Jamani Rorya na hatima yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani Rorya na hatima yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JACADUOGO2., Jun 7, 2011.

 1. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha, inashangaza, inahuzunisha na kutia huruma katika nchi ambayo inadaiwa kuwa ni ya kidemokrasia kama Tanzania kufanya mambo ya aibu chini ya uongozi wa CCM bila ya kiongozi wa taifa la Jamhuri ya Muungano rais Jakaya Mrisho Kikwete kukemea! Kwa kweli inasikitisha na inapunguza imani ya wananchi kwa viongozi wao na suala la ufisadi linazidi kudhihirika wazi miongoni mwa viongozi wetu. Tunawaomba mtambue wazi kuwa watanzania tuna akili timamu na tunatambua kila kitu ndani ya taifa hili. Sisi ni watanzania tunatambua wakati uliopita, tunatambua wakati uliopo na tunatazama kwa upeo wa juu wakati ujao. Ifike mahali viongozi wajue umuhimu wa utu wa watanzania au wananchi wao kwa ujumla wake. (Leaders must know the importance of the Tanzanians’ dignity).

  RORYA ni miongoni mwa majimbo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayosifka kwa mambo mazuri mengi pamoja na mambo mengine mabaya machache kama ilivyoada. RORYA ikiwa ni miongoni mwa majimbo machache yenye maliasili nyingi ikiwa ni pamoja na ziwa Victoria, madini (maeneo ya Kamot karibu na mlima Rorya) na nyingine nyingi. Pamoja na hayo yote RORYA ni miongoni mwa majimbo yaliyo nyuma sana kimaendeleo kwani barabara za jimbo la RORYA hazina kiwango chochote kizuri ikiwa ni pamoja na ukosefu wa lami kwani ndani ya jimbo zima la RORYA hamna barabara ya lami. Ni aibu!!

  Mbaya zaidi kuliko yote ni kwamba RORYA inatawaliwa kimabavu, kwa maslahi ya watu wachache (LAMECK AIRO na CHARLES OCHELE) na bila kujali maslahi ya wanarorya. Hii Ni aibu, Ni fedhea, Ni dharau, Ni ujuha, Ni uroho na ni ukosefu wa hekima na busara katika uongozi.

  Ni dharau pale ambapo maamuzi ya jimbo la RORYA yanapofanywa na kutawaliwa na mfanyabiasha LAMECK AIRO ambaye amesababisha migogoro mingi na uhasama miongoni mwa Wanarorya kuanzia kipindi alipokuwa diwani wa kata ya Koryo hasa katika harakati ya kutangaza makao makuu ya wilaya ya RORYA ambapo alidiriki kutoa rushwa na kubadilisha sehemu ambapo ilitakiwa iwe ni makao makuu ya wilaya ya RORYA yaani makao makuu kutoka SHIRATI na kwenda kuwekwa porini (Ingri juu) pasipo na kigezo chochote cha ubora katika eneo hilo la Ingri juu tofauti na SHIRATI iliyokuwa na kila kigezo ikiwa ni pamoja na maji (ziwa Victoria), umeme na hata barabara zinazopitika tofauti na Ingri juu ambapo kila kitu kinaanza mwanzo na fedha nyingi kutumika katika ujenzi bila tija wala sababu ya msingi.

  Vile vile ni chini ya uwenyekiti wa CHARLES OCHELE wa halmashauri ya wilaya ya RORYA (2005 – 2010) na ushauri wa rafiki yake wa karibu LAMECK AIRO iliyopelekea halmashauri ya RORYA kupata hati chafu kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

  Hii yote ni shauri ya LAMECK AIRO kukosa elimu, upeo na mtazamo wowote katika fani yoyote katika maisha kwani ni darasa la saba na hajui maana ya elimu kwani katika kampeni zake alidiriki katamka katika kampeni ya kuomba kura ya maoni kuwa “ ELIMU NI KELELE” alipoulizwa kuhusu umuhimu wa elimu kwake.

