PCCB hizi rushwa za barabarani mnazuia vipi?

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,585
1,883
Leo nimekutana na issue ya kukarahisha sana ikabidii niulize maswali yakinifu ili nipate suruhisho ya tatizo lililonikuta sababu kwa tafakuri yangu ya kina na kwa jinsi mambo yalivyo nyooka nimeshangaa kuona Bado Kuna taratibu za kuombwa Rushwa hata kwa watumishi wa serikalini na kibaya zaidi hata kwenye sector na nyanja zinazo husisha kukuza mfuko wa serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Leo nikiwa natoka mihangaikoni nawahi kwenda moja kati ya ofisi za mjini nilipita njia ya morogororo road, nikiwa kwenye taa za fire baada ya kituo Cha jangwani nilisimamishwa na maofisa walio jitambulisha kwamba wao ni watumishi wa Tambaza waliopewa jukumu la kukamata pikipiki zisizo na kibali Cha kuingia mjini.

Well natumia pikipiki sana Kama moja ya sehemu za usafiri binafsi lakini pikipiki yangu haikuwahi kuwa na kibali husika Cha kuingia mjini.

Sasa wakati napita hapo nilisimamishwa na Hawa maofisa wa jiji na kuombwa kibali hicho. Sikukahidi nikasema aisee sina hicho kibali je Kama sina hicho kibali na nahitaji kuingia mjini in this rush hour traffic naweza kulipa fine?

Jamaa walisema naweza lipa fine na Kama ntalipa fine papo kwa hapo ntalipa 50,000 lakini Kama wakipeleka yard ntalipishwa 75,000. Nikasema naomba nilipe nipewe RISITI niondoke sababu nina haraka sina namna nitaacha pikipiki hapa.

Nikipozungumza swala la kulipa fine nikaona hao maofisa wamenibadilikia kwamba machine ya EFD haiko sawa kwahiyo lazima gari iende yadi nikalipe 75,000.

Wakati nikifanya process za kutaka kukimbilia ATM nikatoe pesa nilipe Kuna askari wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye namba za usajiri E 2629 akaniomba nimalizane nao kimjini mjini kwamba ananiombea nisaidiwe. Kwamba nasaidiwa kwa kutoa Rushwa?.

Mkuu Eugin wa kituo Cha msimbazi je hivi ndivyo ulivyowapa majukumu vijana wako wanaozunguka na hii Noah

Nilipo goma kufanya hivyo nikaona napandishiwa sauti na baadhi ya maofisa.

Rai yangu kwako Mstahiki Mayor, Mkuu wa Mkoa na Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli, je? kwa mifumo ya tenda zinazotolewa kwenye kampuni Kama hizi kuhakikisha zinachochea ongezeko la mapato nchini Kwa RUSHWA Hizi tufafika kokote?.

Kama swala ni ukusanyaji wa mapato kwanini pikipiki kabla hazijauzwa au kupewa usajiri wowote ule kusiwe na mfumo ambao lazima pikipiki ilipiwe vibali kama hivi? Kuepusha usumbufu Kama huo, mfano mfumo uliotumika kulipia insurance?. Sababu kwa kufanya hivi itasaidia kuongeza mapato bila nguvu kubwa ya kuipa jukumu kampuni binafsi. upotevu wa mapato usio na tija unasababisha na kampuni hizi zinazopewa tenda ya ukusanyaji mapato lakini mwisho uishia huku.

Sawa naelewa kwamba pikipiki ni moja ya vyanzo vya mapato katika bandari yetu pendwa pia uingizaji wa spare parts zake unaonesha namna gani hii ni something, zimeleta ajira kwa vijana wengi lakini kwanini kusiwe na mifumo inayolenga kuhepuka cost na kutoruhusu upotevu wa mapato unaosababiswa na watu wasio na uchungu na upotevu wa mapato haya kwa kujali kujinufahisha wao.


KWELI KAMA TAIFA TUMESHINDWA KUZUIA RUSHWA??.
 
Naomba uwaanike hapa either kwa majina au chochote kitakachofanya watambulike ungeainisha japo namba ya huyo askari
 
Back
Top Bottom