Jamani tujadiliane na hili la personal space

pinkmousse

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
227
88
za jumapili ndugu zangu! naomba tusaidiane mawazo katika hili,ninapenda sana kukaa peke yangu ninapokuwa home, yani napenda personal space yangu,kwa sababu kazini nakutana na watu wengi, napenda kutoka na marafiki ila nyumbani napenda space yangu, mara nyingi nyumbani ninakuwa na watoto wangu, baba yao na dada,wageni napenda ila si wa kulala, napenda waje kusalimia tena kwa taarifa halafu basi waende, na mimi sipendi kulala kwa watu kabisa eti zile za kwenda kutembea wiki mbili kwa watu na kulala siwezi kabisa kwa sababu naona space yangu inakuwa finyu. Kwa mfano kuna watu hawawezi kabisa kukaa peke yao nafahamu ndivyo jinsi walivyo na sina tatizo nalo,je kuna wenzangu mpo tunaoshare hii tabia ya kupenda kukaa pekee nyumbani, au ya kupenda space binafsi? tujadiliane tafadhali,endeleeni kufurahia jumapili
 
ok,swala la extended family nalielewa kwa sababu nilivyolelewa wazazi wangu walilea ndugu wengi ilifika point mnajikuta mko kama ishirini ndani ya nyumba, yani unakuwa huna muda wako mwenyewe ila kwa sasa siwezi tena napenda space yangu
 
Personal space kwangu ina season...ila sio mpenz wa hiyo life style kabisaa..i like socializing bigtime!!
 
Uko difference from a huge groups of peoples, several tmys hua tunasikia watu wengi wanalaani a lonely place ! Wengi wanapenda wageni tena wa kumbonji (kulala) na siku wakiondoka ni vilio! (sitanii) na wanaondoga na mizawadi lukuki.
Sasa Shost wewe uko abnormal! So far am not sure properly if that it's good habit! Shortly nisikumung'unyie maneno sitokutendea haki nikakuvalia marsk au miwani ya mbao niache kukupa nionavyo mie ukweli wa hilo, ni TABIA MBAYA even though kwako ni nzuri by the way maadamu ume'demand comments Jf basi tegemea kupata + pos & - Neg comments.
Jumapili njema tutakutana tena majukwaani.
 
nimekuelewa, nasocialize ila nje ya nyumbani au kama wageni waje kushinda halafu basi,issue ya kulala zaidi ya wiki wiki mbili ndio inakuwa issue
 
asante, nimependa hiyo abnormal ndio maana nikataka tujadili, negative comments ni nzuri zinapanua mawazo na mitazamo ya mambo mengi,sio kwamba sijichanganyi na watu ila nikiwa home napenda kuwa mwenyewe au kama ni wageni wawe wa muda mfupi
 
Pinkmousse hauko peke yako; l love my space pia. Yaani mimi nafikiri nimezidi; sometimes napenda niwe peke yangu the whole house. Mfano mzuri, leo nimetimua my sonushka na mdada wa kazi ili atleast nipate 4 hrs of myself.
Living room nina sofa langu la uvivu ambalo sipendi nimkute mtu amelikalia; ninapata shida sana wakija wageni na kukakia that sofa of mine.
 
daaah natamani nikupe zawadi!! viatu vyetu vinafanana kabisaaaa, kwa sababu nikikosa personal space ninapata stress isiyoelezeka,kula happy na sunday yako
 
Me binafs siku tano za wiki nakuwa busy sana na siku mbili ni za mapumziko, siku moja naitumia kusocialize na marafiki na ndugu na mitoko ya hapa na pale na siku ya pili huwa ni napenda kuwa peke yangu nisome vitabu na kufanya ibada pamoja na kutumia muda mwingi kutafakari maisha yangu
 
Personal space ni muhimu sana. Mimi hata nyumbani kwangu bado kuna wakati nataka niwe peke yangu (bila mume au watoto). Kweli sio rahisi kwa watu kukuelewa ila you have to be yourself. Character is more important than reputation because character is what you are whereas reputation is merely what people think you are... Be yourself.
 
nimekuelewa, nasocialize ila nje ya nyumbani au kama wageni waje kushinda halafu basi,issue ya kulala zaidi ya wiki wiki mbili ndio inakuwa issue

Ofcos msongamano usio na kichwa wala miguu katika nyumba unaboa kwakweli..kwa mfano unakaa mwenge kisha ndugu yako anatokea kinondoni tu hapo lakin anakuja kukusalimia wiki nzima..hiyo inakera indeed! Unakuwa hauna uhuru na baadhi ya mambo yako japo upo kwako....Ila mi huwa personal space kwakweli labda somwhere at the beach lakin katika nyumba..tena nyumba nzima peke yangu,siwezi..very rare nahitaji muda kama huo especially nikiwa na hasira..thats it....
 
daaah natamani nikupe zawadi!! viatu vyetu vinafanana kabisaaaa, kwa sababu nikikosa personal space ninapata stress isiyoelezeka,kula happy na sunday yako

Thanks Pink; yaani nimepumzika, reflect, kaa with minimal cloths na nimepika supper tayari. Kesho nitaamka na nguvu na nitakuwa so jolly ufisini mpaka basi!

Ni katherapy fulani hivi!
 
@judgement
uswahilini tungemwambia ni mchoyo au ana gubu

Nilivyomaliza fomfoo nilikaa tandika uswazi kabisa kwenye vyumba vya uwani na sis wangu; nilikuwa natika nje jioni baada ya Sis kutoka job. Niitwa majina yote hayo; ni maumbile tu!
 
Kati ya siku zinazokuwa ndefu kwangu ni siku ambazo nipo peke yangu. Kifupi siwezi halafu sipendi.
 
hahaahhaaa..kashakwambia anapenda kukaa peke yake..halafu wewe unataka kushare tena hako space??!!

mimi sitamsumbua,all i willl do ni kumfanya awe as comfortable as possible,halafu kimya kimya!
 
Back
Top Bottom