  Katika harakati za kuwania nafasi ya uwenyekiti wa halmashauri ya wilaya RORYA (2010 – 2015) miongoni mwa wana CCM waliochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo walikuwa madiwani watano ikiwa ni pamoja na Yamo Odemba Kagose kata ya Rabuor, Ongujo Wakibar kata ya Mkoma, Okeya Ogigo kata ya Nyamtinga, Lukio Ambogo kata ya Nyahongo na Charles Ochele kata ya Roche. Majina hayo yalichujwa hadi makao makuu CCM kama ilivyo kawaida ili kupata majina mawili yatakayopigiwa kura na madiwani wa CCM RORYA ili kupata jina moja litakalopambanishwa na mpinzani. Hata hivyo majina mawili yaliyotoka taifani yalikuwa ni ya Okeya Ogigo kata ya Nyamtinga na Lukio Ambogo kata ya Nyahongo, lakini cha kushangaza ni pale ambapo LAMECK AIRO (Mbunge) alipotoa tamko kwamba yuko tayari kujiuzulu ubunge kutokana na sababu kwamba jina la Ochele halimo miongoni mwa yale majina mawili yaliyotoka taifani na kwamba atarudisha kadi ya CCM na kuwa mwanachama wa kawaida wa CCM. Aibu kwa mbunge wa RORYA, Lameck Airo! Utarudishaje kadi ya chama halafu uwe mwanachama wa kawaida? Ajabu!

  Kimsingi mbunge huyu hajui kwamba ukisharudisha kadi ya chama huwezi tena kuwa mwanachama wa kawaida na huwezi kuwa mwanachama wa chama hicho. Je, wananchi wa kawaida ambao wengi wao hata hawajui maana ya uanachama, wao wangesemaje? Na kwa nini ajiuzulu ubunge na kurudisha kadi kama hamna jina la Ochele? Kwani Ochele ni nani na ana nini? Kwani Lameck ni nani na ana nini akijiuzulu? Kwani RORYA ni ya Lameck na Ochele?

  Cha kushangaza zaidi na kusikitisha zaidi na hili ni kwa taifa zima, ni pale ambapo katika mazingira ya kutatanisha na kufedhesha taifa la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni pale ambapo bila kutarajia jina CHARLES OCHELE lilipokuja tena kuonekana kwamba ni miongoni mwa wanaoenda kupigiwa kura na madiwani wa CCM kuwania nafasi ya uwenyekiti wa halmashauri ya wilaya RORYA wakati majina yaliyotoka taifani jina lake halikuwepo. Hii ikiwa ni pamoja na msimamo wa LAMECK AIRO kuwa jina la Ochele lisipopitishwa anajiuzulu ubunge na kurudisha kadi ya CCM. Swali ni kwamba kwa nini kama jina la Ochele lilishatolewa na kamati kuu kwa nini jina hilo lirudishwe tena na kamati kuu?

  ü Kama siyo rushwa na ufisadi ni nini?
  ü Kama siyo ukosefu wa uelewa ni nini?
  ü Kama siyo kudharau wanarorya ni nini?
  ü Kama siyo utawala wa kimabavu ni nini?
  ü Kama siyo kupora watu haki yao ni nini?
  ü Kama siyo madharau ni nini?
  ü Je, kiongozi mkuu wa nchi anasemaje kuhusu haya mazingira ya kifisadi?

  Naamini kwamba kila anayefuatilia vyombo vya habari hapa nchini Tanzania anajua wazi madhara ya hayo matukio yaliyotokea RORYA na yaliyosababishwa na LAMECK AIRO. Ikiwa ni pamoja na baadhi ya madiwani wa CCM RORYA kujiuzulu ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM wilaya ndugu, Leonard Yoda. Miongoni mwa madiwani watatu wa jimbo la RORYA waliojiuzulu ni Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma, Lukio Ambogo wa kata ya Nyahongo na Okeya Ogigo wa kata ya Nyamtinga. Wanarorya tunasema Lameck hana sifa yoyote ya kuwa mbunge wa RORYA.

