Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 12,105
- 35,136
Jamani upweke unauma sana endelea kusikia mwenzako anasema ila usikufike.Tatizo hili la upweke limekuwa kwa watu waaina mbali mbali ikiwemo wanawake na wanaume.
Chanzo ni kufiwa au kukosa wenza.Upweke umefanya watu kuishi na ukiwa pia kukosa furaha na wakati mwingine kuwa na msongo wa mawazo hata magonjwa na matokeo yake maisha kuwa mafupi yani kufa mapema.
Mara nyingine watu ambao ni wapweke yaani wanawake ambao hawajaolewa wamekuwa wakidharauliwa na jamii na kuitwa majina ya ajabu na kuwafanya wakose furaha.
Hata hivyo pia watu wamekuwa wakidhani walipendaa kuwa na hali hiyo au kasoro fulani kumbe ni mipango ya Mungu. Kwani naamini hakuna mwanamke ambaye amekuwa akipenda asiolewe ila hutokea.
Karibuni tujadili hili swala la upweke