Jamani uhamiaji wako wapi Geita

Hobic11ac

Member
Apr 7, 2012
29
7
Ndg wanajf nakerwa na kuhuzunishwa jinsi gani idara ya uhamiaji Geita hawako makini. Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kila kukicha unaajiri wafanyakazi kutoka nje hasa kutoka ufilipino, ktk kampuni moja (contractor) inayojihusisha na drilling ina jumla ya wafanyakazi 213 kati ya hao wafilipino ni 47 yaani hata mlinzi wa lango la kuingia kwenye kampuni hiyo ni mfilipino, kali kuliko zote wameleta drivers 2 na punchman 1.

Je hizo nafasi hamna watanzania wenye sifa? Nina imani kabla kuingia nchini wamepitia taratibu immigration je wamewambia kuwa wao ni nani?
 
Hili linchi mimi linanitia kichefu chefu ile mbaya.....sasa mpaka mlinzi wa getini atoke nje ya nchi?Najua pia huko migodini kuna wahandisi kutoka nje Ghana sijui Zambia afu kazi kubwa wanayoifanya ni kutumia spreadsheet tu hawajui lolote la maana at the same time tuna wabongo ni wahandisi pia na hizo kazi wanaziweza ila wamekalia benchi kitaa kazi hakuna....WTF!Ni sera za nchi yenu tu mkuu,mabadiliko yanahitajika.:disapointed:
 
uhamiaji wa nchi gani? Tz? Sahau hata wakija wanaweza kukatiwa cha juu wakasepa.....
 
Kiukweli inakera sana.Takwimu za kukosa ajira zikiwa juu lakini bado wageni waajiriwa kwenye kazi ambazo zinzwataalamu nchini.Hapa napata mashaka kuna viongozi wana mikono yao kwenye hizi ajira.
 
Mkuu hawa wageni wakiombewa vibali vya kufanya kazi tz, wanaombewa kwa kutumia majina hewa yasiyokuwepo, kwa mfano mlinzi watamuita ni "security systems specialist". Inaonekana ni taaluma ya kutisha na yenye kuhitaji ujuuzi wa hali ya juu, lakini ukienda kazini unamkuta anafungua mageti.
 
Mbona kwenye Migodi ya Bariki safishasafisha imepita, maana hapo Tulawaka wengi waliondoshwa
 
Wewe mi si juzi nililaumu sana humu ndani nikaishia kuambiwa kuwa waTanzania hawapati ajira eti kwa sbb ni wavivu na wana exchuzi nyingi sana kazini.But nachokuambia hatuna jinsi maana system yetu iko corrupt sana so acha tuendelee kuumia mpaka mwisho tutakapozinduka usingizini na kukuta hata mkurugenzi wa wilaya ni Kaburu kutoka south Africa ambae qualification zake akizipeleka kwao hata kazi ya kufagia barabara hapati.Mimi sioni shida tena na wala sitapiga mayowe maana wewe jiulize hao watu wanapewa permit ya kufanya kazi humu nchini na nani?Mwisho wa siku utagundua kuwa system yetu haipo makini hata kidogo.Mtu anakuja na passport ya tourist but sisi wenyewe ndo tunamsaidia kumkatia parmit na baadae anatuona sie wachumia tumbo tu basi.
 
Hayo malalamiko yako yapeleke ngazi ya taifa. yote yamepita kwa msaada wa vigogo wa ngazi ya taifa.. uhamiaji geita wanapokea tu maelekezo ya kuwahalalisha na kuwalinda kutoka juu
 
Back
Top Bottom