Jamani nishaurini, nile au nisile...?

Jamani nishaurini, nile au nisile...?

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,438
Wakuu, niko huku Masaki Chole Road karibu na tpsf, nina kikao na kampuni moja ya Wachina, sasa huyu binti wa kichina kaniandalia Chai ya kichina yaani imeungwa na tu vijani tubichi na kaniletea tuvitu flani tumekaa kama tambi lakini kama tuna vijicho halafu vikavu ananiambia ni bites za kichina na kuna tuvitu flani vimefanana na tende lakini mwe navifananisha na mende hivi.....

Mh, mwenzenu hapa nimepatikana....

Niko chooni hivi sasa naweka hii post nasubiri mnijibu kabla sijarudi kwenye kikao, yaani muafrika niko peke yangu halafu nimezungukwa na Wachina watano.

Hebu gfsonwin, watu8, Asprin, snowhite, nivea, Lisa, Eiyer, cacico, Ruttashobolwa, madamu B, Paloma, KakaKiiza, Fidel80, Filipo, Kaizer, marejesho, amu, Mungi, Preta, sweetlady, FirstLady, nyumba kubwa, BADILI TABIA, Mwita Maranya, Nyamayao lara 1 na wale wanaojua menu za kichina waje hapa kunipa maushauri kabla sijala kharamu..............
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kunywa tu hiyo chai haina madhara ingawa sijui kama utaipenda ladha yake maana huwa hawaweki sukari...
 
Ni kweli mkuu, nimeulizia sukari wakanicheka..............
Lakini wenyewe wamedai eti wameniandalia hiyo makitu na kwa mila zao huandaliwa kwa mtu muhimu sana na wanayemthamini, sasa nisipokula si noumer?
 
Haina hatari yoyote, kama wao wanaheshimu mila zao waambie nawe waheshimu za kwako....wangekuandalia ugali na nguru.
 
Jamani niko kikazi na nina kikao na hawa jamaa jioni hii ambapo tukitoka tutakuw ana Dinner kwenye Chinese Restaurant

kunywa maji tu kama vipi... ukianza kuendesha bila leseni usiseme hatujakuonya.
 
kama wewe ni ustaadh huko restaurant kwenye kuagiza nyama hakikisha unasema Beef, mchina ukimtajia jina nyama tu,ye hudhani ni Pork...
 
kunywa maji tu kama vipi... ukianza kuendesha bila leseni usiseme hatujakuonya.

Hapo kwenye kuharisha ndo noumer na kesho nasafiri kikazim kwenda ZNZ si kitanuka au hizi charter zina toilet?
 
Ni kweli mkuu, nimeulizia sukari wakanicheka..............
Lakini wenyewe wamedai eti wameniandalia hiyo makitu na kwa mila zao huandaliwa kwa mtu muhimu sana na wanayemthamini, sasa nisipokula si noumer?

Kula halafu ukimaliza wahi toilet ukatapike...
 
Wakuu, niko huku Masaki Chole Road karibu na tpsf, nina kikao na kampuni moja ya Wachina, sasa huyu binti wa kichina kaniandalia Chai ya kichina yaani imeungwa na tu vijani tubichi na kaniletea tuvitu flani tumekaa kama tambi lakini kama tuna vijicho halafu vikavu ananiambia ni bites za kichina na kuna tuvitu flani vimefanana na tende lakini mwe navifananisha na mende hivi.....

Mh, mwenzenu hapa nimepatikana....

Niko chooni hivi sasa naweka hii post nasubiri mnijibu kabla sijarudi kwenye kikao, yaani muafrika niko peke yangu halafu nimezungukwa na Wachina watano.

Hebu gfsonwin, watu8, Asprin, snowhite, nivea, Lisa, Eiyer, cacico, Ruttashobolwa, madamu B, Paloma, KakaKiiza, Fidel80, Filipo, Kaizer, marejesho, amu, Mungi, Preta, sweetlady, FirstLady, nyumba kubwa, BADILI TABIA, Mwita Maranya, Nyamayao lara 1 na wale wanaojua menu za kichina waje hapa kunipa maushauri kabla sijala kharamu..............

Kabla hujakunywa pga majeshi ya gwajima..
 
Last edited by a moderator:
Kula halafu ukimaliza wahi toilet ukatapike...

Aaaaaghh............
Mimi hawa jamaa ni hii kazi tu, halafu ndio watu ninaotakiwa nifungamane nao kikazi, mbona hii kazi itanishinda...........
 
heheheeee ukibugi hamia china meeen
hivi ushawahi onja mchina?

NImetuonja, tunaonekana tutamu, lakini hutu tulitofanana na mende wala sigusi, nimeomba juisi badala ya chai...
 
Back
Top Bottom