  LAMECK AIRO ni miongoni mwa wagombea ubunge waliotumia hela nyingi sana katika kampeni zake kwani hakuwa na uwezo wowote wa kujinadi wala hakuwa na sera, hivyo aliamua kutumia pesa (Rushwa) katika kampeni hadi alipofanikiwa kuwarubuni wananchi na kupata kura za kuchakachuliwa. Alijitahidi kutuma vibaraka wake katika baadhi ya kata za RORYA ili kuwania udiwani lakini kwa bahati mbaya kwake na kwa hao vibaraka wake na bahati nzuri kwetu hao vibaraka wake walishindwa kuhimili mikikimikiki na hatimaye walibwagwa chini. Miongoni mwa hao vibaraka ni pamoja na aliyemuweka kugombea udiwani katika kata ya TAI, ndugu, LAZARO ROJA AKUKU aliyemjengea nyumba na kupewa gari na pesa nyingi zilizotumika kuhonga wapiga kura ndani ya kipindi cha kampeni. Mwingine ni TOPA aliyegombea katika kata ya BUKURA aliyepewa pikipiki na hela. Wote walibwagwa!

  Tunawashauri Wanarorya kuwa na tabia ya kusikiliza hoja na sera za wagombea na kuwauliza maswali juu ya mustakabali wa RORYA na Tanzania kwa ujumla, hasa kuwahoji wababaishaji wa sera kama AIRO. Waache tabia ya kumchagua mtu kwa sababu ya pesa zake na kuachana kabisa na ile tabia ya “GONYA” (nifungue). Wajiulize kwamba huo mlungula wanaopewa umetoka wapi na mtoaji (AIRO) ataurudishaje? Wanarorya tubadilike, tuachane na ukale, ukanda na tujali maendeleo ya RORYA

  Madhara ya LAMECK AIRO kwa Wanarorya:
  1. RORYA kupata hati chafu kwa zaidi ya miaka miwili.
  2. Makao makuu kuwa porini(Ingri juu) badala ya Shirati.
  3. Madiwani waliochaguliwa na wananchi kujiuzulu kwa sababu yake.
  4. Kutotambua umuhimu wa elimu kwa kusema kwamba “elimu ni kelele”
  5. Kutoa rushwa ili Ochele awe mwenyekiti wa halmashauri.

  Hata hivyo ieleweke kuwa RORYA ni ya Wanarorya na siyo mali ya mtu binafsi kuitumia kama mradi binafsi. Hivyo tunataka mabadiliko ya haraka sana.
  .
  NB:
  Tunaomba kujua kuwa uchaguzi katika zile kata tatu (3) zilizoachwa wazi utafanyika lini? Wananchi tumechoka kusubiri kuanzia DECEMBER 2010 mpaka leo!!!!! Jamani RORYA.

  JACADUOGO
  WUOD RORYA
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu wana Rorya mnalo la kuwaambia watanzania kwa kina kabla ya malalako haya. Rorya ni wilaya yenye wasomi na vijana wengi wenye uelewa mkubwa sana tu wa mambo lakini Ochele na huyo Lamerk mliowapa madaraka na mamlaka makubwa ya kuwafanyia maamuzi wote ni darasa la saba.! Kuna nini nyuma ya hili??
   
 3. T

  Thesi JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jacaduogo2 umesema ukweli kabisa. Mimi napata machungu kweli mambo yanavopelekeshwa Rorya na hawa vihiyo wawili LA na OChl. Hawa wamekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya Rorya. Haya yote yanashabikiwa na chama cha magamba kilichokumbatia wafanyabiashara na wezi bila kujali athari zake kwa wananchi na maendeleo.

