kaburunye
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 672
- 74
Wanajamvi naombeni ushauri wenu nifanye nini. Wiki iliyopita traffic mmoja alinikamata kwa kuwa road licence ya kigari changu ilikuwa imeisha. Akaniambia ananipeleka kituoni na tulipofika kituo cha mabasi cha salender akasema nipaki pembeni. Baada ya maongezi ya hapa na pale na kuonekana kuwa mazingira ya mimi kutoa rushwa ni magumu basi akachukua leseni yangu na akaniandikia notification ili nikalipe faini na baadae nimletee risiti anirudishie leseni yangu. Kwa sasa ndo nimepata pesa ya kulipia road licence (mwisho wa mwezi) na nataka kesho nikakate. Mpango wangu ni kuwa nikishakata road licence nimwibukie traffic anipe leseni ila nahisi atanidai risiti ya faini ambayo kwa kweli siko tayari kuilipa baada ya kuwa nime-renew road licence yangu. Wadau mnanipa mbinu gani ya kiufundi ili huyu traffic nimfunge goli la mkono??