawana afya wala elimu ni bora kwa viongozi wetu (Bora viongozi), kwani ni rahisi kwao kutawala vibonde, ndondocha na wagoigoi. Kilo ya sembe, fulana na kanga moja wakati wa uchaguzi inatosha kumrubuni mtu wa aina hii kila baada ya miaka mitano. Sisi wa kufa tu.
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Mimi nasikia machungu sana hivi ulishawahi kujiuliza SUPERDOLL Ndiye mmiliki waviwanda vikubwa vya sukari nchini??Kagera na morogoro???na mbia wake nimiongoni wa Viongozi mafisadi wakuu wa awamu ya tatu??Je unategemea nini??Na sukari nyingi wanapeleka nje wakati nchi ina uhaba wa sukari!!Hapohapo serikali inaagiza sukari Brasil nivichekesho!!
   
Loading...