Jamani tulipeni fadhila

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
3,421
3,391
Mimi sijui nina moyo gani au sijui binaadamu wote tuna moyo huu,Mimi mwenzenu mpaka sasa Nina miaka34 ila ninakumbukumbu ambazo zinanifanya nakuwa ka chizi,hamuezi amini mnakumbuka wakati tunasoma au udogoni kuna wale watu ambao ukikutana nao wanakupa hela ya shule?ukimuamkia tu utaona anazama mfukukoni na kukutoa,Mimi nawakumbuka3,Sema sasa wameshakuwa watu wazima sana,wingine wamekufa ,mmoja nilimtafutaka nikampata nikawa natabia ya kumtoa maana umri umeenda na hana kitu,na nilikuwa najisikia furaha sana nikimpa hela ,Ila juzi nimeenda nikaambiwa ameshafariki,dah alikuwa MTU mzuri sana,we kaa utulie vuta kumbukumbu vizuri huezi kosa watu hao,mmoja alifariki kabla sijaanza kushika hela daa Michael, mungu akuweke mahali pema huko uliko,pamoja na kazi ngumu alizokuwa anafanya,ila alitokea kunipenda sana na alikuwa ananitoa kinoma,sasa kuna mmoja huyu nasikia yupo nilimtafuta sana,japo nimuone niongee nae najua ,nikishamaliza kuongea nae atawasimulia watu wengine,nao huenda wakaiga moyo wake,mungu bariki wale woote wenye moyo safi,moyo Wa kugawana wapatacho na wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vizuri pia kuwakumbuka walimu waliokusaidia wakati uko Shule ya Msingi na Sekondari maana wana kazi kubwa walifanya hadi umefika hapo ulipo sasa
 
Back
Top Bottom