  Ni AIBU kubwa kwa serikali iliyoko madarakani kupeleka makao makuu ya wilaya ya Rorya Ingri juu porini pasipokuwepo miundombinu yoyote au kuwa sehemu ambayo ni economic strategic point kisa eti Lameck na Prof Bangi mmoja kutaka nyumbani kwao kuwa makao makuu ya wilaya. Ni aibu ni aibu rais kufungua makao makuu ya wilaya sehemu kama ile kwa kuangalia maslahi ya kisiasa na urafiki na mafisadi wanaotaka maslahi yao kama haya. Hapa nikifikika unapata jibu kwanini Rais wetu alitamka hajui kwanini nchi yetu ni maskini.

  Utachezeaje maslahi ya wananchi laki 2 kwa kutaka kuwafurahisha wafanyabiashara wa2 ili wawaunge mkono kwenye chama chenu? Huu ni ufisadi wa kifikra. Sasa kama Rais na waziri mkuu wanakubali upuuzi kama huu unategemea wanafanya miupuuzi mingapi inayorudisha nchi yetu nyuma? Eti wanapeleka makao makuu ya wilaya Karibu na Utegi kwao Lameck, Ochele na Prof Bangi huyo pasipo kuangalia sehemu ambako panastahili kuwa makao makuu ya wilaya.

  Wanarorya wamewekeza Shirati na ndio mji wao siku zote pakiwa na miundombinu, umeme, kiwanja cha ndege, hospitali nk Rais anakubali vipi upuuzi kama huu kuhamisha makao makuu kwa ushawishi wa mbunge na mwenyekiti wa halmashauri darasa la saba? Wanarorya suluhisho pekee hapa ni kuipiga chini chama cha CCM na tunawaomba watanzania wanaoipenda nchi yetu watuunge mkono kuangusha huu utawala wa kipuuzi wa CCM.

  Kije chama kingine kiweke mgombea mzalendo na mwenye uelewa wa mambo balada ya ubinafsi wa kipuuzi wa kutaka makao makuu ya wilaya kuwa nyumbani kwao mbunge wa CCM kihiyo kwa hasara ya wilaya nzima.na kichukue serikali. Ingri juu bora pabaki magofu. Bora hasara ya 1bil TSH serikali itakayopata kuliko hundred bilions tutakazopata miaka nenda rudi kwa kuweka makao makuu Ingri juu.
   
 4. T

  Thesi JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Macondo tatizo la Rorya kukubali kuwachagua CCM ni ujinga wa wananchi wengi wilaya hiyo. CCM imekuwa ikitumia ushawishi wa rushwa kuwarubuni wananchi lakini pia tunatilia shaka kuwa wimbi la mabadiliko lililoletwa na Dr Slaa 2010 halikuacha nyuma wilaya ya jimbo la Rorya. Pamoja na kutumia mapesa mengi na kuhonga wananchi wengi hawakushawishika kumchagua Lameck.

  Inaamimika kuwa alichakachua kura kama walivofanya CCM kwenye majimbo mengi mwaka jana. Ukweli ni kuwa watu waliogopa kuwa hakuna atakayepambana na Lameck hivo wengi hawakuthubutu. Lakini matokeo yalionyesha tofauti kuwa angekuwepo mgombea imara jimbo hilo lilikuwa la CDM. Kumbuka wanaRorya ni kati ya majimbo ambayo walichagua wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995.

  Jimbo hili ni kati ya majimbo wanakotoka wafanyabiashara wakubwa wa kanda ya ziwa ambao kwa kutaka kulinda maslahi yao ya kibiashara wamekuwa wakitumia pesa kuhakikisha jimbo hilo liko mikononi mwao. Tatizo wafanyabiashara wote hao ni darasa la saba hivo uelewa wao pia ni mdogo kuchanganua mambo na mbinu za kuleta maendeleo.

