Jamani Tanga kuna nini lakini?

Quinton Canosa

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
1,220
1,225
Habari zenu wana jamii forum
Kwa muda sasa nimesikia sifa za huu mkoa wa Tanga kuhusu mapenzi.Watu wanasema mapenzi ndiko yalikozaliwa,na kuna stori nyingi sana kuhusu mji wa Tanga mara maji ya kuoga yanawekwa sijui karafuu,pilipili hoho,mara mdalasini.Vile vile wanasema wanawake waliotokea mkoa wa Tanga wanayajua mapenzi kuliko wanawake wa mkoa mwingine wowote na stori nyingine nyingi sana kuhusu huko Tanga ila mimi nimepita tu sijawahi kuishi huko ambako wanasema mwanaume unaweza ukaenda na usirudi,na kama una pesa ukirudi kwenu unakuwa mikono mitupu kwa mapenzi ya moto.Nimeandika hivi sababu jirani yangu alikwenda na gari yake aina ya fuso yake huko amerudi mikono mitupu ukimuuliza gari iko wapi hana sababu ya msingi,na amekuja kuuza kiwanja anataka arudi tena huko.Sasa jamani Tanga kunani huko na hayo mapenzi wamefunzwa na nani?
 
case study unayo si umuulize huyo jamaa yako?
k ni zile zile kuna jama nasikia alikuwa na mabasi yake katembea na wanawake makabila yote kaandika mabasi yake zafanana maana hakuona jipya
 
Naogopa aisee

uisiogope. unaenda kufanya utafiti kwa vitendo.
nasikia kuna kibao "KARIBU MKOA WA TANGÄ" unapoingia ila hakuna kibao "KWA HERI MKOA WA TANGA"unapotoka mkoani humo. Eti hawajaweka kwa sababu wanaoingia hawaotoki.
 
Hizo ni stori za zamani sana kabla ya azimio la Arusha siku hizi kila mtu anajua kila kitu!
 
Mapenzi huku ndo sifa yetu kubwa,ila kwa sasa tuache kwanza tunafikiria msiba uliotupata kwa timu zetu zote kushuka kitu ambacho hakijawahi kutokea dunian,tumeandika historia hapa.
 
Uliyoyasema yote ni kweli, Tanga waja leo kurudi majaliwa..

Kuna jamaa yangu mmoja wa kanda flani hivi mpaka leo mwaka wa nane hata kwako kagoma kurudi ndugu zake walimfata akakataa...anamtoto mmoja matata sana...

Anaishi mitaa ya home pale Nguvumali.
 
Back
Top Bottom