Jamani nitumie mbinu gani kupata mfuko mmoja wa Mbolea ya kukuzia?

CAMANGA

Member
May 14, 2023
53
259
Yaani ukisikia kufikiria mpaka kufika kwenye bar ndo huku

Mwenzenu Nina heka nne za mahindi na Mungu kanisaidia mahindi yako vizuri natamani nipate mfuko mmoja wa MBOLEA nikuzie angalau hekta moja tu ili Nije nivune mazao yakuridhisha

Lakini Kila namna ninayofikiria ya kupata pesa siioni aisee

Jamani nisaidieni huko wapendwa
 
Mi mwenyewe hapa nautafuta, naambiwa kama sijajiandikisha nitauziwa 140,000 badala ya 70,000. Naona sipo katika mpango wa ruzuku kwa wakulima kuuziwa mbolea kwa bei nafuu, ngoja ninunue tu kwa hiyo bei ya juu kwa mfuko mmoja.
 
Hii serikali yetu nayo ya ajabu, sasa kama inatangaza BBT kwa vijana kujiingiza katika kilimo kwa nini isi regulate bei ya mbolea iwe rahisi kuinunua vijana tujiingize katika kilimo tuzalishe mazao ya kilimo ya kutosha?

Tumejiingiza kwenye kilimo ila tatizo ni bei kubwa ya mbolea ni kikwazo kwenye kilimo. Tunatumia gharama kwenye mbegu usipoweka mbolea unavuna kidogo inakuwa ni hasara tupu mazao hayastawi vizuri
 
Hii serikali yetu nayo ya ajabu, sasa kama inatangaza BBT kwa vijana kujiingiza katika kilimo kwa nini isi regulate bei ya mbolea iwe rahisi kuinunua vijana tujiingize katika kilimo tuzalishe mazao ya kilimo ya kutosha? Tumejiingiza kwenye kilimo ila tatizo ni bei kubwa ya mbolea ni kikwazo kwenye kilimo. Tunatumia gharama kwenye mbegu usipoweka mbolea unavuna kidogo inakuwa ni hasara tupu mazao hayastawi vizuri
Kwenye bei ya mbolea serikali imejitahidi pakubwa sanaaaaaa,
Inatoa ruzuku kubwa sanaa
 
Yaani ukisikia kufikiria mpaka kufika kwenye bar ndo huku

Mwenzenu Nina heka nne za mahindi na Mungu kanisaidia mahindi yako vizuri natamani nipate mfuko mmoja wa MBOLEA nikuzie angalau hekta moja tu ili Nije nivune mazao yakuridhisha...
2007-2020 tulikuwa tunapata mbolea popote karibu na makazi yetu tena kwa bei bwerere mara ghafla akajitokeza chizi mmoja akaleta ujuaji wake leo tuko hapa.

Mungu ikikupendeza chukua na hawa.
 
Back
Top Bottom