  Wamewaaminisha wananchi kuwa ukiwa na pesa utaleta maendeleo kitu ambacho ni hatari make inatakiwa kuwepo na vyanzo nya kiuchumi vinavoendeshwa na wananchi kikamilifu badala ya kusubiri kuomba kwa mtu. Mbunge darasa la saba, mwenyekiti wa halmashauri darasa la saba unategemea nini kama si mauzauza ya hati chafu?

  Sasa tunawataka wazalendo wa Rorya sio vibaraka kama Maina Owino niliyemwona akiandika upuuzi wake hapa wajitokeze kulikomboa Rorya mikononi mwa mafisadi 2015. Na ikitokea tu kesi ya uchaguzi ikashinda kwenye jimbo hili na uchaguzi kurudiwa Lameck Airo atausoma ubunge make sasa CCM hawana lao tena kwenye jimbo hilo kwa wakati huu.
   
 5. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mpeni John Mashaka....jimbo hilo,si ametokea huko....?:glasses-nerdy:
   
 6. theophilius

  theophilius Senior Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mh! sina cha kuongeza!
   
 7. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  acheni majungu nyie wajaluo kwanza hao wasomi ndiyo wizi wakubwa, kwa miaka 50 ya uhuru wasomi ndiyo walikuwa viongozi wetu na hakuna maendeleo subirini miaka 5 ya huyo mbunge wenu harafu mlinganishe na miaka 10 ya professor mliyekuwa naye. MNA BORE!!
   
 8. T

  Thesi JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ukiangalia post zangu hapo juu huyo prof nimemwita prof Bangi kulingana na matendo yake. Yeye ndiye aliyewakuza na kuwalea hao vihiyo. Hao vihiyo ni zao la prof Bangi hivo ni wale wale. Tatizo hapa ni CCM inayolea uongozi mbovu kupitia viongozi wabovu. Ndio maana nimesema dawa ni kuing'oa CCM madarakani chama kingine kiingie lakini pia tunamtaka mbunge mzalendo anayezingatia maendeleo ya jimbo badala ya maslahi ya kifisadi. Haya sio majungu.

  Ni upuuzi mtupu kutumia kigezo dhaifu cha makao makuu kuwa katikati pasipokuangalia sababu muhimu ya uwezo wa sehemu hiyo kukua kiuchumi na kuwa kichocheo cha ukuaji kwa wilaya nzima. Makoa makuu panatakiwa pawe pale ambako ni "economic strategic point". Nani alikuambia Mwanza pako katikati ya mkoa wa Mwanza?

  Dar je, pako katikati? angalia hata miji mikuu ya nchi mbalimbali. Ni pale ambako wananchi wamewekeza kulingana na shughuli zao za kiuchumi ndiko serikali inatakiwa iongeze support vinginevo pamefanyika research kuhalalisha sehemu nyingine na sio kura za madiwani walioongwa na mafisadi kama Lameck kufanya kwao pawe makao makuu na Rais wa nchi kuja kubariki upuuzi huo.

  Bora nani fisadi au Msomi? Bora msomi asiyefisadi. Ila msomi akiwa fisadi pia hatumtaki. Tunataka wazalendo. Sasa mtu ni kihiyo ni fisadi kuna jema hapo? Tunataka wasomi wanaolewa mambo lakini wawe wamejitolea kushughulikia maendeleo ya wilaya. Hatutaki ufisadi wa wafanyabiashara wanaojiita G6 tena Rorya na chama chao cha magamba.
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Poleni, mlipaswa kuchagua wanamageuzi na kulinda kura zenu kwa gharama yoyote ile
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hawa watu 2 ni hatari sana huyu lameck si ndiyo alipewa tenda ya kushona gwanda za jeshi nchi nzima na prof Sarungu wakafanya ufisadi sana tunajua alafu bi mfanya biashara asiye lipa kodi pale Mwanza na huyu Ochere ni mvumvi wa samaki na anawanyanyasa sana wavuvi wadogo wadogo.

  Tunawajua sana na shule hawana kabisa km lameck wala ajaishia la saba ni la tatu pamoja na mwenzake hawa iko siku habari yao itakwisha na peter zakaria wa tarime wana jeuri sana na wamenyanyasa sana wananchi tunawajua sana mambo yao tunayajua na haya yote yameletwa na CCM
   
 11. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana-Rorya wenzangu mbona siwaelewi au ni matatizo binafsi. Zaidi ni malalamiko tuuu juu ya uamuzi wa wengi maana baada ya uchaguzi sikusikia mtu ameenda kupinga mahakamani, ambayo ndiyo nafasi ya msma kweli. Angalau hoja yenu hii ingeenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkashindwa tungewasamehe kwa malalamiko hayo.

  Tuonyeshe kwamba tumekwenda shule kwa kukubali taratibu na sheria za nchi na kwamba uchaguzi umekwisha sasa ni saa ya kujenga nchi. Ebu ona hakuna constructive ideas ni malalmiko tuuu na unsupported claims tuuuu na hii ni sawa na kudharau wengi na kufikiri ni wewe tu mwenye kujua na wengine wote hawajui.

  Hii ni hatari kabisa na tusifanye makosa kumpa uongozi watu kama hawa wasioheshimu maoni ya wengine. Ukingalia matatizo katika chama tawala na vyama vya upinzani ni pale maoni ya wengi yanapopondwa.

  Nikigusia tu hoja yako, professor ni kiwango cha juu cha msomi. Tulikuwa na Professor amefanya nini cha kukumbukwa. Msomi ni mzuri anapokuwa anapotenda mazuri lakini ujue ni afadhali mjinga mbaya kuliko msomi mbaya. Ni sawa na kisu kikali. Mjinga ni mwoga na hata anapojaribu ni rahisi kumkamata lakini si kwa msomi.

  Ni kweli Lamek hakusoma sana lakini ni msikivu and in my opinion delivers more than Sarungi. Kumbuka mimi nathamini ninachofaidika kutokana na huduma au usomi wako na kamwe siyo una vyeti na madigrii ya juu kiasi gani.

  Kuhusu makao makuu watu wa Shirati mumeonyesha ubinafsi mtupu tu. Maana ya wilaya mpya ni kupeleka huduma karibu na wananchi husika. Mfano mzuri ni wilaya mpya anakotoka Magufuri kwa watu wanaotumia wanaoweza kujivuna kwa vitendo kuwa wamesoma na tukakubali.

  Kuweka makao makuu kwenye perifery ya eneo ni uchaa na tusitoe mahala yalipofanyika makosa kukidhi objective za wakoloni wakati huo badala ya wananchi.

  Hili ndilo somo la leo kwa wan-Rorya.
   
 12. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nawahakikishia Yohana Mashaka anamng'oa Lameck Airo 2015. Jamaa ameshatangaza nia, na viongozi wengi ndani ya chama wanamuunga mkono. Hata na wana magwanda wanamkubali huyu dogo. Ila tu hatuna uhakika atagombea kupitia chama gani
   
 13. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Naona sasa mnaanza kuwa na akili watoto wa Rorya. Naombeni woote mnaotoka rorya tujiunge pamoja sasa through Rorya Development Initiative (RDI) ili tuweze kuongelea ustawi wa jamii yetu na siyo kuwaachia hawa wendawazimu 2 mustakabali wa eneo letu.
   
 14. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa yenyewe ni ndefu inachosha hata kusoma, Pamoja na malalamiko yote hayo eti Mbunge wao bado ni CCM kama si ujinga nini, jambo lingine la kujiuliza hivi wapinzani walikata rufaa????? Chakushangaza ni kwamba Mbunge mwenyewe hajawahi kuuliza swali Bungeni tangu alipokula kiapo.
   
 15. cheze

  cheze JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
  Omera hii kitu ni problem ya wanarory kurubuniwa na hao kina Lameki na ochele kwa kupewa TAKRIMA,haiwezekani kuwachagua viongozi kwa kuzingatia uwezo wa fedha na mali walizonazo. Wanaroya wanaitaji KUELIMISHWA na KUELEWESHWA juu ya MABADILIKO..

  Hili jimbo limekuwa likitawaliwa na CCM kwa muda sasa achilia mbali Marando ambaye pia hakufanya lolote..Barabara ni zavumbi,shule za msingi na sekondari ni chache, hazina walimu na vifaa vya kufundishia,huduma za zahanati,mawasiliano,posta na benki ndo usiseme.
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  wivu kitu kibaya sana
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Habari ya Rorya ni nzito nitakuja baadaye .Mleta mada nitafute kwa PM tujipange tafadhali .
   
 18. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu pamoja na aya zako kumi na moja ndefu sana, mimejitahidi kusoma mara nne lakini kuna mambo ya msingi manne naomba ufafanuzi tafadhali sana:-
  1. Aliyeteuwa makao makuu ya wilaya ya Rorya kwa kumbukumbu zangu alikuwa Rais kikwete, baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya madiwani wenu, sasa unasema Airo ali honga ili makao hayo yawe pale yalipo yaani Ingri juu; Je una maana Airo alimuhonga Kikwete ndipo akatangaza Ingri juu kuwa Makao Makuu ya Rorya?
  2. Unasema katika mpeni za Ubunge 2010; Airo alisema kuwa "Elimu ni kelele" na hivyo kwa tafsiri yako una maana alibeza swala la elimu, hakika nakubaliana na tafsi yako lakini nataka kujuwa ilikuwaje pamoja na hayo yote bado mkampa kura za ushindi? Kwanini hamkumnyima Ubunge?
  3. Pia umesema jina la Diwani aitwaye Ochere halikuwemo katika majina mawili yaliyopitishwa na CCM makao makuu kwa ajili ya Uwenyekiti wa Halmashauri ya Rorya, ila lilirudishwa kwa shinikizo la Airo na hasa pale alipotishia kujiengua ubunge na hata kurudisha kadi ya CCM ndipo CCM wakarudisha hilo jina; sasa huoni kuwa CCM haijali wananchni wa Rorya na kuwa haijali maskini bali inajali matajiri na watoa rushwa zaidi, swali kwanini msijitoe CCM na kuanzisha kambi ya CDM hapo Rorya?
  4. Swali la Mwisho, Je mpo tayari kutoa ushindi wa hizo kata tatu kwa CDM?
  Naomba ufafanuzi tafadhali sana kabla sijaanza kutoa mchango wangu juu ya kuwasaidia kujinasuwa na huo ukoloni mliopewa na CCM.
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wajaluo wanaibomoa Rorya. WAjaluo wanadhani wao pekee ndio wakazi wa Rorya wanayapuuza makabila mengine kama Wakeloni, Wasuba, Wakurya, Wahasha, Wasimbiti, Wakene, Wasweta, nk.

  Huyu Lameck Aiyiro ndio alikuwa anawatukana wasomi kwamba wasomi wamesoma lakini wanambebea briefcase wakati anapanda ndege kwenda ulaya (Kuna kaukweli lakini)!! Lameck na Ochelle ni wa kupigwa mawe.

  Lameck hajawahi kuchangia hata siku moja huko bungeni tangia achaguliwe kuwa mbunge; hawezi kuchangia kwa kuwa hajui nini kinaendelea bungeni!! Watu walidhani pesa za Lameck ndizo zitapeleka maendeleo Rorya kwa kuwadanganya kwa vitu vidogo.

  Kama alikuwa na pesa za kupeleka maendeleo bila serikali angepeleka tu bila kugombea ubunge ili mwingine apate ubunge akaibane serikali ipeleke maendeleo huko rorya.

  Afadhali wachague mtu mwingine 2015 hawa wengine warudi kwa wajomba zao huko nchi jirani.
   
 20. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  M.M. for 2015
   
Loading...